Swali la tafsiri ya terrorism linasaidia nini kesi dhidi ya Mbowe?

Kazi ipo.
Kesi ya Shutuma za Ugaidi swali "Nini maana ya Terrorism kwa Kiswahili"...
Inamaana wewe mleta mada huoni kabisa uhusiano wa swali na kesi?

Au umepost kujitafutia ka umaarufu kako tu,?
 
Kama siloli naye anashindwa kutofautisha jinai na ugaidi basi hata watu wakiibiana wake mmoja akaanza kumtwanga ngumi huyo ni gaidi....
 
Hivi wale manjagu tuliokuwa tunawaona wanasoma vyuoni huko wako wapi waokoe jahazi maana kupeleka watu hawajui kitu na kudharirisha kada nzima ni hatari sana kwa kweli..
 
Chedema ni kampuni ya mtu sio chama cha siasa..alafu kwa tafsiri jingine ni chama cha kuwatete kabila fulani Tanzania.
 
Ndio wananchi wote wanaopenda demokrasia wanafanya makosa makubwa kulala vitandani mwao wakati demokrasia inapohujumiwa na watawala.
 
Kama unaona ushahidi wa Jamhuri umekaa Wazi si ufurahi Sasa? Unaleta thread za kifala Fala na Kuwait'a watu majina ya kutweza ili uonekand wa maana kumbe Zuzu tu. Tuoneshe hapà huo ushahidi ulio Wazi na kesi ilipomkalia Mbowe pabaya!!!
 
Hivi unajua kwamba Mbowe bado hajafikiwa katika kesi. Kwahiyo subiri zamu ya kusikilizwa mashtaka yake ndio utajua anasaidiwa au anaisaidia serikali kujijua ina jeshi la polisi la namna gani?
 
Ndo maana nalubaliana na wanaosema CCM imeishiwa wenye hoja. Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba Cpl Abdalla aliulizwa swali moja tu.
1.Haluulizwa Kwa nini kielelezo mahakamani ni risasi yeye kaleta maganda?
2.Hakuulizwa Kwa nini kaharibu kielelezo na ni Sheria ipi au maagizo yapi yalimruhusu kubadili Hali ya kielelezo toka risasi kuwa maganda?
3.Hakuulizwa Kwa nini Aina ya maganda ni tofauti na Ganda la risasi moja nzima iliyobaki?
4.Hakuulizwa barua ya maelekezo ya kufanya uchunguzi iliandikwa katika lugha gani akajibu ni Kiswahili?
5.Hakuilizwa alichagua kuandika ripoti kwa kiingeeeza Kwa vile anaijua lugha hiyo vizuri Sana akajibu ndiyo?
6.Hakuulizwa kama anaijua vizuri nini maana ya terrorist akajibu ni ugaidi na terrorism akasema ni Utalii?

NB: Msilete hoja Kwa kudonoa wenzenu tunafuatilia hatua Kwa hatua.
 
Darasa aliwahi kuimba, "kumwelimisha Zuzu utajipa kazi". Huyo utakesha naye.
 
Kweli kabisa ingawa wafuatiliaji si wanasheria lakini wanajua kama haki inatendeka au la.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kwani sheria inasemaje mwenyekiti akiwa kifungoni tuchague mwingine maisha ya chama yaendelee tu
 
Wew n kima hujui ktu
 
Mku, mfano mzuri ni rais wa sasa wa Zambia alivyotendewa na rais aliyeshindwa, Edgar Lungu

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…