Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Ingekuwa ina ukweli asilimia 100, Warusi wenyewe wanaojitawala huenda wangekuwa watawala wa hii dunia mpaka sasa.
 
Hapana professor, takwimu na nimeattach link ya Reuters inaonyesha jinsi Ujerumani inaizidi kupunguza utegemezi wa Gas ya Russia In fact Germany inategemea gesi ya Norway kuliko ya Russia


So sielewi kivipi iwe reliant kwa gas ya Urusi wakati Kuna alternatives
 
Mkuu embu kuwa serious basi.
 
Ukweli wa hiyo theory unapimwa kwa impact ya yankiuchumu wa Russia duniani.Mgogoro wa Uchumi unayoikumba Ulaya nzima na USA imetokana na vikwazo vilivyowekwa na wao wenyewe dhidi ya Russia.

Issue ya vikwazo kwa Russia imepelekea kuyumba kwa uchumi wote wa Dunia,hii ni kutokana na ukweli kuwa Russia amesababisha Currency ya USA ($) kuyumba vilevile masoko ya mitaji na dhamana kwenye masoko ya USA na Europe kuyumba-hali iliyopelekea Nchi zote kuyumba kiuchumi.

Asiyelijua hili hana akili na asiyetaka kulikubali basi ubongo wake una kamasi.
 
Issue ni kuwa kwa zaidi ya miaka 150 hakujapatikana hizo njia mbadala zitakuja kupatikana Leo?,hata wakisema wasitegemee mafuta na gasi kama njia kuu ya nishati chochote watakacho kibuni kitahitaji resources na hizo resources lazima utakwenda Russia tu.

Kwa sasa hata ukimyenga Russia ukimbilie katika Nchi zingine bado ni Yale Yale issue itakuja kwenye reserve ya hiyo Nishati Nchi nyingi zinazo hizo nishati but kwa ujazo gani?? Kabla hawajaishiwa.Vipi swala LA gharama ambalo litaongeza gharama za ualishaji Mara dufu.
 
No it's not true, ingekua pesa ni nyingi kuliko bidhaa basi kungetokea hyperinflation kama iliyotokea kipindi cha Great Economic Depression.

I would request actual data to back this fact.
Mkuu unabisha kuwa USA ha print pesa ambayo haiendani na production yake?
USA ame print USD kama njugu na kupeleka Ukraine.
 
Gharama za kuzifata huko zilipo mpaka kuzifikisha kwao ni kubwa kuliko kuzifata za Urusi....Sana Sana wameziwekea baadhi ya 'vigingi' kama adhabu mfano 'price cap' kwenye mafuta ya Urusi pekee.

Hakuna Price cap iliyofanikiwa na Crude oil imeanza kupanda tena. Labda useme ni Price cap ipi umefanikiwa mpaka sasa.
 
Mkuu unabisha kuwa USA ha print pesa ambayo haiendani na production yake?
USA ame print USD kama njugu na kupeleka Ukraine.
Mkuu The Boy Wonder amekiri kwamba pesa ya USA ni reserve currency na kwamba Kila nchi inaitumia kwenye kufanya biashara kimataifa so hata siku Moja supply ya dollar haiwezi kuzidi demand ya dollars kwenye biashara ya kimataifa.

Hata Tanzania tunaprint Hela sana ila wakati Gani inaongezwa au inapunguzwa kwenye uchumi is strictly regulated to avoid hyperinflation
 
Ndoto za asubuhi, kama wangekuwa na uwezo huo wangethubutu waone. Mbona nchi nyingine wanavamia iweje isiwe Urusi?! Siku hao wamagharibi wakithubutu ndio utakuwa mwisho wao. Wamejaribu vikwazo tu lakini nchi zao hazikaliki ni fujo za wenyewe kwa wenyewe kila kukicha watu wao hawaitaki nato na umoja wa ulaya...
 
Waivamie ya Nini wakati imeshindwa vita? Hivi Russia kuiteka Kiev imeshindikana kwa zaidi ya mwaka Sasa ndio sembuse wapambane na NATO?

