Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Mkuu vita ni biashara nzito sana hapa ulimwengu inayofanywa zaidi na mataifa kama US, China na Russia.

Mambo yanayoendelea huko Russia na Ukraine mengi ni Propaganda.

Russia hajawahi kutoa takwimu za ukweli za uchumi wake toka vita ianze. Kama sikosei mwaka jana waliingia bungeni wakiwa na hesabu za mapato tu ya nchi ila matumizi hakuna, taarifa ya bank kuu yao ilificha ripot ya fedha kwa miezi kadhaa.

Asikwambie mtu, Russia anahenyeka saaana tu kwa vikwazo.
 
Russia ni taifa teule
 
Dah!... uchambuzi mzuri sana..... hongera mchumi.
 
Urusi wenyewe wanaomba warudidhwe kwenye mfumo wa swift ndo warudi kwenye grain deal kama vikwazo havifanyi kazi kwann atake kurudi?
 
Kweli kuna propaganda nyingi mno kwenye hii vita. Japo nachofahamu mimi ni kwamba hii vita imekuwa mbaya zaidi kiuchumi kuliko kijeshi. Mpaka sasa hakuna taifa kubwa barani Ulaya ambalo halijaumizwa na mfumuko wa bei au mdororo wa uchumi.

Ila kubwa ni kwamba mwaka 2022 taasisi kubwa za kifedha zilitoa utabiri kwamba uchumi wa Urusi (GDP) ungenguka kwa asilimia 12%, lakini baadaye wakabadilishwa takwimu za makadirio na kusema kwamba uchumi wa Urusi utaanguka kwa asilimia 2% hadi 3%.

Nachojiuliza nini kilitohea hadi wakaandika makadirio makubwa hivi lakini ghafla wakabadilisha takwimu. Wangebadilisha kutoka 12% hadi 10% ningeelewa, maana uchumi hupimwa kwa makadirio (Estimates), ila kutoka 12% hadi 3% ni parefu sana.

Hebu tujuzane zaidi.....
 
T14 Armata Kwanini urusi uchumi wake haujaanguka kama ilivyotarajiwa na USA na WEST?.
USA na West hawajawahi tarajia uchumi wa Urusi uanguke. Lengo lao kwenye sanctions ni kuilazimisha Urusi iwe na options kwenye harakati zake za expansionism. Ijue wakati inaendelea kufanya uvamizi itaendelea kupoteza mazingira ya kiuchumi na hao wanaoweka vikwazo, isiwe na uhuru wa kuvamia ikijisikia.
Kama West na US zingetaka kuiua kiuchumi Urusi basi zingeanzia kwenye machine tools na precision machinery ambako Urusi haijiwezi
Importation ya mitambo muhimu ya uzalishaji ingesitishwa yote na Urusi wangeishia kutegemea black market au kutegemea machine tools za China ambazo huwa haizipendelei.

Kwanza Marekani inahusika kwenye kuisaidia Soviet Union kukua kiviwanda mwanzoni mwa utawala wao, Volgograd tractor plant ilijengwa na Wamarekani pale Soviet Union iko busy kukua kwenye kilimo. Walikuja kupishana na Marekani walivyoanza kujitutumua na kujishindanisha na Marekani. Na technology transfer wakawa wanaitumia kutengeneza silaha, mfano hiyo Volgograd plant ilitengeneza vifaru, infantry fighting vehicles na artillery.
Sasa nchi gani itakubali ikupe teknolojia uunde silaha alafu uitunishie misuli, wakaachana nayo.
Hata China wanamfanyia hivi Warusi na Wamarekani, unamuuzia licence ya helicopter kutoka Sikosrky ya Marekani yeye anatumia kutengeneza attack helicopter. Sasa unaamua kumpa teknolojia chache zisizo na dual use na sometimes unagoma kumuuzia baadhi ya vitu asiige.

Marekani iliwahi kuwashawishi Germany na Japan baada ya WW2 kustaariba na kuishi kama waungwana duniani wakati kwenye vita walipigana. Leo hizo ni nchi za tatu ya nne kiuchumi duniani, South Korea waliopambaniwa na Marekani ni nchi inazidi Urusi kiuchumi. Hizo nchi tatu ni almost hazina kitu kwenye rasilimali wala ukubwa wa ardhi kama Urusi. Kama Urusi wangekuwa serious na vitu vya msingi hizo nchi tatu hazikutakiwa ziikaribie kiuchumi.

Una rasilimali za kutosha madini mengi kuanzia aluminium, gold, bauxite, iron ore, copper, diamond hadi rare earth metals, gesi ni wa kwanza duniani, mafuta ya kutosha mpaka unaitwa OPEC wakati sio mwanachama, unalima ngano, una mbao, una ardhi kubwa sana wakati idadi ya watu milioni 144 ukitaka kutenga eneo kubwa la kilimo unaweza, una uvuvi. Bado unazidiwa na Italy kwa GDP. Sasa wewe upewe nini hapa duniani?

Urusi sio kwamba hawaipendi, ni yenyewe inalazimisha kujipanbanisha na kuishi kama karne ya 20. Marekani haina haja ya kupambana na Urusi, na inachofanya ni kilekile tena pungufu ya ambacho superpower yeyote kwa timeline yoyote hapa duniani huwa anafanya.
 
