Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Labda hili swali tungeliuliza hata kuhusiana na Jeshi la Wananchi. Hasa baada ya hizi teuzi. Najiuliza inawezekana kwenye majeshi yetu hakuna wanawake wenye uwezo na ufahamu wa mambo ya kazi, operesheni na mikakati ya kijeshi kuweza kushika nafasi za juu kwenye majeshi hayo?
Labda Rais yeye kwa vile anajua mengi inawezekana baada ya kuangalia akagundua kuwa bado hakuna wanawake wanauwezo wa kushika nafasi ya juu... si kwa sababu ni wanawake bali kwa sababu hawana uwezo.
Ila kama wapo wenye uwezo JWTZ au Polisi au Magereza (labda huku atateuliwa mwanamke - sijui Katherine Mwipopo anacheo gani sasa). Rais atawapa nafasi au mpaka wajioneshe vipi kuwa wanaweza kushika nafasi hizo.
Labda Jaji Mkuu Mwanamke wa kwanza.