Wanabodi.
Huu ni uzi kuhusu Swali la Morality: Jee ni Lazima Kuusema Kila Ukweli Unaousikia?. Kwenye Medani za Siasa, Kabla ya Kuusema Ukweli Tunaousikia, Jee Tutangulize Mbele Maslahi ya Taifa Kwa Kujiuliza Kwanza, na Kuupima Kwanza Ukweli Huo Una Matokeo Gani, kwa Taifa Ndipo Tuuseme, au Tendelee na Hii Tabia ya Ukisikia Jambo Lolote, Wewe Liseme Tuu Bila Kujali Linamatokeo Gani as Long as Jambo Hilo ni la Ukweli?.
Ili Kupata Manufaa ya Kisiasa, Jee ni Lazima Wanasiasa Wetu, Tupoliticise Kila Kitu?, Kila Jambo, Kila Tukio?.
Declaration of interest.
Mimi Paskali ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, na kanuni kuu ya mwana habari, (cardinal rule ni " tell the truth, no matter what!", hivyo mimi ni mtu mkweli daima, na ni muumini wa ile ahadi ya mwana TANU " Nitasema kweli daima, fitna kwangu mwiko", ila katika kuusema ukweli au kuandika ukweli, nasema na kuandika kwa kutumia responsible journalism kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwa kujiuliza jee ukweli huu ukisemwa, utajenga, au utabomoa?.
Ukiona jambo, japo ni ukweli lakini ukweli huo, utabomoa, then ukweli huo, siusemi, kama ukweli niliousema kwenye bandiko hili
Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ...
Hii Kamata Kamata ya Kila Waompinga Magufuli, Ni Magufuli Anawatuma au Polisi Wanajipendekeza Tuu?.
My honest opinion, ingawa ni kweli rais Magufuli hapendi critics, mimi nilimsikia mwenyewe kwa masikio yangu toka kwenye kinywa chake na sio kwa kuhadithiwa, alisema anapenda challenge, ila hizo challenge ziwe ni ukosoaji wa kweli wenye nia njema, hivyo naamini hizi kamata kamata zinazoendelea za kuwakamata karibu kila wanasiasa wanaompinga rais Magufuli, siamini kama ni Magufuli anawatuma!, naamini hivyo ni kazi ya polisi wetu ambao wana jikomba komba tuu ili kuonekana wanafanya kazi.
Kwenye siasa za multipartisim duniani kote, kazi ya the opposition ni kupinga, kuopose kila kitu kinachofanywa na chama tawala hata kiwe ni kitu kizuri namna gani!, that is their right, kupinga, ndio maana wanaitwa wapinzani. Na serikali zote zinazoheshimu demokrasia ya kweli, lazima zikubali kupingwa.
Nimeishi kidogo UK, US, na Uswiss. Uingereza pale Times Squire karibu kila siku ni maandamano. US ule mtaa jirani na Capitol Hill kuna uwanja unakuwa huru kupinga chochote, Uswiss uwanja huru wa kupinga, ni pale uwanja wa wazi nje ya ukumbi wa Bunge, the The Bundes House. Hivyo sioni mantiki ya sababu zozote wanaompinga rais kubughudhiwa!, this is not democracy, Tanzania sio nchi ya kidikiteta!, tena kiukweli, kama katiba yetu imeruhusu mikutano na maandamano, hakuna any justified reasons at all za rais Magufuli kupiga marufuku, ni ukiukwaji wa wazi wa katiba ya JMT, but to be honest, yeye kama rais wa JMT kwa mujibu wa katiba yetu, hana mamlaka ya kuzuia jambo lililoruhusiwa na katiba, and he gas nothing to loose akiruhusu mikutano na maandamano.
Wito kwa IGP, Kamanda Sirro, controll vijana wako watekeleze majukumu yao kwa sheria taratibu na kanuni na sio kwa kutaka kujipendekeza au kujikomba komba!.
Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako ...
Je, Rais wetu, Magufuli anasoma JF? Rais, Please msikilize Binti ...
Jee Wapinzani Kazi yao ni Kupinga Tuu Kila Kitu au Kukosoa Tuu Hakuna Kupongeza Hata kwa Mazuri?.
Japo kazi ya upinzani ni kupinga na kukosoa, lakini tunapokuja kwenye issues muhimu kwa maslahi ya taifa, maslahi yataifa ndio yanatangulizwa mbele, sisi sote kama Watanzania, we stand as one, tunakuwa kitu kimoja, tunakuwa watu wamoja, tunaweka mbembeni tofauti zetu za kisiasa, hakuna tena siasa za vyama, wala siasa za watu, tunaweka pembeni siasa, tunaitanguliza mbele Tanzania, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, we stand as one, na kila kitu kinafuatia baadae.
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...
Kwenye Haki za Wanyonge, Magufuli ni Kama Khalifa Mkuu Harun El ...
Conclusion
Namalizia kwa haya maswali ya msingi, kuhusu ni hoja za morality kusema kweli daima, lakini Jee ni Lazima Kuusema Kila Ukweli Unaousikia?. Kwenye Medani za Siasa, Kabla ya Kuusema Ukweli Tunaousikia, Jee Tutangulize Kwanza Mbele Maslahi ya Taifa Kwa Kuupima Kwanza, Ukweli Huo Una Matokeo Gani, Ndipo Tuuseme, au Tuendeleze Kila Ukisikia Lolote, Lisema Tuu kwa Sababu ni la Ukweli?. Jee Ili Kupata Manufaa ya Kisiasa, Jee ni Lazima Wanasiasa Wetu, Tupoliticise Kila Kitu?.
Wito Wangu ni Sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni ni kweli!.
Wasalaam.
Paskali
Rejea.
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or ...
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...
Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa ...
Tusimlaumu Rais Magufuli Kwa Kila Kosa, Rais Yeye Hana Kosa Bali ...
Pongezi Rais Wetu Magufuli Kwa Kuwa Mkweli Daima, Tuanzishwa The ...
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
Kitendo cha kuita nchi majirani zako kuwa ni "vinchi" ni uungwana ...
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ...
Hoja ya Udikiteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi ...
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio ...