Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

Mimi sielewi nia na lengo la kuficha ukweli kwa jambo linalohusu kodi zetu na matumizi yake.

Hivi tunamficha nani?Kwasababu hizi taarifa zimetoka nje yaani kwa hao tunaotakiwa kuwaficha.

Serikali imekiri yote yaliyosemwa na Lissu ndio yaliyopo.Au tunataka kuwaficha wenye hela yao yaani walipa kodi juu ya matumizi ya hela yao?

Nionavyo mimi kila mtanzania anapaswa kujua kodi yake inafanya nini.Ni haki yake ya msingi.

Watanzania tunapaswa kujua kwanini tunashikiwa denge yetu.
Nani kasababisha deni hilo.

Hatua gani za kisheria zinachukuliwa kwa wale wote waliosababisha hasara kwa taifa.
Kama zinavyochukuliwa hatua kwa wale wote waliohusika kutia hasara nchi yetu.
Serikali isilipe deni na ndege ije.

Hii ndio njia mzuri ya kumsaidia mh.Rais.Isilipe mpaka tuone wahusika wapo mahakamani.

Hongera sana Mh.Lissu raid ajae ndie atakaekusifu usivunjike moyo .Kafulila aliitwa tumbili wakati wa Kikwete rais wa wakati huu akamuita mzalendo na watesi wake ndio matumbili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu anayejisifiasifia na kuwanyanyasa wenzie huwezi kumwacha aendelee na tabia hiyo bila kumwanika adharani na madhara siyaoni zaidi ya kujua tuna kiongozi mkuu wa namna gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal wewe ni zao la nchi kuwa na utawala wenye watu wa hovyo km wa ccm.Otherwise ,sijui ni kukosa maadili au ni ujinga au ni combination ya vyote. UMEANDIAK UJINGA UKIAMINI UAFANYA IBADA NZURI KABISA. NAOMBA UNIJIBU HILI. UNAAMINI VIPI KUWA KUNYAMAZA KIMYA NDIO KUNA MASLAHI MAKUBWA KWA TAIFA KULIKO KUSEMA KWELI?Km huna hicho kipimo, naomba uache kuchafua hali ya hewa kwa njaa zao zisizoisha.Miaka nenda rudi hujikomboi na kuwa na faida kwa taifa.Sasa umefanya njaa ni ajira ya kudumnu.
 
sio kila ukweli unausema aisee utakuja angamiza Taifa
Taifa litaokolewa kwa kusema ukweli tunapata hasara kwa kuficha ukweli.


Sent using Jamii Forums mobile app
 



Kaka yangu Paskali, naweza kukupa somo jipya litakalo kusaidia katika maisha yako yaliosalia hapa duniani.

Kamwe hakuna ukweli unaobomoa, maana ukweli ndio asili ya Mungu mwenyewe kwa hiyo unaposema ukweli mahali popote umeufurahisha moyo wa Mungu. Kiroho, Kimwili, na kisaikolojia usiposema ukweli umejiumiza mwenyewe.

Labda jambo ambalo ungesema katika kusema ukweli lazima hekima itumike. Nitamani ni kuwekee mfano mmoja wa kusema ukweli kwa hekima.

Mfalme Daudi alimtamani mke wa mwanajeshi wake, kwa hiyo akamfanyia hila kuhakikisha anauawa vitani, Mungu hakupendezwa na jambo hilo, kwa hiyo alimtuma nabii Nathan kumwambia Daudi uovu wake. Nabii alimwambia Daudi kuwa kuna mtu mmoja tajiri ametembelewa na wageni, ila amechukua kondoo wa maskini akawachinjia wageni wake.

Mfalme Daudi alihamaki na kusema kwamba huyo tajiri lazima auawe, nabii akamwambia Daudi kuwa mtu huyo niwewe Daudi alilia sana na kutubu. Ukweli kwa njia ya hekima, ila ukweli unatakiwa usemwe kila wakati
 
Transparency ni kitu muhimu sana.Mi sidhani kama kuzuiwa ndege tena ya kiraia sababu ya deni ni issue senstive kiasi cha kufanywa siri.Kuna vitu vya kufanya siri.Kwanza madudu yote ya ufisadi ya serikali yetu mengi tuliyajua baada ya kufichuliwa na wapinzani,sasa imagine wangeamua kufuata ushauri wako na kuyafanya siri ingekuwaje?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiusema ukweli chumbani unahatarisha maisha yako atakuondoa ili siku moja siri yake isije ikavuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla lazima tena ni lazima nasema ni lazima saana TAIFA LIWE NA MASLAHI KWANGU.

Incident moja tu ya ukosefu wa maslahi yangu kwenye taifa:

UNABOMOAJE NYUMBA YANGU?

Nitaistawishia wapi jamii yanguili niwe na haki zote za kutetea maslahi hewa ya taifa la kuambiwa kuwa ni langu?

Kubomoa nyumba za watu ni wendawazimu, kupora mali zinazomilikiwa na watu kihalali ni ukichaa.

