Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,135
- 48,827
Nimeuliza makusudi ili nipate ufafanuzi .
Kuna fungu lolote kutoka serikalini linatengwa na kuingizwa kwenye akaunti ya TFF ? Nakumbuka wakati wa FAT ya Muhidin Ndolanga , FIFA ilipiga Marufuku kwa serikali kuingilia masuala ya soka , sasa siku hizi FIFA wamebadili msimamo wao ?
Je hela zile ni za Umma ama ni mchango wa FIFA kwa TFF ?
Sawa mkuu nakuelewa vizuri sana, ila usichukie na wala usichoke kurudi tena. Swali langu ni hili, umesema ni makosa binafsi wameyafanya Malinzi na Mwesiga, je wameyafanya wakiwa kwenye nyadhifa zao au?
Na kam wameyafanya wakiwa madarakani, Je ni nani alienda kuwashitaki takukuru? Na takukuru ushahidi wao atauleta nani mahakamani?
Maana sitaki kwenda mbali sana. Hii kesi ndani yake inautakatishaji fedha, sielewi vizuri hii money rounderin inakaaje, ila kwa uelewa mdogo ni kuzichukua hela halamu ukazifanya kuwa halali
mfn: ndio ule wa madawa ya kulevya kupata hela, kuziingiza bank nakuzitoa tena, hapo umezitakatisha. Sasa basi hao akina Malinzi mametakatishaje? Rudi mkuu, tafadhali. Kuna maswali mengi yasio na majibu.
mkuu, mimi naona depending on legal interpretation, hii issue inaweza kusababisha Tz kufungiwa kwani masuala ya football (be it technical or administrative) hayatakiwi kupelekwa mahakamani.
mkuu Petro E. Mselewa unasemaje?
Sahihi mkuu,kuna kijana tunaishi nae jirani alikuwa miongoni mwa wa kikosi kile,alituambia hicho unachokisema. Waliambiwa fedha imeisha,Mkuu kuna watu wapuuzi sana, mimi nilifika kwa yule nahodha anaishi mazingira magumu sana, anasema walipewa nauli na fedha ya kula njia hawajalipwa posho wote. Ina maana fedha zote zilizotolewa na Serengeti jamaa katia ndani ili kujiandaa na uchaguzi.
Ila wizi wa fedha za TFF ni kazi ya FIFA?Asprin mbona unakurupuka sana, mifano yako ni hovyo sana. Kuua sio kazi ya FIFA au umechangia tu kuonekana upo?
Swali lenye akili sana...Fifa walimchangia Malinzi na Cargo Star au Tanzania Football Federation?
Unajua kama una akili ndogo, acha akili kubwa zifanye kazi.Ila wizi wa fedha za TFF ni kazi ya FIFA?
Au umechangia ili uonekane unajua kusoma na kuandika?
Afadhali umesaidia kuiweka vizuri zaidi.Swala tu sio kuwa pesa za Umma, hata mtu binafsi pesa zake zikitumika visivyo mf kuibiwa nk, polisi wataingia kazini na baadaye mahakama. Pesa za TFF ziwe za umma au zisiwe ili mradi kuna kosa limefanyika lazima washughulikiwe. Haya mambo ya kuanza kuhoji kama pesa ni ya umma au la yametoka wapi? Kosa ni kosa!
Akili ndogo ndo kama hizi zinazohalalisha wizi wa fedha za watanzania kwa ajili ya kuendeleza soka la watanzaniaUnajua kama una akili ndogo, acha akili kubwa zifanye kazi.
1.Hayo waliyafanya wakiwa kwenye nyadhifa ndio maana ikasemwa ni matumizi mabaya ya ofisi. Yaani kwa kuwa ndani ya zile ofisi waliweza kuwa na access ya accounts za TFF na wakafanya wanayotaka kwa manufaa yao na sio ya taasisi.Sawa mkuu nakuelewa vizuri sana, ila usichukie na wala usichoke kurudi tena. Swali langu ni hili, umesema ni makosa binafsi wameyafanya Malinzi na Mwesiga, je wameyafanya wakiwa kwenye nyadhifa zao au?
Na kam wameyafanya wakiwa madarakani, Je ni nani alienda kuwashitaki takukuru? Na takukuru ushahidi wao atauleta nani mahakamani?
Maana sitaki kwenda mbali sana. Hii kesi ndani yake inautakatishaji fedha, sielewi vizuri hii money rounderin inakaaje, ila kwa uelewa mdogo ni kuzichukua hela halamu ukazifanya kuwa halali
mfn: ndio ule wa madawa ya kulevya kupata hela, kuziingiza bank nakuzitoa tena, hapo umezitakatisha. Sasa basi hao akina Malinzi mametakatishaje? Rudi mkuu, tafadhali. Kuna maswali mengi yasio na majibu.
Hivi,huyo aliyemlipa Nyonzima, (Kama ni kweli) halafu akaja kuuzwa kwa bei ya mara nne ya aliyonunuliwa. Je huyo aliyetoa hiyo hela,hana haki ya kuchukua hiyo fedha?Hata za Simba ni za umma wa wana Simba
mkuu taratibu basi.Mbona UEFA haijafungiwa? Kajifunzw kutoka kwenye sakata la Blatter na Platin. Msiwe wavivu kujifunza.
Unaruhusiwa kusema hayo mkuu..Tukumbuke kwamba mpaka muda huu Jamal Malinzi bado ni mtuhumiwa tu , na msije kushangaa akaja kubainika hana kosa lolote.
Kwahiyo tunapochangia tusiweke na hukumu ambayo haijasomwa .