Swali la kizushi kwa Kiranga.


Ngabu usione choyo. Na wewe umo huvumi tu.
 
We only deem miracles as such due to the poverty of our minds.

You nailed it bro!..Hatuwezi fika popote kama tutaendekeza uvivu wa kusoma Kiranga hajatoka Mars! Tushughulishe bongo zetu ili tufikie na kuzidi viwango vyao..!
 

Utanisamehe kama sijakuelewa ila kwenye maelezo yako nimeshindwa kupata conclusion kama yesu alikuwa mtu halisi au hakuwahi kuwepo?
Achilia mbali miujiza na matendo yake and inconsistency zote.
 

Kiranga amekataa kuhusu kuamini,Kiranga achilia mbali kujua kuhusu uwepo wa Mungu,amekataa hata wazo la Kuamini katika kuamini,Kiranga amekueleza jinsi alivyo,wewe unalazimisha kuwa hayupo hivyo,Hoja kama hizi zako ndizo zinazompa kirang nguvu.
 
Last edited by a moderator:
Capt Tamar umenikoti mara nyingi sana,,unachakachua thread
 
Last edited by a moderator:
Ngoja na mimi niongezee idadi ya watu walikukoti.

Duh!! Hii thread ilikuwa tamu mnoooo!nimeichimbua mbali kweli.Samahani mkuu matumbo device yangu ndiyo iliyo nichaakachulia point yangu,mkuu IGWE hii timu yenu ikikaa vizuri hatimaye inaweza ku break the hardshell lililozunguka Imani,asanteni mno for this usefull post.
 
Last edited by a moderator:
Kiranga anamchukia Mungu hana kingine..

Siwezi kumchukia mungu wakati hayupo, na kabla hujaweza kunionesha kwamba mungu yupo, huwezi kusema namchukia.

unapoamua kuondoa kwa makusudi uwepo wa Mungu

Huwezi kuamua kuondoa uwepo wa mungu ambaye hayupo na wala hajathibitishwa kuwepo. Wewe unayesema naamua kuondoa uwepo wa mungu, inakubidi unioneshe kwamba yupo kwanza kabla ya kusema naondoa uwepo wake.

Ama sivyo na mimi nitasema umeondoa dola milioni moja kwenye akaunti yangu, hivyo unanichukia, dola milioni moja ambazo hata hazikuwepo in the first place.

ili hali unajua yupo,

Wewe unajuaje kwamba mimi najua yupo? Umeingiaje kichwani mwangu na kujua hili kiasi hata nikisema sijui kama yupo wewe ujue kwamba najua kama yupo?

Hicho kipimo unachotumia kipimo gani hicho? Maana unaweza kutupatia Mwana JF wa kwanza kupata nishani ya Nobel.

uko ni kumchukia...

Na wewe unanichukia kwa kuwa umeondoa dola zangu milioni moja kwenye akaunti yangu.

yani kisaikolojia ni kwamba kwake uwepo wa Mungu unamsumbua unamgasi na unamnyima uhuru wa kufanya maouvu yake,

Lord Buddha hakuamini katika uwepo wa mungu, lakini alikuwa na discipline ya hali ya juu kuhusu kufanya maovu.

Watawa wa Kikatoliki supposedly wanaamini katika uwepo wa mungu lakini haweshi kuvilawiti vitoto.

Wazee wa makanisa na mashehe kibao tunawaona wanavyopuyanga kama hawana akili nzuri.

Wanaoamini mungu kibao wanauana kwa jina la mungu.

Kuamini mungu hakuzuii maovu, na wala kutoamini mungu hakusababishi maovu.Hasa kwa mtu aliyezisoma dini na kuona mapungufu yake. A lot of secular humanists have higher standards than believers.

Tena hao believers wakitaka kufanya mabaya, kwa mfano kukuua, wanayapa mabaya hayo upako wa utakatifu kwa kutumia jina la mungu, unauawa katika "holy war". Mie nisiyeamini mungu siwezi kuua mtu kwa ujinga wa "holy war".Ntafikiri mara mbili kabla ya kufanya uovu huu, kwa sababu sina mungu wa kumsingizia, najua ni responsibility yangu.

