Naomba nisikubaliane na wewe Bwana Gembe kwamba Balali alipewa kazi kwa vile alikuwa na uwezo.Naomba nikubaliane na Mwanakijiji kwamba Balali aliwekwa Bank Kuu kwa makusudi fulani.Kumbuka kwamba Balali alikuwa mwajiriwa wa World Bank.Ambacho bado kinanisumbua akili ni kwamba hivi Tanzania tulikosa watu wenye 'qualifications' za kufanya kazi Bank Kuu mpaka World Bank watuletee mtu Kama Balali?This is extremely suspicious.Ninahisi World Bank walikuwa na ajenda ya siri na ninahisi ajenda yao ni hili lililotokea.Wale wenye "idea of conspiracies" zinazoendelea nadhani wanajua kwamba World Bank,IMF au mashirika yeyote ya wakubwa hawa hawana nia ya kweli ya kutuendeleza kiuchumi.Maneno yao yanaonekana kuwa matatamu sana "to unsuspicious minds,but the truth is the opposite." Ndio maana mara nyiki tumeingizwa mkenge,na kama hatukuwa waangalifu tutaendelea kuumia.
Mwanakijiji,
Mie nina uhakika kabisa balali alipewa kazi kutokana na uwezo aliokuwa nao na wakati Ballali anakuja hapa Tanzania hakuja kama Msahuri wa Mzee Ben bali alikuja kufanya kazi ya World Bank kakita jitihada za WB kusaidia nchi zilizokuwa zinaendelea.
Ballali aliletwa na World Bank na kama kuna mtu alimshauri Mkapa ampe kazi Ballali atakuwa ni Katibu Mkuu kiongozi na yeye alifanya hivyo baada ya kupatikana vetting report kutoka kwa watu wa Usalama wa Taifa.
Nakumbuka Ballali aliitwa na Mkapa pale Magogoni siku ya Jumapili na kuambiwa ameteuliwa kuwa Gavana na hakupewa muda wa kutafakari kuhusiana na hilo ila inasemekana kuna wizi flani ulitokea pale BOT na Mkapa alikasirishwa sana na kuagiza yafanyike mabadiliko makubwa pale BOT. Sema kipindi hicho watu wa aina ya Ngurumo na Mwanakijiji, Watu wenye uwezo wa kusema yale magumu kama Kubenea walikuwa hawana meno.
Ilikuwa ni tabia ya Mkapa kumfukuza mtu yeyote yule pindi anapokosea, mtakumbuka jinsi alivyomfukuza Mattaka pale PPF. Alivyomuomba Mboma aachie ngazi baada ya kashfa ya sukari, mie nilishangaa sana Mboma kurudi na kutaka ubunge!
Mkuu Mwanakijiji kama utakumbuka wakati Mkapa akiwa pale Foreign alikuwa ni Waziri pekee ambaye alikuwa akirudisha pesa wizarani kila mwaka na alikuwa na rekodi safi sana katika utendaji na utumiaji wa pesa za umma, na hii ilisababisha Mwalimu kumkubali mapema sana tofauti na wengine waliogombea 1995 (kumbukeni kashfa flani za madini 1994).
Mzee Mkapa alibadilika sana kuanzia kifo cha mwalimu, nadhani alighafirika na kupoteza mwelekeo na kuna watu walijiingiza sana pale na kujidai walikuwa watu wa karibu na mwalimu.
The one and only person wa kulaumiwa mpaka leo ni Ruhinda!