Hivi Kuna Taifa lilikua na nguvu kuliko USSR? ila iliporomoka kirahisi tu ndio sembuse a weakened Russia?

Wanachohofia ni madhara ya vita tu yatakua makubwa ila sio kwamba wanaogopa kushindwa vita.
 
Yetu macho tusubiri.
 
Iraq hawakuogopa madhara ya kivita mkuu.
 
Ni maandalizi.
Russia alijiandaa kwa haya, Donetsk ilikaribia kujitenga mwaka 2014. Separatist chini ya makamanda kama Motorola na Givi walikaribia Kuichukua Mauripol, kabla ya kupewa order ya Kusitisha kutoka Kremlin.

Nadhani Russia ilijipima msuli wake, ikajiona haiwezi kuwasupport kama ikiwekewa vikwazo kwa wakati ule. Wamejipanga na 2022 wamerudi tena. Kwahiyo si ajabu uchumi wao kutoanguka kama ilivyotarajiwa. Westerns either hawakulijua hili au walipuuzia lakini wakati wanaweka vikwazo walitarajia internal disputes ziiangushe russia, walichosahau ni kuwa Mpaka January 2022 kupeleka jeshi Ukraine ilikuwa ni stance ya wapinzani.

Wamefanya nini? Wameuondoa uchumi wao kutoka kwenye utegemezi wa magharibi ( japo sio asilimia 100), na wakifanikiwa kuikamata Afrika basi hawatokamatika.
 
Niliuliza swali hili maksudi kutaka kupima uaelewa wako wa mfumo mzima wa BRETTON WOODS. Ila ukanijibu kwamba haiwezekani fedha zikachapishwa nyingi kuliko bidhaa za masokoni. Ulinishangaza sana ndugu mchumi. Binafsi, nikakwambia siyo kweli na nikakuwekea Money Base (MO) ya Marekani na mahesabu yake, ila ukaendelea kubisha. Kwanini, hukuzingatia kikokotoo nilichokiweka ndugu mchumi na ukaendelea kubisha, ???

Mosi, Kiufupi ni kwamba, kadiri mataifa mengi yanavyopunguza matumizi ya dola uchumi wa Marekani na dunia nzima uko hatarini mno. Hili ni suala ambalo wengi hamjaliona tangu huu mgogoro uanze. Uvamizi wa Ukraine ni geresha tu, ila vita yenyewe ipo kwenye uwanja wa kiuchumi na inalenga kumuumiza Marekani zaidi. Marekani ana mengi ya kupoteza kuliko Urusi kwasababu, udhaifu wake mkuu uko kwenye dola (The Dollar is America only ultimate weapon).

Pili, wakati vita ya pili ya dunia inaisha Marekani ndiyo taifa lililokuwa na dhahabu yote ya dunia. Kumbuka biashara na mikopo baina ya mataifa mengine ya Marekani ilitolewa kwa dhahabu. Vita inakaribia kuisha, kila dhahabu ya duniani hapa ilikuwepo Marekani. Mwaka 1944, wakafanya kikao na kuamua kwamba kwasababu Marekani ndiyo taifa lenye dhahabu yote duniani, basi dola ndiyo iwe, The International Reserve Currency. Mataifa yakasaini, The Bretton Woods Agreement.

Tatu, dola ya Marekani mbali na kuwa chombo cha manunuzi, ikawa ni moja ya bidhaa muhimu kwenye soko la dunia ambayo inauzwa na taifa la Marekani peke yake. Hivyo ili mataifa mengine yaweze kufanya biashara za kimataifa, yalitakiwa yaende Marekani kununua dola ndiyo yafanye biashara. Utaratibu ukawa ni kwamba, taifa inabidi liuze bidhaa zake zisizopungua thamani ya dola 100 ili kupata dola kadhaa za kimarekani. Ikumbukwe Marekani, anachapisha hizi fedha kwa gharama (Seigniorage) ya dola 0.5.

