Swali la tafsiri ya terrorism linasaidia nini kesi dhidi ya Mbowe?

Swali la tafsiri ya terrorism linasaidia nini kesi dhidi ya Mbowe?

Kwa sababu Upinzani hautakiwi Nchi hii Watawala wanatafuta kila Njia ya kuufuta ikiwa ni pamoja na Kuwabambikizia Kesi
Mfano Kesi ya Mdude ile ya Mbeya n.k
Hiyo ni kweli tupu. Hata Mzee Ali Hassan Mwinyi Rais mstaafu alikiri mwenyewe kuwa vyama vya upinzani viliwekewa mizengwe na CCM tangu wakati wa uwanzisjwaji wa vyama vingi nchini. Hivyo kila awamu inakuja na mizengwe yake.
 
Hapo vip!!

Binafsi maswali kama haya natafsiri kama maswali ya kitoto yasiyoweza kusaidia upande wa utetezi.
Hata kama lengo nikumchanyanya shaidi ila me naona haisadie sana kwa jinsi kesi na ushaidi wa jamuhuri ulivyokaa wazi.

Cha ajabu baadhi ya vyomba vya habari vinasema shahidi ashindwa kujibu maswali kwa kuangali swali kama hili ambalo haliwezi kusaidi katika kesi hii.

Naona kuna ushabiki wa baadhi ya mitandao na vyombo vya habari kwa lengo la kutaka kutengeneza image ya kesi hii kwa wananchi pasipo kuonyesha upande mwingine wa shilingi.

Narudi hii kesi imemkalia bwana yulevibaya tuache ushabaki.

IMG_8151.jpg
 
Swali hilo kama ilivyo maswali mengine ya Mawakilo wa utetezi Hayana Msaada Wowote kwa Mheshimiwa Mbowe hasa linapokuja Suala la Tuhuma dhidi yake

Mawakili.wa Mbowe wajikite kupangua hoja zinazowaeoloshwa.na Jamhuri dhidi ya mteja wao

Askari ambaye Ni shahidi wa Serikali amejieleza vizuri Sana na anaijua kazi yake vizuri
 
Huwa najiuliza maswali kwa nini ikitokea kiongozi wa upizani ameshitakiwa anaonekana anaonewa hata kabla ya tuhuma yenyewe kufahamika?ni mind set,ushabaki,ujinga au kitu gani...
Shida ni fisi kumshitaki swala kwa fisi mwenzie. Kuna kila viashiria vya wazi kuwa Chadema hakitakiwi nchini. Risasi kwa akina lissu na kupotea kwa wanachama wao ni mwendelezo TU wa hili. Kuna mtu alitaka kuufuta upinzani nchini kabla ya 2020.
 
Shida ya Mallya anatamka neno terrorism kichaga, linasikika tourism...

Na ndio maana katika re-examination, shahidi alifafanua alivyosikia.
 
Hapo vip!!

Binafsi maswali kama haya natafsiri kama maswali ya kitoto yasiyoweza kusaidia upande wa utetezi.
Hata kama lengo nikumchanyanya shaidi ila me naona haisadie sana kwa jinsi kesi na ushaidi wa jamuhuri ulivyokaa wazi.

Cha ajabu baadhi ya vyomba vya habari vinasema shahidi ashindwa kujibu maswali kwa kuangali swali kama hili ambalo haliwezi kusaidi katika kesi hii.

Naona kuna ushabiki wa baadhi ya mitandao na vyombo vya habari kwa lengo la kutaka kutengeneza image ya kesi hii kwa wananchi pasipo kuonyesha upande mwingine wa shilingi.

Narudi hii kesi imemkalia bwana yulevibaya tuache ushabaki.
Ni swa, swali linapima ufahamu mdogo tu. Inaonyesha uelewa wa shahidi ni mdogo ilhali wajibu ni mkubwa. Hii ina madhara kwa wengine.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Hilo neno lipo kwenye ripoti anayodai kuwa aliandika yeye. Wakili Kamuuliza kama anajua maana ya terrorist na terrorism ili kulinganisha kama kweli aliandika yeye,kilichofuata ni kicheko mahakamani
hii ndiyo JF yenyewe kabisa ... asante sana
 
Huwa najiuliza maswali kwa nini ikitokea kiongozi wa upizani ameshitakiwa anaonekana anaonewa hata kabla ya tuhuma yenyewe kufahamika?ni mind set,ushabaki,ujinga au kitu gani...
Ni kwa sababu ni wanasiasa na siasa ni vita baina ya wanasiasa.
Mpira una sheria 17, siasa haina bali walio madarakani Ndio wanaoweka sheria. Hii ndio sababu ya vita.
Jogoo liloanza kuwika haliruhusu jogoo lingine kuwika.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Ni wazi kesi ilikwisha amuliwa, lakini pia wananchi tunapata funzo kuhusu elimu na uwezo wa walio kwenye madaraka.
Serikali ikikudhamiria hauta ishinda, hukumu pendekezwa itatolewa na utaambiwa rufaa iko wazi.
Mbowe aliwahi kufungwa bila kosa na mahakama ikathibitisha hilo na ikamuachia!
Kama walio kwenye madaraka uwezo wao ndiyo huo wewe ambaye kwa kukosa uwezo huna madaraka utakuwa na uwezo wa chini sana
 
