Swali la kizushi - Je Pesa za TFF zinazodaiwa kupigwa na Malinzi ni Mali ya Umma ?

Swali la kizushi - Je Pesa za TFF zinazodaiwa kupigwa na Malinzi ni Mali ya Umma ?

Nimeuliza makusudi ili nipate ufafanuzi .

Kuna fungu lolote kutoka serikalini linatengwa na kuingizwa kwenye akaunti ya TFF ? Nakumbuka wakati wa FAT ya Muhidin Ndolanga , FIFA ilipiga Marufuku kwa serikali kuingilia masuala ya soka , sasa siku hizi FIFA wamebadili msimamo wao ?

Je hela zile ni za Umma ama ni mchango wa FIFA kwa TFF ?

Katafute sakata la Blatter na Platin.
 
Sawa mkuu nakuelewa vizuri sana, ila usichukie na wala usichoke kurudi tena. Swali langu ni hili, umesema ni makosa binafsi wameyafanya Malinzi na Mwesiga, je wameyafanya wakiwa kwenye nyadhifa zao au?

Na kam wameyafanya wakiwa madarakani, Je ni nani alienda kuwashitaki takukuru? Na takukuru ushahidi wao atauleta nani mahakamani?

Maana sitaki kwenda mbali sana. Hii kesi ndani yake inautakatishaji fedha, sielewi vizuri hii money rounderin inakaaje, ila kwa uelewa mdogo ni kuzichukua hela halamu ukazifanya kuwa halali

mfn: ndio ule wa madawa ya kulevya kupata hela, kuziingiza bank nakuzitoa tena, hapo umezitakatisha. Sasa basi hao akina Malinzi mametakatishaje? Rudi mkuu, tafadhali. Kuna maswali mengi yasio na majibu.

Ndio wamefanya wakiwa kwenye nyadhifa zao.

Takukuru wanafatilia biashara na shughuli zote zinazofanywa hapa nchini,pesa yako ikiingia kwenyw account yako kama haeleweki lazima takukuru waitwe wafanya uchunguzi.

Takukuru ndio walifungua mashtaka na ndio wanafanya uchunguzi na ushaidi utatoka kwao.

Ni Money Laundering,Malinzi alijiingizia pesa kwa njia ya wizi. Aliiba pesa za TFF kwa kisingizio kuwa ameokopesha TFF wakati hajaikopesha. Katumia njia haramu kujipatia pesa.
 
mkuu, mimi naona depending on legal interpretation, hii issue inaweza kusababisha Tz kufungiwa kwani masuala ya football (be it technical or administrative) hayatakiwi kupelekwa mahakamani.

mkuu Petro E. Mselewa unasemaje?

Mbona UEFA haijafungiwa? Kajifunzw kutoka kwenye sakata la Blatter na Platin. Msiwe wavivu kujifunza.
 
Money Laundering no term pana kisogo..UTAKATISHAJI WA FEDHA...
kuna tetesi kwamba, yote ya kuhusu viongozi wa soka yanayoendelea sasa pamoja na mambo mengine, issue ya ESCROW inatajwa kuwaibua.
Money Laundering (kesi) inaweza kumhusu yeyote iwapo itaonekana umepokea fedha kutoka kwenye vyanzo visivyoeleweka au kutoka kwenye chanzo kinachotuhumiwa kufanya biashara haramu.
 
Mkuu kuna watu wapuuzi sana, mimi nilifika kwa yule nahodha anaishi mazingira magumu sana, anasema walipewa nauli na fedha ya kula njia hawajalipwa posho wote. Ina maana fedha zote zilizotolewa na Serengeti jamaa katia ndani ili kujiandaa na uchaguzi.
Sahihi mkuu,kuna kijana tunaishi nae jirani alikuwa miongoni mwa wa kikosi kile,alituambia hicho unachokisema. Waliambiwa fedha imeisha,
 
Toka TFF hadi Simba sc, mpaka Ndondo fc.
Uhakiki wa matumizi ya pesa unaendelea.
Tukimaliza huko,
tunaanza uhakiki,
Makanisani,
Misikitini na nyumba zote za ibada.
Ilimradi tu kama zitakuwa na usajiri toka serikalini.

Kazi ndo kwanza imeanza.
 
Asprin mbona unakurupuka sana, mifano yako ni hovyo sana. Kuua sio kazi ya FIFA au umechangia tu kuonekana upo?
Ila wizi wa fedha za TFF ni kazi ya FIFA?

Au umechangia ili uonekane unajua kusoma na kuandika?
 
Swala tu sio kuwa pesa za Umma, hata mtu binafsi pesa zake zikitumika visivyo mf kuibiwa nk, polisi wataingia kazini na baadaye mahakama. Pesa za TFF ziwe za umma au zisiwe ili mradi kuna kosa limefanyika lazima washughulikiwe. Haya mambo ya kuanza kuhoji kama pesa ni ya umma au la yametoka wapi? Kosa ni kosa!
Afadhali umesaidia kuiweka vizuri zaidi.
Maana alitaka kujenga dhana kwamba eti kama zimetoka FIFA au ni za Club siyo za serikali per se, basi watu wafanye wayatayo. Haitkuwa nchi, bali vurugu!
 