Nne, mbali na hili, mataifa yakawa yanazipata hizi dola kupitia taasisi za kifedha za Marekani kwa njia ya mikopo au uwekezaji kwenye masoko ya hisa na hati-fungani za kimarekani. Hivyo soko la mitaji na dhamana la Marekani likageuka kuwa kubwa mno kupita kiasi. Utaratibu ukawa hivi: Taifa kama Uingereza, linaenda kununua dola za Marekani ili kufanya biashara ya kimataifa, ila baada ya kupata faida inazichukua hizo fedha tena na kwenye kuziwekeza nchini Marekani kwenye soko la mitaji ili Marekani azizungushe na kuwapa faida.

Hivyo fedha zinatoka Marekani na kurudi Marekani na kurudi Marekani. Marekani anachofanya ni kuwapa Makaratasi yaliyochapishwa tu. Hata kama hajapata faida, anachapisha fedha anawapa maana mnazihitaji kufanyia biashara ya kimataifa.

Tano, mchezo huu ulienda hadi kufika mwaka 1969. Mataifa ya Ulaya kama Ufaransa yakaanza kulalamika kwamba dunia nzima tunaupa ruzuku uchumi wa Marekani (The Entire World is subsidizing American Economy), jambo ambalo ni kweli. Bahati mbaya sana ikafahamika kwamba dhahabu ambayo ilikuwa imeunganishwa na fedha ya Marekani imeisha. Ufaransa chini ya Charles De Gaulle wakaanza kwenye kubebe dhahabu yao Marekani.

Hali ya Marekani ikageuka kuwa mbaya kufika mwaka 1970, na ikategemewa kwamba dola ndiyo ilikuwa inaenda kuanguka. Raisi Richard Nixon akaihakikishia dunia kwamba angefanya marekabisho kwenye mfumo mzima wa fedha wa dunia, endapo mataifa yatakubali kuendelea kutumia fedha ya Marekani, ndipo wakasaini makubaliano ya Bretton Woods II. Wewe kama mchumi, ulitakiwa uwe unayafahamu vizuri haya.

Sita, mfumo wa Bretton Woods II, ulimtaka Marekani na yeye akubali kuingiza bidhaa kutoka nchi nyingine na kwenda kuwekeza viwanda vyake nchi za nje ambako kuna gharama rahisi na mataifa mengine yakawekeza pamoja na Marekani. Haya makubaliano yaliiokoa dola ambayo ilikuwa inaenda kuanguka. Hivyo ukitaka kuelewa vizuri uchumi wa dunia unaendaje, ni lazima ufahamu kilichotokea mwaka 1965-1975.

Saba, Marekani baada ya kuona amebanwa, hana dhahabu na amekaliwa kooni na mataifa mengine akaamua kuacha kabisa mfumo wa matumizi ya dhahabu, The Gold-Standard. Akatumia mbinu ya kiakili kwamba aende kufanya makubaliano na mataifa ya kiarabu kwamba yatumie fedha ya kimarekani kwenye biashara zao zote za mafuta. Hivyo akatengeneza mfumo mpya uitwao, The Petro-Dollar System. Ambapo nishati ilikuwa ndiyo bidhaa muhimu, lakini ni lazima inunuliwe kwa fedha za kimarekani.

Mataifa ya kiarabu yakawa matajiri ndani ya muda mfupi na Marekani akawa hayagusi kabisa. Hivi unadhani wakina Mfalme Faisal wa Saudi Arabia, walivyomuwekea Marekani vikwazo vya mafuta mwaka 1973, waliitoa ile jehuri wapi, ??? Marekani alikuwa anawategemea waarabu, na wao wanamtegemea Marekani. Anahitaji mafuta ya mwarabu, lakini anahitaji zaidi dola iendelee kutumika na mataifa ya duniani.

Nane, Marekani alivyoachana na matumizi ya dhahabu, akaanza kutumia fedha makaratasi ambazo zimepewa thamani na benki kuu (Fiat Currency). Hapa ndipo akapata nguvu zaidi. Akiwa anahitaji kufadhili bajeti yake au kupata fedha ya kupambana vita baridi, alikuwa anachapisha fedha nyingi tu. Utofauti na mataifa mengine ni kwamba Marekani anachapa fedha bila kuwa na woga wa mfumuko wa bei kwasasabu fedha yake itanunuliwa tu na mataifa mengine, ambayo yatakuja tena kuwekeza Marekani. Hili ndilo lipo mpaka leo hii.