Huna point hapo.

au kuna kitu ambacho anahisi Mungu kamuonea haswa kwenye maumbile..

Speculation juu ya speculation, mimi niko fit.

Na unaleta swali hapa, kama mungu yupo muweza yote na ana upendo wote, kwa nini wengine awaumbe vilema toka wanazaliwa na wengine tuko fit?

sasa ili kujipa uhuru bandia wa kufanya maovu yake

Mimi nimesoma standards za morality zilizo juu ya zaidi ya standards za wanaoamini mungu, kwa nini unafikiri kwamba kuamini mungu ndiyo kipimo cha kutofanya maovu wakati kuna watu ambao hawataki kuamini mungu kwa sababu kuamini mungu kunaruhusu kufanya maovu kwa kuwa na to low standards?

Ukiandika vitu kama hivi unajionesha kwamba ni wazi hujasoma mifumo tofauti ya falsafa na dini za dunia.

Unakuwa ni kama mtu ambaye hajawahi kutoka kijijini kwao, hajajua mambo ya miji ya dunia, anaona kigorofa cha kijijini kile cha ghorofa mbili ndicho kinakuwa ni jengo refu kabisa katika dunia yake.

Huku hajui kuna mighorofa ya ajabu huko kwingine.

Tembea kwanza uone mighorofa ya dunia halafu ndo uweze kusema lipi ni refu duniani.

Akija mtu kuniambia anajua kuhusu secular humanism na kuhusu atheist buddhism, halafu akaniambia hawa watu wana standards zilizo chini ya theists, naweza kujadiliana naye.Wewe sanasana nitakuwa nakutajia vitu ambavyo hujawahi kuvisikia tu kwa mujibu wa maandiko yako yanaonekana.

Utakuwa sawa na yule mdau ambaye kwa vile yeye katika maisha yake yote hajawahi kufikiria kwamba inawezekana hakuna mungu, na hajawahi kusikia kwamba kuna watu hawaamini kwamba mungu yupo, alipokuja kusikia hapa kwamba Kiranga anasema haamini kuna mungu akacheka tu na kuona natania.Itakuwaje nisiamini kuwepo kwa mungu? Katika dunia yake anaona hata hiyo fikra tu haiwezekani. Huyu hana tofauti na wewe.

anajiaminisha Mungu hayupo..

Ntajiaminishaje kwamba mungu hayupo wakati hajathibitishwa kwamba yupo in the first place? Inaonekana kama wewe ndiye unayejiaminisha kwamba mungu yupo, si mimi ninayejiaminisha kwamba mungu hayupo.

Ndiyo maana masuala ya dini na mungu yanaitwa "imani". Get it?

Kusema kwamba mungu yupo ni imani, kusema sijui kama mungu yupo si imani.

au kumkomesha kutokana na mapungufu aliyompa

Mpaka sasa kati yangu mimi ninayekwambia ghorofa lako la sakafu mbili unaliona refu kwa sababu ujatembea kuona mighorofa ya dunia na wewe unayenipa habari zilizofungwa na kukosa kujua habari za dunia nani ana mapungufu?

Have you read the Tripitaka? The Dhammapada? Have you seen the high level of morality in them?

Can you compare the high level of morality in them to the old testament or Quran?

anakomaa kwamba hayupo..

Hujanionesha kwamba yupo.

kwaio kama Mungu hayupo ata zile sheria zake hazina maana sana kwake..

Sheria gani? Hizo za biblia ambazo kila sheria utakayonipa kuna kipengele kingine kinachosema tofauti na kuweza kuipindisha?

Kwa nini nitake kuwa na sheria isiyoeleweka kutoka kwa mungu asiyethibitishika inayoniruhusu kuua kwa mfano (biblia), wakati kuna morality isiyo na complications za mungu ambayo iko wazi tu kwamba kuua hakuruhusiwi?

Sijui umeiona hoja agnostic(wewe sio mkristo)???