Yaani unihujumu, unisimange, unitese halafu ukifiwa nilie along side you?

wananchi wa uganda waliwasaidia wanajeshi wetu kumfurusha Idd Amini and it was for their country's betterment future. Naamini unauona usahihi wa waganda kuisaliti nchi yao kwa lengo la kuiokoa.

Imeandikwa "atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, atakaye kuiangamiza ataiponya"

IKAMATWE HATA IKULU NATAWAUNGA MKONO WATAKAOIKAMATA ILI TULIPE.

Si hivyo tu hata malawi wakituvamia sisi wananchi tutawapa ushirikiano wa hali na mali.

======Conclusion =====
Magufuli ameivuruga nchi yetu.
 

Yaani kaka Paskali umechenganya mambo mengi mno, kiasi kwamba majibu ya maswali yako yamo humo humo kwenye maswali yako!

Kwa ku-summarize labda niiweke hoja yangu hivi; UKWELI kwanza, siasa na mengineyo baadaye.


Kanuni ya kupanda na kuvuna inahusika hapa.....yaani kama tutajenga mfumo, utamaduni, sheria, uzalendo au kanuni yoyote ile kwa uongo (au hila) basi tutavuna uongo na upuuzi tu na sio maendeleo wala haki wala ustawi wala kitu chema mbeleni.

Kwa hiyo Ukweli hauna mpinzani wala mfanani. Hujiulizi kwa nini hata mtu anaweza kuwa na wazo la ajabu kama hilo swali lako? How can you compromise with Truth (hence facts and realities) then out of whims and wishful hopes for something good/positive in the end?

Halafu tena, je! ni kwanini hasa tunajaribu kuvitenga vitu hivyo? Kwa nini tusijiweke high moral-standards kuwa lazima tuwe wakweli, wawajibikaji na wazalendo (in one package) kwa sababu ndio ninavyojua ilivyo kwa walioendelea. Lakini hapa Tanzania tunataka ku define our own (sic) patriotism "version", alas!

Kama kungekuwa na uwajibikaji wa kawaida au wa kisiasa wala Lissu asingepata fursa aliyoitumia kwa sababu Serikali aidha ingekwisha maliza matatizo yale au ingekuwa imeto taarifa na muongozo zamani sana kabla ya Lissu.
 
Naomba tena naomba sana paschal mayalla asifundishe watanzania kuwa wadanganyifu

sioni sababu kwanini paschal mayala anataka watanzania wawe waongo eti kwa sababu ya maslahi ya taifa, hapohapo anamlaani tundu lisu kwakufichua usiri uliopo baina ya serikali na deni hilo,hapa paschal anasahau kuwa tundu lisu ni raia halali wa tanzania na anahaki ya kueleza hisia zake hata kama hakitaifurahisha serikali iliyopo madarakani

Paschal mayala unaposema watu wawe waongo sababu ya kuficha maslahi ya serikali je unajaribu kuifumbua nini jamii?ina maana kila kitu kinachofanywa na serikali ni uongo

Paschal mayalla unajua hizo ndege zimenunuliwa na watanzia wote bila kujali itikadi zao sasa unaanzaje kusema mlipakodi huyu awe muongo kwenye mali yake mwenyewe?


paschal nitaomba uniambie uchumi wa nchi gani unaondeshwa kwa kuwataka raia wake wawe waongo.

paschal umeprove failure kwelikweli, inamaana viongozi wafanye uovu huko ughaibuni na wenye nchi wakae kimya?

JamiiForums mbona mmeunganisha uzi au mmeanza kuficha uovu sasa
 
Mayalla nisamee nikuite MWONGO, NA MNAFIKI. Unafundisha watu kusema uongo, huna aibu,. Tena unajiita mwanasheria, shyster lawyer! umekosa aibu kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni msikuma na anatetea msukuma na dini yake ni sawa na yule mpenga kamasi.hapo ndipo utajua huyu jamaa ni mbinafsi mchuki mdini na mkabila chunga sana hao watu wawili


Swissme
 


Hawa jamaa undugu, na ujamaa wao ni mkubwa kuliko uhai wa taifa.Wana viutani na kujichekesha kipuuzi wakati wanataka mtetea mwenzao kutoka ktk makosa.Kila mahalia wataitana watani au ndugu ktk nafasi za umma wanapokutana kikabila. Pascal hajui hata hayo masalhi ya taifa yanalindwaje ,kwa vile ukabila ,ukanda na ujinga mwingine wa hivyo ndio unamweka mjini ingawa bado haujamkomboa.

Hawa watu ni duni sana, majambazi wenyewe huwa wanapiga na kuacha na kurudi mitaani wanawekeza kwa mafanikio na kuto ajira hadi akija mchumi anaweza ona mchango wake ktk jamii pana na watu wa karibu ya walioibia kuliko aliyeiporwa hela. CCM imetufikisha hapa, tuna akina pascal wanaweza jipa vyeo kibao vya social media kwa kupuyanga TBC na viwanja vya sabasaba km sio ktk dili za national housing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…