Tisa, ili kuongeza fedha kwenye soko la mitaji na fedha, benki kuu (The Federal Reserve) ikaamua kupunguza kabisa riba hadi kufika 0.6%. Ambapo mikopo kutoka kwenye mabenki ikawa ni ya bei rahisi mno hadi kwa watu wa chini kabisa. Watu wakawa wanakopa sana halafu wanawekeza fedha hizo kwenye masoko ya hisa na hati-fungani. Wamarekani wengi wakageuka kuwa matajiri, ili utajiri wako ndiyo huo ambao msingi wake ni fedha za makaratasi.

Ndiyo maana masoko ya dhamana ya Marekani yakitikisika kidogo tu, lazima uone mabenki yanafungwa na watu maelfu ya watu kuumizwa. Sasa, nikakuuliza makusudi kabisa, kwamba unadhani Marekani alivyopandisha riba (Hiking Interest Rates) kutoka 0.6% hadi kufika 6% ndani ya mwaka 2022, ni jambo la kawaida, ???

Wewe ukanijibu ni jambo la kawaida maana uchumi ndivyo ulivyo. Nikashangaa mno, imekuwaje wewe ambaye huwa una akili umembwela kama washabiki wengine wa humu ndani wasiokuwa na ufahamu wa mambo!!! Mpaka sasa sijapata majawabu.

Kumi, Mradi wa NORD-STREAM II, baina ya Urusi na Ujerumani ulikuwa ni wa matrilioni ya fedha na ulitegemewa ufanywe kupitia fedha za Ulaya na Urusi. Marekani alitaka ufanywe kupitia dola na mwishowe alivyoona mwanya akaamua kulipua kabisa mabomba ili mradi ufe kibudu. Mengi yamejificha na wengi badi hatujang'amua tu. Hii vita inalenga zaidi kumuumiza Marekani, Ukraine ni geresha tu.

NB 1: Lengo la mataifa kama Urusi, Saudi-Arabia, Uchina hata Ufaransa, yanafahamu kabisa kupambana na Marekani kijeshi ni kujitakia matatizo (Is courting death), maana Marekani ndiyo taifa lenye jeshi kubwa na linaloogopesha zaidi hapa duniani (They're armed to the teeth). Mbinu rahisi kabisa ya kumkomesha ni kucheza na mfumo wa fedha wa dunia ambako ndiko kuna udhaifu mkubwa, ili watu wapoteze imani ya kuwekeza kwenye masoko ya fedha ya Marekani.

Kama leo Marekani amenyang'anya fedha za Urusi (Foreign Reserves) ambazo aliziwekeza kule Marekani, unadhani mataifa kama Uchina ambalo limewekeza sana kwenye dola za Marekani kwa kununua deni la Marekani (Treasury Bills) ataziacha fedha zake nchini huko bila kuogopa kwamba siku yeye akivamia Taiwan atakutwa na yanayomkuta Urusi, ??? Hebu fikiri.

Mwisho kabisa, Marekani ana deni la taifa la Trillion 31 ambalo kiuhalisia limeshavuka uwezo pato lake la taifa. IMF wanasema nchi inakuwa na deni stahimilivu pale ambapo halivuki asilimia 70% ya GDP ya taifa hilo. Bahati mbaya deni la Marekani limevuka. Ila kwanini, Marekani hajapata, Default kama mataifa mengine, ???

Sababu ya kwanza ni kwamba, deni la Marekani lipo katika dola za kimarekani.
Sababu ya pili ni kwamba, kama Marekani anachapisha tu dola zake ili kufanya marejesho.