Hapa hamna hoja kuna viroja vinavyofanywa kuonekana hoja kutokana na matongotongo ya ushamba yaliyojaa kwenye macho ya baadhi ya watu ambao wanajiingiza katika kujadili mambo makubwa bila hata ya kusoma the basic requirements kwanza.
 
Na wengine washatengeneza mafriji ya kuwahifadhi majumbani mwao mpaka hapo sayansi itakapoweza kujua kwa uhakika kama wanaweza kuhuishwa tena ama la!

This is the level of parochialism we have to confront here!

comment yako hii imenifanya nitafakari mengi.
 
Mungu ana sababu zake za kufanya hivyo i.e. kuumbaya mabaya na ubaya, sababu ambazo sisi wanadamu hatuwezi kuzijua.
Kiranga Mungu ana uwezo wa kuzuia yote haya mabaya,lkn alisema hatauteketeza tena ulimwengu kwa moto wala kwa maji bali kwa magonjwa,njaa na mabalaa.Na anapotoa adhabu hizi watoto wadogo wasio na hatia hawaepekiki sababu ni vizazi vyetu sisi tunaoadhibiwa.
Ni vigumu kunielewa sababu maelezo yangu yanatoka katika Biblia na wewe huamini Biblia.

Pamoja na kuwa ninachokiamini kwa nguvu na akili zangu zote wewe hukuamini kwa nguvu na akili zako zote,nakiri kuwa nakukubali sana katika uwezo wako mkubwa wa kutoa hoja na namna unavyotetea hoja zako kistaarabu.
 
Last edited by a moderator:

Duh,

Unamuongelea Kiranga au "mdogo wake" Nyani Ngabu?

Maana unamtaja Kiranga lakini unam quote Nyani Ngabu
 
Duh,

Unamuongelea Kiranga au "mdogo wake" Nyani Ngabu?

Maana unamtaja Kiranga lakini unam quote Nyani Ngabu

Hahaa usijali mkuu hata sijui ilikuaje nikam-guote Nyani Ngabu
Cha msingi nilichotaka kukwambia kimekufikia.
 
Last edited by a moderator:

Hapo kwenye brown,,,,Nitatafuta ivo vitu nisome,kiukweli sijavisoma bado...


hapo kwenye bluu kuna namna nyingi tu za kuthibitisha uwepo wa Mungu ni ubishi tu na chuki dhidi yake ndio utafanya ukatae,anzia kwenye Ubongo wako unavyofanya kazi ni namna tosha ya kukuthibitishia uwepo wa Mungu,ubongo unavyopokea taarifa,unavyocontrol mwili,unavyopanga mipango yako,unavyowaza,unavyoamua n.k n.k unaweza ona ni kitu kidogo ila ukikaa chini na kutafakari inaweza kuanzia kumtambua Mungu muumba wa vyote kabla ujaenda mbali sana.

Tatizo la nyie wapinga Mungu mnapenda kuthibitishiwa kwa kuonyeshwa kwamba Mungu uyu hapa,kama ukuonyeshwa unasema hayupo...ila unakubali hewa ipo wakati haujaiona.
 


yeah Kiranga yupo vizuri katika kupanga hoja zake,ingekuwa wewe ungemshukuru Mungu kwa neema izo, cha kusikitisha yeye hana wa kumshukuru.
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye brown,,,,Nitatafuta ivo vitu nisome,kiukweli sijavisoma bado...

Kwanza unakubali kwamba hujasoma vitu basic kabisa katika mjadala. Hujajua hata tamaduni nyingine tu zinavyolichukulia suala la mungu.

Which is not a crime.

But if you don't know the basics, don't attempt to argue as if you do!

Which is exactly what you are doing down here.


hapo kwenye bluu kuna namna nyingi tu za kuthibitisha uwepo wa Mungu ni ubishi tu na chuki dhidi yake ndio utafanya ukatae,

Hujanionesha ni vipi kukataa kitu ambacho hakijathibitishwa kunakuwa ni ubishi na chuki tu.

Kwangu mimi ubishi ni kusema kitu kipo, ukaombwa kutoa uthibitisho, ukawa huwezi kutoa uthibitisho na kuendelea kusema tu kwamba kipo.

