Swali la Kiimani & Sayansi:- Kwanini watu hawapati stroke (kupigwa na majini) kwenye vyoo vya umma?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328
Ni kawaida sana kwa watu kupatwa na stroke wakiwa kwenye vyoo vya majumbani kwao.

Lakini sio kawaida hata kidogo kukuta mtu kapatwa na stroke kwenye vyoo vya umma.

Kwanini Hali hii utokea hivi?
 
Ujaona mwaka juzi tulimzika mshikaji alidonda kwenye vyoo vya umma.

Sio kila kitu dunia hii utafahamau
 
Ni kawaida sana kwa watu kupatwa na stroke wakiwa kwenye vyoo vya majumbani kwao.

Lakini sio kawaida hata kidogo kukuta mtu kapatwa na stroke kwenye vyoo vya umma.

Kwanini Hali hii utokea hivi?
Ngoja waje wajuvi😃😃😃😃. Hili swali linataka majibu haswa na ni swali gumu.
 
Asilimia kubwa ya wanaodondoka huwa ni bafuni na sio chooni, tuogapo tujitahidi kutumia maji angalau ya uvuguvugu na hata kama yakiwa ni baridi basi tuanzie kuoga miguuni kupanda juu

Mtanishukuru baadae, sio kila kitu ni ushirikina kuna mda mwili unakuwa na joto ww unatumia maji ya baridi tena unaanza kichwani, yaani ni kama vile umeipua sifuria jikoni mda huo huo ukataka kulipoza na maji
 
Uko sahihi sana sana sana. Tatizo akili zilishalisha matango pori. Kuja kubadilika inahitaji nguvu ya ziada.
 
Swali batili na majibu yatakuwa batili.

Swali limeanza moja kwa moja kuhusisha stroke na majini kama vile kitaalamu stroke husababishwa na majini.
Pia ingefaa kueleza maana ya stroke unayoikusudia.
 
Ni kawaida sana kwa watu kupatwa na stroke wakiwa kwenye vyoo vya majumbani kwao.

Lakini sio kawaida hata kidogo kukuta mtu kapatwa na stroke kwenye vyoo vya umma.

Kwanini Hali hii utokea hivi?
Ushasema habari za majini, kama ni habari za majini maana yake unaongelea tawi la uchawi. Mchawi anawezaje kukupata kwenye choo cha umma ilhali unaingia huko mara moja kwa mwaka!

Ni rahisi yeye kukupata kwenye choo chako au choo cha nyumba ya kupanga , ni rahisi kutambua ratiba yako ya kuingia chooni kwenye choo chako au choo cha nyumba ya kupanga kuliko kwenye choo cha umma (vyoo vya stendi).

Huwezi kumvua papa (samaki) wa baharini kwa kumtega kwenye madimbwi ya maji. Kwani ukitaka kununua changudoa wa bei powa si lazima uende maeneo wanapopatikana (wanaposimama) kuliko kwenda kuhangaika kumtafuta kwenye nyumba ya ibada.
 
Back
Top Bottom