Upande mwingine, taifa la Marekani mbali ya kuwa na deni kubwa la trilioni 31, ina uhaba wa bajeti wa dola za Kimarekani Trilioni 1.15. Ila Marekani anaendelea kudunda tu kwasababu, anaweza kuchapisha fedha ili kukidhi mahitaji ya bejeti. Fedha za makaratasi zikizidi, hata nyinyi watanzania mtaenda kuzinunua tu ili muweze kufanya biashara za kimataifa.
===============================================================
BAADA YA KUELEZANA HAYO, BASI ZINGATIA HAYA YAFUATAYO:

Kipindi cha UVIKO, serikali ya Marekani ilichapisha dola za kimarekani Trilioni 1.9, ambazo hata mimi binafsi nilizipata. Hizi ni fedha nyingi mno ambazo ni makaratasi (Money Made Out of Thin Air) yaliyopewa thamani. Bahati mbaya sasa, kabla ya hizi fedha hazijaingia vizuri kwenye mzunguko, ili mataifa mengi wanunue vita vya Ukraine ikaanza.

Tangu vita ianze, Dola imepungua mzunguko kutoka 75% dunia nzima hadi kufika 59% ndani ya mwaka 2022 peke yake. Hili ni hatari mno kwa Marekani. Jambo kama hili mara ya mwisho lilitokea mwaka 2000 baada ya Tech-Bubble na September 11. Ndiyo, dola haiwezi kuanguka kirahisi maana hakuna fedha mbadala kwa sasa inayoaminika (No Alternative Reserve Currency of Similar Confidence). Asilimia 46% ya soko la dhamana na mitaji dunia nzima liko katika fedha ya Marekani na wadua wake wawekezaji wakubwa ni Japan, Uchina, UAE, Saudi-Arabia nk

Nimefurahi sana kuona bwana Econometrician ameelewa kinachoendelea. Uvamizi wa Ukraine ni geresha tu. Hatari yenye iko kwenye uchumi, maana wakubwa wameamua kuvimbishiana misuli na kukomoana. OPEC wanamvimbia Marekani kwasababu wanafahamu kwamba wao ndiyo wameshikilia karata ya mwisho ya uhai wa dola ya Kimarekani. Marekani analifahamu hili na hawezi kufanya lolote. Siku Saudi Arabia wakiacha kutumia dola kwenye biashara ya mafuta, ndiyo basi tena, The Collapse of Bretton-Woods II.

NB 2: Kama dola ya Marekani itaendelea kupungua mzunguko, basi hata nguvu yake kiuchumi na faida anazozipata kutokana na kuchapisha fedha makaratasi zitapungua. Pia haya yafuatayao yanaweza kutokea:

1. Marekani itashindwa kulipa deni lake kupitia kuchapisha fedha (Defaulting)
2. Marekani itashindwa kupata fedha za bajeti, (America has a huge budget deficit)
3. Marekani itaagiza bidhaa za nje kwa gharama mno kwasababu hatatumia fedha zake tena.
4. Marekani itakumbwa na tatizo kubwa la mfumuko wa bei usioisha (Hyper-Inflation)
5. Masoko ya hisa ya Marekani yataanguka vibaya mno na dunia nzima tutaumizwa.

Ndugu Zitto JR, kama hadi hapa hujaelewa chochote, basi sidhani kama ntakushauri chochote kile ukanielewa. Niliuliza swali kuhusu AUSTRALIA, ambalo linaendana na hali ilivyo nchini Marekani, ila ukakwepa kunijibu. Ungeyafahamu ya AUSTRALIA, basi ungefahamu ni wapi Marekani kama taifa anajikwaa hadi kufika hapa alipo, japo yeye ni taifa kubwa sana.
 