Shida yako unatoa mawazo yako kishabiki sna na kimahaba kwa nchi za magharibi ila kiuhalisia west waliweka vikwazo ili kuuwa uchumi wa Russia rejea kauli ya Biden baada ya uvamizi wa Russia ukrein

West ni kweli wanateknolojia kubwa sana na siyo kwamba wanampa Russia kwa mapenzi mema ila ni sababu ya soko la uhakika, nchi nyingi zinanunua bidha za bei powa kutoka China japo ni nzuri ila haziwezi fikia za west lakin za China ni gharama nafuu zaidi kuliko za west sasa wapi watapata soko la uwakika kama la Russia ambaye yeye ana pesa

Nakukumbusha tu hakuna nchi yoyote ulaya au Asia aambaayo ingepigwa sanction kama za Russia ingesaavive ata mwaka mmoja uchhumi wa Russia ni halisi na ndyo nchi yenye madeni madogo kuliko awo uliwo wataja, japana deni lake linaanza kuwa mzigo kwa nchi, italy ni nchi inayoemea mipiraa kiuchumi ata pale umoja wa ulaya hana sauti tena kama France au Germany
 
Italy inayohema kiuchumi hapo Ulaya inaizidi Russia kwa GDP, HDI, GDP per capita na vipimo vingi kiuchumi. Wakati Italy haina upendeleo wa natural resources kama Russia.
Japan wana deni kubwa sana ukilinganisha na nchi nyingine duniani, ila wana uchumi mkubwa unauzidi wa Russia mbali. Na almost hawana rasilimali yoyote.
China na India zina watu wengi zinapambana kulisha, kujenga shule na hospitali, kuajiri na usumbufu mwingine unaotokana na kuwa na population kubwa ila bado zinapiga hatua nzuri wakati Russia ina watu wachache na rasilimali nyingi sana kiasi kwamba matumizi ya kawaida kwa population ni madogo ila inashindwa weka concentration kwenye vitu vya maana kiuchumi.
Hivi hushangai kuona mabilionea wa Russia karibia wote ni oligarchies? Hushangai almost kila bilionea wa Russia anatokana na kubinafsishwa kwa rasilimali, hakuna bilionea wa kampuni ya simu au kampuni ya magari au aliyegundua mifumo ya usafirishaji au teknolojia?

Hapo kwa Biden na vikwazo umesema vizuri "baada ya uvamizi wa Russia Ukraine". Sasa uvamizi ni wa 2022, kilichoishinda Russia kuwa kati ya nchi 10 kubwa kiuchumi kwa GDP kabla ya 2022 ni nini?
Basi turudi nyuma, kabla ya Russia kuivamia Crimea mwaka 2014 ilikuwa wapi kiuchumi duniani?
Bila hata sanctions Russia ni ya kawaida.
 
yani wewe unajiona unaelewa mahitaji ya warusi kuliko warusi wenyewe?

mrusi amekuwepo kabla US haijakuwepo, alafu leo useme US ndio kaisaidia Urusi kiviwanda? hizi propaganda unakolishwa pole sana!
 
tatizo jingine unapima uchumi wa nchi kwa kuangalia utajiri unaoelea, usio na mizizi...... na hiki ndio kipimo west wanakipenda, kwa sababu kinawafariji kwamba nchi zao ni tajiri.....

uchumi wa Urusi haujaanguka kwa sababu haupo kama uchumi wa ulaya na marekani (uchumi fake), unajisifu kwa utajiri wa makaratasi? masoko ya hisa hewa? mabenki?....

huu ndio uchumi unaosema afrika ni bara maskini zaidi duniani, lkn tukisema kila mtu aishi kwa kujitegemea ulaya sijui kama wataweza!
 
Ndyo maana nakwambia uchumi halisi haudanganyi iyoo GDP, na mengine yote haijafika robo ya kile Russia anacho, Leo hii Italy ingekulaaa sanction mabenk, masoko ya hisa vyote vingesambaratika ila vipi Russia na mtoa mada ameleta mada nzuri tu kwanini pamoja na vikwazo vyote bado Russia ameonekana ngangari

Alafu kila nchi ni mjivuni kwa vitu vyake na uhalisia wa nchi yake Russia ana rasilimali nyingi kuliko west Russia kupata kile ambachho hhana kutoka west siyo kkosa na vilevile ni salama kkwa dunia ya Leo maana anggekuwa na teknolojia kubwa na wingi wa rasilimali alionawoo sidhani kama asinggetamani kuitawala dunia.

Ndyo maana tunawaita pro NATO vilaza matajiri wa west ambao mnawaita mabilione mnawaona wanahaki ya kumiliki utajiri walionawo ila nchi nyingine awoo ni majambazi wa rasilimali za nchi zao.
Na pessa nyingi za matajiri wa Russia ndizo zilizungushhwa kwenye biashara nyingi zilizopo ulaya maggharibi hassa UK na German Leo hii ili kubariki ujambazi wenu wa pesa zao mnawaita majina mabaya
 
Nimetaja vipimo vitatu. Kama hutaki taja vya kwako unavyotumia mwenyewe vinavyosema Urusi ana uchumi mkubwa. Na ututajie ni ya ngapi kiuchumi duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…