SWALI: Kwanini wanawake na waislamu wanakadiriwa kuajiriwa zaidi na Utumishi(PSRS)?

SWALI: Kwanini wanawake na waislamu wanakadiriwa kuajiriwa zaidi na Utumishi(PSRS)?

Vita dhidiyaujinga

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2026
Posts
279
Reaction score
385
Habari,..swali langu linaendelea kwa kuangalia takwimu za ajira za ivi karibuni (recent placements) za sekretarieti ya ajira.

Kwa majina ya walioitwa kazini hasa uwalimu wa masomo ya Kiswahili,Kingereza,Historia (hasa Kiswahili)ambayo ndiyo nimeifatilia kwa sehemu kubwa inaonekana kundi la wanawake na waislamu wameajiriwa zaidi.

SWALI linaendelea..1.je, wanawake na waislamu ndio wanaweledi mkubwa wa kufaulu saili (interviews) za sekretarieti ya ajira?
2.Je, wanawake na waislamu ndio wameonekana watendaji wazuri kwa tafiti za kiutendaji za ivi karibuni (recent proper employees analysi)?

3.Je,ni upendeleo juu ya wanawake na waislamu,?
4.Je wanawake na waislamu ndio wanaoomba ajira kuliko makundi mengine ambayo hayajatajwa?
5.Je, ni changamoto za kimfumo pengine ajira zinatolewa randomly?
 
Wanawake wanapewa vipaumbele zaidi katika ajira hizo za hao Jamaa, Ukilingana alama na mwanamke Jua Huna chako halafu kutokana na idadi kubwa ya waombaji Jua Tu lazima mtalingana alama, hata hivyo Kwa ujumla bado wanaume wanaendelea kuwa wengi katika suala zima la kupata kazi. Kama umekosa Fanya shughuli nyingine za Ndoto yako.
 
Weka ushahidi. Kama Hakuna ushahidi nashauri ujiandae vizuri na usaili ili round ijayo ufanye vizuri
 
Habari,..swali langu linaendelea kwa kuangalia takwimu za ajira za ivi karibuni (recent placements) za sekretarieti ya ajira.

Kwa majina ya walioitwa kazini hasa uwalimu wa masomo ya Kiswahili,Kingereza,Historia (hasa Kiswahili)ambayo ndiyo nimeifatilia kwa sehemu kubwa inaonekana kundi la wanawake na waislamu wameajiriwa zaidi.

SWALI linaendelea..1.je, wanawake na waislamu ndio wanaweledi mkubwa wa kufaulu saili (interviews) za sekretarieti ya ajira?
2.Je, wanawake na waislamu ndio wameonekana watendaji wazuri kwa tafiti za kiutendaji za ivi karibuni (recent proper employees analysi)?

3.Je,ni upendeleo juu ya wanawake na waislamu,?
4.Je wanawake na waislamu ndio wanaoomba ajira kuliko makundi mengine ambayo hayajatajwa?
5.Je, ni changamoto za kimfumo pengine ajira zinatolewa randomly? "

vita dhidiyaujinga".
 
Kuwa mvumilivu mkuu, kila Kaya itatoa muwakilishi katika ajira za utumishi.
 
Sina Ajira, ila Ualimu hapana nilikataa kabisa. Na endapo ningesoma ualimu, ningekua kwenye Ajira pindi tu nilipomaliza.
 
Nina degree bado sijaupload vyeti ajira portal
Nataka kuweka cheti cha form Four na cheti cha udereva
Niombe kama dereva kuepuka compensation ya degree baada ya hapo.
Nitafanya recategorization
 
Back
Top Bottom