Nimetaja vipimo vitatu. Kama hutaki taja vya kwako unavyotumia mwenyewe vinavyosema Urusi ana uchumi mkubwa. Na ututajie ni ya ngapi kiuchumi duniani
Siku zote uchumi unaotokana na mikopo ni uchumi hewa si himilivu hasa ukipata tatizo la kijamii au kiuchumi. Kwa mfano ukienda benki kukopa ni kweli UNAKUWA na fedha mfukoni lakini siku mwenye fedha akizihitaji na ukawa unazo pungufu ya alizozikukopesha au ukawa umeshindwa kulipa mkopo Kwa kadri ya makubaliano atatanga mali ulizo nazo ili ziuzwe kufidia fedha zake. Kama ulikuwa na nyumba au shamba litauzwa na utabaki masikini kuliko kabla hujakopa. Gdp ya mkopo si ya kuringia. Russia ameshinda hii vita ya kiuchumi Kwa sababu alikuwa na vitu muhimu ambavyo kama nchi mukivikosa vinaleta taharuki kubwa nchini kimaisha na kiuchumi.

1.CHAKULA
Urusi ni mzalishaji mkubwa wa chakula na anategemewa na dunia nzima , Kwa hiyo wananchi wake hawakuona kupanda kwa bei ya chakula ila kupungua Kwa bei baada ya soko la nje kusuasua.

2.Mafuta
Baada ya baadhi ya nchi kususa kununua mafuta yake aliyateremsha
bei Kwa soko la ndani na nchi marafiki Kwa hiyo wananchi kupata nafuu ya maisha, pia kupata masoko mapya Kwa nchi marafiki.

3.
Gesi
Baada ya ulaya kususa kununua gesi yake na hujuma kufanyika kwenye mfumo wa kupereka gesi ulaya ,alihimalisha soko la ndani Kwa kuweka unafuu wa bei.
Hivyo ndivyo vitu muhimu vinavyogusa wengi hivyo kufanya wananchi wa kawaida kutokuona mfumuko wa bei unaoathiri maisha yao.

4.
ZANA ZA KIJESHI.
Vita inakomba Hera nyingi hasa za nje kama unategemea kila ZANA uiagize nje ya nchi kama ilivyokuwa kwetu wakati wa vita ya Kagera. Mtihani huu Urusi kaushinda Kwa kuwa na akiba kubwa ya siraha na uzalishaji unafanyika ndani ya nchi, Kwa hiyo alichofanya ni kuongeza tu uzalishaji wa siraha.

Mambo hayo hapo juu ndiyo yalifanya uchumi wa Russia usitetereke huku waliomwekea vikwazo na wenye uchumi wa madeni wakipata mdororo wa uchumi. Unajidai kula kuku Kwa fedha ya mkopo ha ha ha ....!
 
Yani wewe jamaa unaulizwa vizuri tu lakini unajibu kama mwanamke mjamzito.
 
Kufupi ni kwamba vikwazo vyote walivyomuwekea Urusi vimefeli vibaya mno . Na hii ni kwa sababu Putin alikuwa ameshajipanga kabla ya kuivamia Ukraine, kitu ambacho mataifa ya Magharibi yalikuwa hayakijui
 
Umenirudisha darasani kwa Historia na Uchumi , shukrani mkuu 👏🏾👏🏾👏🏾
 
Kufupi ni kwamba vikwazo vyote walivyomuwekea Urusi vimefeli vibaya mno . Na hii ni kwa sababu Putin alikuwa ameshajipanga kabla ya kuivamia Ukraine, kitu ambacho mataifa ya Magharibi yalikuwa hayakijui
Nimezungumza na baadhi ya wachumi humu ndani. Nikawauliza hivi ni sahihi kusema kwamba taifa ni dhaifu kiuchumi kwa kuzingatia tu, uchumi wa kifedha, Finance Economy. Bila kuzingatia uwezo wa nchi kwenye uchumi wa bidhaa, Commodity Economy, ???

Maana uchumi wa Urusi ni mdogo mno kuliko hata ule wa Italia, ila sasa madhara ya kumtenga Urusi kiuchumi na kidiplomasia yamekuwa makubwa mno na kuumiza pande zote. Hata Marekani, EU na G7 walisema kwamba wangeweka vikwazo ambavyo vingeangusha uchumi wa Urusi ndani ya wiki chache. Je, walikosea kuangalia ukubwa na nguvu zao kwenye jicho la, Finance Economy, peke yake, ???

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…