Swali la mwaka: Nani alimleta Ballali nchini?

Naomba nisikubaliane na wewe Bwana Gembe kwamba Balali alipewa kazi kwa vile alikuwa na uwezo.Naomba nikubaliane na Mwanakijiji kwamba Balali aliwekwa Bank Kuu kwa makusudi fulani.Kumbuka kwamba Balali alikuwa mwajiriwa wa World Bank.Ambacho bado kinanisumbua akili ni kwamba hivi Tanzania tulikosa watu wenye 'qualifications' za kufanya kazi Bank Kuu mpaka World Bank watuletee mtu Kama Balali?This is extremely suspicious.Ninahisi World Bank walikuwa na ajenda ya siri na ninahisi ajenda yao ni hili lililotokea.Wale wenye "idea of conspiracies" zinazoendelea nadhani wanajua kwamba World Bank,IMF au mashirika yeyote ya wakubwa hawa hawana nia ya kweli ya kutuendeleza kiuchumi.Maneno yao yanaonekana kuwa matatamu sana "to unsuspicious minds,but the truth is the opposite." Ndio maana mara nyiki tumeingizwa mkenge,na kama hatukuwa waangalifu tutaendelea kuumia.

 

Dah!!!! Mshkaji unatukata stimu. Acha watu wamkome nyani regardless whether they are along MKJJ's track
 
Hii thread imekuwa inajiruida sana mbele yangu. Kuna wakati nikiwa safarini kwenda mapumzikoni Tanzania niliwahi kukutana na jamaa mmoja aliyewahi kufanya kazi nyeti pale State Department akanituma nimfikishie salamu zake kwa Mkapa, Ballali, Anna Muganda na mama mwingine aliyekuwa na jina la kutokea Songea ambaye wakati huo alikuwa anafanya kazi Wizara ya Afya. Bwana huyu alikuwa anawajua watu hao personally kutokana na kukutana nao mara kwa mara hapo Washington DC wakati akiwa state Department nao wakiwa kwenye majukumu yao ya kawaida ambapo Mkapa alikuwa Balozi wa Tanzania hapo Marekani.

Kwa hiyo Mkapa na Ballali walikuwa wanafahamiana siku nyingi sana. Nadhani Mkapa ndiye aliyemleta rafiki yake huyo wa zamani, ingawa inasemekana kuwa wakati huo Ballali alishakuwa raia wa Marekani (sina uhakika lakini na sidhani kama tetesi hizo ni za kweli).
 
Mama wa kwanza wa zamani alimtafutia mke ballali.....
 
Ndg Mtanzania,
Anaanza na jina (M), anatokea mkoa unaoanza na jina (M), na mimi naanza na Jina (M)ajita basi nakupoa mji MUSOMA ili "M" iendelee kuwa common factor.Kubaali basi na pls pasua jipu.

Majita,

Bahati mbaya tayari nimeshapewa mji na kuukubali na kutoa jina. Nikikubali na mji wa pili nitakuwa fisadi.

Dada yenu ndiye alimtambulisha Ballali kwa Mkapa. Baada fisadi mkuu kuchukua ushauri zaidi ya unaokubalika, wenye mali wakaona huyo mama hafai na ikabidi aondoke.

Mkuu FMES kamwaga mtiririko mzima.
 
Wakuu mtujibie basi swali hilo la nani alimshauri Mkapa amchukue Balali.Ninavyoona mimi dili hilo wahusika ni Chenge,Rostam,Mkapa na Balali.
 
Nani alimleta balali nchini...Kwani balali lilikuwa boga?balali alikwea mwenyewe pipa na kujileta mwenyewe bongo.
 
Nani alimleta balali nchini...Kwani balali lilikuwa boga?balali alikwea mwenyewe pipa na kujileta mwenyewe bongo.

Mkuu naona umepotea kabisa.
Yawezekana hujui Balali mwana wa Mufindi alicho tundea taifa hili na kuzugwa kuwa kafa...nisiendelee isije ikawa nongwa.Watu bado wana machungu wanataka kujua nani aliye mpa dili Balali BoT?
 
Mkuu naona umepotea kabisa.
Yawezekana hujui Balali mwana wa Mufindi alicho tundea taifa hili na kuzugwa kuwa kafa...nisiendelee isije ikawa nongwa.Watu bado wana machungu wanataka kujua nani aliye mpa dili Balali BoT?

Ukishajua nani aliyempa balali dili BoT what next?
 

Mkuu Mtanzania!!
Yaani utafanya kila nitakapo kuwa napiga kona kwenda kupata moja moto moja baridi nikizungukia uani kwa familia ya huyu dada yetu niwe natapika kwa kuyatinga.Ila kwa vile fisadi anaweza akawa yeye peke yake bila familia yake kuhusika ngoja nisitapike,ila kale ka methali sijui "......... janga hula na wa kwao bado kananisuta"
 
nimefatilia hii story hapa nafikiria Balali alitumiwa bila yeye kujua, watoto wa mjiji walijua balali ajazoea mambo ya corruption na mambo mengine ya madili ya dar, kwahiyo alikuwa a good target for the really ufisadi. Na watu waliomchezea Balali ni watu ambao wapo BOT and Mafisadi wengine wa mjini hapa
 
Mkjj pata break kidogo kwanza.

[media]http://www.youtube.com/watch?v=UXDh7OwlOOM[/media]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…