Na chuki ni kusema mtu mwingine ana chuki kwa sababu tu kakuomba uthibitisho wa kitu ambacho hakina uthibitisho.

Unamchukia kwa sababu hupendi maswali yake, yaliyojikita katika uchunguzi.

Na unafanya kile wanasaikolojia wanachokiita "projection". Unamchukia wewe, halafu unajisahaulisha kwamba unamchukia, unampa jina baya la mchukia mungu si kwa sababu yeye ni mchukia mungu, bali kwa sababu wewe unamchukia yeye huyu Kiranga.

Give a dog a bad name, then kill it.

Kama Gaddafi alivyowaita wa Libya "Qaeda" na Cocroaches. Akawaua.

Au kama Wanyarwanda walivyoitana "cockroaches" kabla ya kuuana.

Hapa kama kuna chuki, ni chuki yako juu yangu. Mimi nauliza maswali ya uchunguzi ambayo huna uwezo wa kuyajibu, ndiyo maana unanichukia, even subconsciously, without fully realizing it. Kama yule mzungu anayesema yeye si mbaguzi wa rangi lakini akimuona mtu mweusi anakuja mbele anavuka barabara kwenda upande wa pili bila hata ya kujijua.

How do you like me now? Or better yet, how do you hate me now?


Wewe unaelewa jinsi ubongo unavyofanya kazi?

Tatizo la nyie wapinga Mungu mnapenda kuthibitishiwa kwa kuonyeshwa kwamba Mungu uyu hapa,kama ukuonyeshwa unasema hayupo...ila unakubali hewa ipo wakati haujaiona.

Hewa inaonekana kwenye vifaa vya kuipima, elements zake zipo kwenye periodic table of elements, mwendo wake unapimika, so that is not an argument.

Hujasema kitu cha kueleweka bado.

Imani ya mungu, mpaka sasa, inaonekana kuwa inatokana na matongotongo ya kukosa elimu tulikorithi kutoka antiquity tu.

Ukichunguza the classic arguments utaona habari nzima ya mungu ni a simplistic attempt at explaining the world, which we do not need anymore as there are better tools of explaining the world, tools that are not perfect, but nevertheless better at calibrating out outlook on the universe than the god idea.
 
yeah Kiranga yupo vizuri katika kupanga hoja zake,ingekuwa wewe ungemshukuru Mungu kwa neema izo, cha kusikitisha yeye hana wa kumshukuru.

Mimi nashukuru genes nzuri za wazazi wangu kama kuna kitu cha kushukuru kwa kuwa na the basic requirements for intellectual promiscuity and natural curiosity.

Inaonekana wewe unataka mungu awepo ili tu uwe na wa kumshukuru regardless kama yupo au hayupo. Kuna watu fulani wana hii Slavic nature, wanapenda kutumikia na kushukuru tu regardless.

Trust me, mimi ningeweza kuji convince kwamba mungu yupo ningefurahi sana.

Kwa nini?

Kwa sababu uchafu wote wa dunia, vita, magonjwa, uonevu, majanga etc, yote haya, kama kayaumba yeye, ultimately yangekuwa mzigo wake. Ingekuwa responsibility yake.

Na usiniambie katupa akili therefore ni responsibility yetu.Kwa sababu hata hizo akili kikomo chake angekuwa kakiweka yeye.

Kwa hiyo mimi ningefurahi sana kama mungu angekuwepo.

Lakini sasa naona hayupo. Mambo yote haya yanakuwa responsibility yangu binadamu.

Kama mvua hainyeshi hamna haja ya kwenda kanisani na kumuomba mungu, tuangalie tunavyokata miti ovyo.

Magonjwa, watu wanaweza kujifunza kuyaponya etc etc.

Mtu asiyeamini mungu ana uwezo mkubwa wa kuyaboresha mazingira yake kuliko anayeamini mungu.

So even as I wish there was a god to take care of everything, this is as much a wishful thinking as that orphan kid who does not have support thinking that his father is Bill Gates.

I would rather deal with he reality than succumb to a good fairy tale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…