Unajua kama una akili ndogo, acha akili kubwa zifanye kazi.
Akili ndogo ndo kama hizi zinazohalalisha wizi wa fedha za watanzania kwa ajili ya kuendeleza soka la watanzania
 
Sawa mkuu nakuelewa vizuri sana, ila usichukie na wala usichoke kurudi tena. Swali langu ni hili, umesema ni makosa binafsi wameyafanya Malinzi na Mwesiga, je wameyafanya wakiwa kwenye nyadhifa zao au?

Na kam wameyafanya wakiwa madarakani, Je ni nani alienda kuwashitaki takukuru? Na takukuru ushahidi wao atauleta nani mahakamani?

Maana sitaki kwenda mbali sana. Hii kesi ndani yake inautakatishaji fedha, sielewi vizuri hii money rounderin inakaaje, ila kwa uelewa mdogo ni kuzichukua hela halamu ukazifanya kuwa halali

mfn: ndio ule wa madawa ya kulevya kupata hela, kuziingiza bank nakuzitoa tena, hapo umezitakatisha. Sasa basi hao akina Malinzi mametakatishaje? Rudi mkuu, tafadhali. Kuna maswali mengi yasio na majibu.
1.Hayo waliyafanya wakiwa kwenye nyadhifa ndio maana ikasemwa ni matumizi mabaya ya ofisi. Yaani kwa kuwa ndani ya zile ofisi waliweza kuwa na access ya accounts za TFF na wakafanya wanayotaka kwa manufaa yao na sio ya taasisi.

2. Umeuliza nani aliwashtaki. Kwa kifupi kesi yoyote ikishaonekana kuwa ni jinai na sio madai, mshitaki ni jamhuri. TAKUKURU ni chombo ambacho kimepewa mamlaka kisheria na jamhuri na ndio chombo pekee ambacho FIFA wameruhusu kuweza kuingia kazini kwenye maswala ya soka pale inapoonekana kuna tatizo ili kuchunguza makosa ya aina hiyo (Aliekuwa raisi wa FIFA aliepita nae aliwahi kuchunguzwa kwa matumizi mabaya) , wao ndio watachunguza, kukusanya ushahidi na kuufikisha mahakamani.

3. Umeuliza utakatishaji fedha. Fedha yoyote inayobadilishwa mfumo wa uingiaji wake au upatikanaji ambao haukuwa halali uonekane una uhalali kwa namna fulani. Hiyo ni moja kati ya tuhuma zinazowakabili na ndio kosa lililowaletea ugumu wa kupata dhamana. Ukiangalia kuna sehemu jamaa alitaka kuimiliki pesa ya TFF akaghushi nyaraka zaidi ya ishirini kuonyesha kuwa anaidai TFF kwa hy akajiharalishia kubadili umiliki wa pesa ya TFF ionekane ni ya kwake. Na kuna nyingine kibao yeye na Mwesigwa walishirikiana kwa pamoja.

Lakini kuna watu wanahoji ni kwa nini kipindi hiki vha uchaguzi na sio kipindi kingine?
Wakati wowote adui yako huwa anatafuta udhaifu wako ulipo ili autumie kukubomoa. Hayo makosa yalikuwepo na inawezekana PCCB hawakuyashtukia (labda) kwa hiyo watu wakapenyeza taarifa PCCB wakaingia kazini. Ni kama kwenye siasa unapofika wakati wa chaguzi hapo ndio tuhuma za watu zilizojificha zinapoanza kuonekanana kujulikana.
Lakini kosa halichagui muda kusema kwa nini sasa, wakati linapogundulika linafanyiwa kazi na mahakama ndio itatuthibitishia kama wamefanya au la..... Ni swala la kusubiri.
 
Atakuwa ameelewa sasa.. anafikiri wadau wamekaa kimya hawajui kinachoendelea kumbe watu wanafuatilia mchezo kwa karibu
vitendo alivyofanya malinzi ni vya aibu na in dharau kwa serikali na watanzania wote kama atatoka salama basi itakuwa imehalalishwa rasmi watu wapo juu ya sheria
 
Hata za Simba ni za umma wa wana Simba
Hivi,huyo aliyemlipa Nyonzima, (Kama ni kweli) halafu akaja kuuzwa kwa bei ya mara nne ya aliyonunuliwa. Je huyo aliyetoa hiyo hela,hana haki ya kuchukua hiyo fedha?
Na jeee,kuhusu kuikopesha klabu,si pamoja na mishahara walipwayo wachezaji?
 
Tukumbuke kwamba mpaka muda huu Jamal Malinzi bado ni mtuhumiwa tu , na msije kushangaa akaja kubainika hana kosa lolote.

Kwahiyo tunapochangia tusiweke na hukumu ambayo haijasomwa .
 
Tukumbuke kwamba mpaka muda huu Jamal Malinzi bado ni mtuhumiwa tu , na msije kushangaa akaja kubainika hana kosa lolote.

Kwahiyo tunapochangia tusiweke na hukumu ambayo haijasomwa .
Unaruhusiwa kusema hayo mkuu..

Ila ni mimi najua suala la scandal za rushwa kwa mgombea hazijawahi kumuacha mtu salama.
 
Back
Top Bottom