Hilo neno lipo kwenye ripoti anayodai kuwa aliandika yeye. Wakili Kamuuliza kama anajua maana ya terrorist na terrorism ili kulinganisha kama kweli aliandika yeye,kilichofuata ni kicheko mahakamani
Umejibu vizuri sana mkuu mtoa mada anaweza kujihisi mpumbavu na hata wanaomtetea

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo neno"terrorism" ila tatizo ni mtu kuandika lugha asoijua. Hoja hapa ilikuwa ni kutanabahisha watu kuandika lugha wanayoifahamu; au mimi ndo sikufahamu.
Ina maana alipoandika terrorism kwenye ripoti alimaanisha masuala ya utalii? Hapa ni ishara kuwa aliandaliwa ripoti hakuiandaa yeye.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Huwa najiuliza maswali kwa nini ikitokea kiongozi wa upizani ameshitakiwa anaonekana anaonewa hata kabla ya tuhuma yenyewe kufahamika?ni mind set,ushabaki,ujinga au kitu gani...
Wewe umenikariri mimi na ndani ya hicho ulichkikariri nimeandika kifungo cha Mbowe ambacho alikitumikia lakini akaachiwa bila rufaa kuwa alifungwa kimakosa! Na hili lilitokea pia kwa Sugu, sasa ni mind set gani ipo au unaona hakuna uonevu. Nakushauri ujiunge Chadema kwa utafiti tu, baada ya miezi mitatu utajua Segerea ikoje ndani.
 
Wewe hauwezi kufahamu
Wewe ndiyo hufahamu. Unaonekana uko too low kwenye reasoning. Logical questions zinafanya mashahidi watoe ushahidi ambao mwisho unaacha doubts (mashaka). Kumbuka mahakamani ili umpate mtu na kosa, lazima ushahidi usiache shaka yoyote (you need to prove beyond reasonable doubts). Sasa hao mashahidi wanavyojikanyaga wanaacha mashaka (doubts) ambapo mwisho Jaji atatumia rungu lake kuwaachia huru watuhumiwa. Kazi ya mawakili wa utetezi ni kuziweka wazi hizo doubts na wale wa serikali ni kuhakikisha mashahidi wao wanatoa ushahidi ulionyooka ili kuondoa hizo doubts.

Hakuna maswali ya kipuuzi mahakamani.
 
Hapo vip!!

Binafsi maswali kama haya natafsiri kama maswali ya kitoto yasiyoweza kusaidia upande wa utetezi.
Hata kama lengo nikumchanyanya shaidi ila me naona haisadie sana kwa jinsi kesi na ushaidi wa jamuhuri ulivyokaa wazi.

Cha ajabu baadhi ya vyomba vya habari vinasema shahidi ashindwa kujibu maswali kwa kuangali swali kama hili ambalo haliwezi kusaidi katika kesi hii.

Naona kuna ushabiki wa baadhi ya mitandao na vyombo vya habari kwa lengo la kutaka kutengeneza image ya kesi hii kwa wananchi pasipo kuonyesha upande mwingine wa shilingi.

Narudi hii kesi imemkalia bwana yulevibaya tuache ushabaki.
sawa ndugu jaji
 
Huwa najiuliza maswali kwa nini ikitokea kiongozi wa upizani ameshitakiwa anaonekana anaonewa hata kabla ya tuhuma yenyewe kufahamika?ni mind set,ushabaki,ujinga au kitu gani...s
Riport kaandika yeye katumia Hilo neno anaulizwa ufahamu wake kuhusu Hilo neno anaonekana hajui utaiamini hiyo ripoti?
Upo kwenye usaili (interview)
Unaulizwa Mambo yaliyopo kwenye CV yako unaulizwa mwaka uliomaliza shule unataja mwaka tofauti na uliopo kwenye CV
Unaulizwa swali la ufahamu tu kuhusu fani yako gaidi Ni Nini na Ugaidi Ni Nini unaanza kuleta stori za mtalii!
Mosi tunaanza kuwa na mashaka na ufahamu au utaalamu wako katika fani yako Kama Ni interview unakuwa ushapoteza toka dakika ya Kwanza.
Tambua kuwa hukumu ya kweli huwa Ni hukumu ya watu sio hukumu ya mtu.
haki ikitendeka watu hushuhudia kuwa haki imetendeka.
HATA MAANDIKO YANATUKUMBUSHA MUNGU ATAHUKUMU MBELE ZA BINAADAMU WOTE, NAO WATASHUHUDIA NA KUSEMA HAKIKA BWANA HUKUMU ZAKO NI ZA HAKI NA KWELI.
Kama tumeahidiwa kuipitia hukumu ya Mungu tunashindwaje kuthibitisha hukumu ya binadamu?
Akihukumiwa katika haki na kweli tutaona na asipohukumiwa katika haki na kweli pia tutajua.
 
Back
Top Bottom