Kiranga anamchukia Mungu hana kingine..
Siwezi kumchukia mungu wakati hayupo, na kabla hujaweza kunionesha kwamba mungu yupo, huwezi kusema namchukia.
unapoamua kuondoa kwa makusudi uwepo wa Mungu
Huwezi kuamua kuondoa uwepo wa mungu ambaye hayupo na wala hajathibitishwa kuwepo. Wewe unayesema naamua kuondoa uwepo wa mungu, inakubidi unioneshe kwamba yupo kwanza kabla ya kusema naondoa uwepo wake.
Ama sivyo na mimi nitasema umeondoa dola milioni moja kwenye akaunti yangu, hivyo unanichukia, dola milioni moja ambazo hata hazikuwepo in the first place.
Wewe unajuaje kwamba mimi najua yupo? Umeingiaje kichwani mwangu na kujua hili kiasi hata nikisema sijui kama yupo wewe ujue kwamba najua kama yupo?
Hicho kipimo unachotumia kipimo gani hicho? Maana unaweza kutupatia Mwana JF wa kwanza kupata nishani ya Nobel.
Na wewe unanichukia kwa kuwa umeondoa dola zangu milioni moja kwenye akaunti yangu.
yani kisaikolojia ni kwamba kwake uwepo wa Mungu unamsumbua unamgasi na unamnyima uhuru wa kufanya maouvu yake,
Lord Buddha hakuamini katika uwepo wa mungu, lakini alikuwa na discipline ya hali ya juu kuhusu kufanya maovu.
Watawa wa Kikatoliki supposedly wanaamini katika uwepo wa mungu lakini haweshi kuvilawiti vitoto.
Wazee wa makanisa na mashehe kibao tunawaona wanavyopuyanga kama hawana akili nzuri.
Wanaoamini mungu kibao wanauana kwa jina la mungu.
Kuamini mungu hakuzuii maovu, na wala kutoamini mungu hakusababishi maovu.Hasa kwa mtu aliyezisoma dini na kuona mapungufu yake. A lot of secular humanists have higher standards than believers.
Tena hao believers wakitaka kufanya mabaya, kwa mfano kukuua, wanayapa mabaya hayo upako wa utakatifu kwa kutumia jina la mungu, unauawa katika "holy war". Mie nisiyeamini mungu siwezi kuua mtu kwa ujinga wa "holy war".Ntafikiri mara mbili kabla ya kufanya uovu huu, kwa sababu sina mungu wa kumsingizia, najua ni responsibility yangu.
Huna point hapo.
au kuna kitu ambacho anahisi Mungu kamuonea haswa kwenye maumbile..
Speculation juu ya speculation, mimi niko fit.
Na unaleta swali hapa, kama mungu yupo muweza yote na ana upendo wote, kwa nini wengine awaumbe vilema toka wanazaliwa na wengine tuko fit?
sasa ili kujipa uhuru bandia wa kufanya maovu yake
Mimi nimesoma standards za morality zilizo juu ya zaidi ya standards za wanaoamini mungu, kwa nini unafikiri kwamba kuamini mungu ndiyo kipimo cha kutofanya maovu wakati kuna watu ambao hawataki kuamini mungu kwa sababu kuamini mungu kunaruhusu kufanya maovu kwa kuwa na to low standards?
Ukiandika vitu kama hivi unajionesha kwamba ni wazi hujasoma mifumo tofauti ya falsafa na dini za dunia.
Unakuwa ni kama mtu ambaye hajawahi kutoka kijijini kwao, hajajua mambo ya miji ya dunia, anaona kigorofa cha kijijini kile cha ghorofa mbili ndicho kinakuwa ni jengo refu kabisa katika dunia yake.
Huku hajui kuna mighorofa ya ajabu huko kwingine.
Tembea kwanza uone mighorofa ya dunia halafu ndo uweze kusema lipi ni refu duniani.
Akija mtu kuniambia anajua kuhusu secular humanism na kuhusu atheist buddhism, halafu akaniambia hawa watu wana standards zilizo chini ya theists, naweza kujadiliana naye.Wewe sanasana nitakuwa nakutajia vitu ambavyo hujawahi kuvisikia tu kwa mujibu wa maandiko yako yanaonekana.
Utakuwa sawa na yule mdau ambaye kwa vile yeye katika maisha yake yote hajawahi kufikiria kwamba inawezekana hakuna mungu, na hajawahi kusikia kwamba kuna watu hawaamini kwamba mungu yupo, alipokuja kusikia hapa kwamba Kiranga anasema haamini kuna mungu akacheka tu na kuona natania.Itakuwaje nisiamini kuwepo kwa mungu? Katika dunia yake anaona hata hiyo fikra tu haiwezekani. Huyu hana tofauti na wewe.
anajiaminisha Mungu hayupo..
Ntajiaminishaje kwamba mungu hayupo wakati hajathibitishwa kwamba yupo in the first place? Inaonekana kama wewe ndiye unayejiaminisha kwamba mungu yupo, si mimi ninayejiaminisha kwamba mungu hayupo.
Ndiyo maana masuala ya dini na mungu yanaitwa "imani". Get it?
Kusema kwamba mungu yupo ni imani, kusema sijui kama mungu yupo si imani.
au kumkomesha kutokana na mapungufu aliyompa
Mpaka sasa kati yangu mimi ninayekwambia ghorofa lako la sakafu mbili unaliona refu kwa sababu ujatembea kuona mighorofa ya dunia na wewe unayenipa habari zilizofungwa na kukosa kujua habari za dunia nani ana mapungufu?
Have you read the Tripitaka? The Dhammapada? Have you seen the high level of morality in them?
Can you compare the high level of morality in them to the old testament or Quran?
Hujanionesha kwamba yupo.
kwaio kama Mungu hayupo ata zile sheria zake hazina maana sana kwake..
Sheria gani? Hizo za biblia ambazo kila sheria utakayonipa kuna kipengele kingine kinachosema tofauti na kuweza kuipindisha?
Kwa nini nitake kuwa na sheria isiyoeleweka kutoka kwa mungu asiyethibitishika inayoniruhusu kuua kwa mfano (biblia), wakati kuna morality isiyo na complications za mungu ambayo iko wazi tu kwamba kuua hakuruhusiwi?
Sijui umeiona hoja agnostic(wewe sio mkristo)???
Hapa hamna hoja kuna viroja vinavyofanywa kuonekana hoja kutokana na matongotongo ya ushamba yaliyojaa kwenye macho ya baadhi ya watu ambao wanajiingiza katika kujadili mambo makubwa bila hata ya kusoma the basic requirements kwanza.