Uchumi hautenganishwi na siasa. Sera za uchumi zinatolewa na wanasiasa na uchumi unaongozwa kwa mlengo wao. Mambo ya kiuchumi kama industrialization, trade, treaties, kujenga Panama na Suez, uwepo wa Fed, gold standard na kila kitu cha kiuchumi kinaanzia kwenye siasa. Wanasiasa wana uwezo wa kuharibu au kukuza uchumi, siasa haiachi kitu kwenye nchi. Ndio maana wanapiga kura kwa wanasiasa, hawapigi kwa wakuu wa majeshi ili waongoze jeshi wanavyotaka, hawapigi kwa Chairman wa Central bank au Governor wake.
Baada ya kusababisha mfumuko wa bei kwa Magharibi, Russia imekuwa ya ngapi kiuchumi ambayo haina mfumuko?
Baada ya Waarabu kuiwekea Marekani oil embargo mwaka 1973 kama adhabu ya kuisadia Israel kwenye Yom Kippur war, Marekani ikafeli uchumi sio?
Finland mwaka jana imefungiwa gesi kabisa kabisa na Urusi, umeona wamepungukiwa nini cha ajabu?
Urusi yenyewe imepandisha interest rate mwaka jana. Na kwani hizo rasilimali za OPEC ni za Urusi? Yaani Iran, Qatar, Saudi Arabia au Kuwait waache kuuza mafuta kukuza uchumi wao wamsikilize mtu kaamua kuanzisha ugomvi?bUnategemea watu wana oil-dependet economy wazime visima ili kuikomesha Western ambao ndio wateja wao, wamsikilize Russia ambaye ni mshindani? Sababu za OPEC kusitisha kuuza rasilimali kwa West ni zipi, yani Russia wenyewe hawajasitisha sembuse OPEC.
Sababu walijiweka kwenye utegemezi wa gesi ya Urusi. Na Urusi ambavyo haina siasa za akili (jambo unalopinga kwamba tusizungumzie siasa) wameamua kuihakikishia Ulaya kwamba wao sio dependable kwenye nishati, muda wowote wanazira na kutishia kuzima mara kupunguza flow. Alternatives hata kama ni expensive zinatafutwa, subiri miaka kadhaa uone watishia gesi wataiweka wapi. Russia wanatumia gesi kama silaha, Western wanatumia uchumi kama silaha.
Je, Russia haijapata recession?
Kwani huo mwaka 2008 mabenki yalikuwa insolvent sababu ya nini au nayo ni Urusi. Urusi kwa maamuzi ya kiuchumi na kisiasa ina uwezo mdogo kuharibu uchumi wa dunia. Marekani kwa sera mbovu za siasa inaweza poromosha uchumi wa dunia, China nayo inaweza fanya jambo ikaharibu. Urusi atatumia nguvu nyingi kuharibu uchumi duniani, labda aamue naye kujiua kiuchumi.
Je data za mabenki ya Urusi zinasemaje, mabenki yao yanakua au yako insolvent.
Mbadala ila wa gharama kubwa upo, unahitaji miaka kadhaa ya kujiandaa. Hata hivyo Urusi haitoi gesi bure, kama haitaki hiyo hela basi ifunge mabomba tuione itaishije. More than 15% ya mapato yao yanategemea gesi na mafuta, wafunge kwa wengine wote waiachie China na India pekee. Wakati huo China ina mikataba na nchi kama Saudi Arabia, haiwezi chukua kiasi kikubwa zaidi kwa Russia wala haiwezi chukua kila flow kutoka kwao.
Alafu Warusi milioni 144 ambao hawana hata purchasing power ni negligible kwenye uchumi wa dunia. Urusi mwaka jana hata magari waliyonunua hayafiki nusu ya waliyonunua Brazil.
Tufanye sababu ni Russia. Sasa imekuwa ya ngapi kiuchumi baada ya kuifanya Fed ipandishe interest hadi asilimia 6?
Ni kipi Russia imepata mpaka useme imefanikiwa kiuchumi, au ni kipi Marekani imekosa.
Lini Gazprom au Rosneft imeacha kuuzia Ulaya gesi?
Ukiachana na Nord Stream 2 ambayo pipeline imelipuliwa na sidhani kama ilikuwa imekamilika, gesi inaendelea kuuzwa. Kwanini wasipate hela sasa kama bei ya soko ni nzuri.
Au ni vikwazo gani vilisema ni marufuku Russia kuuza nishati, sanasana waliweka threshold kwenye mafuta watakaonunua. Na ni nchi chache zilifanya hivyo.
Hiyo ni India. Wapi imeandikwa kwamba Urusi ikiwekewa vikwazo India ishuke kiuchumi? Yani Yanga ichukue kombe, uulize kwanini TP Mazembe haifanyi usajili.
Kama unataka ziende sawa, kwanini Russia ilivyovamia Ukraine na India haikuivamia Pakistan au China.
Alafu soko la hisa la Urusi likawa la ngapi kwa thamani ya makusanyo ya mitaji baada ya masoko ya Ulaya kuanguka?
Urusi soko lake la hisa hata masoko makubwa duniani halipo.
Na je ni mara ya kwanza masoko ya hisa Ulaya kuanguka, je mara zote yanaangushwa na Urusi?
Ni maamuzi ya kiuchumi ya nchi hizo. Au hizo phenomena zimeanza leo baada ya Urusi kuwekewa vikwazo?
Sababu kuna sarafu nyingine nyingi zenye kuwa mbadala wake kama GBP, CAD, Swiss Franc, RMB, Euro, Yen na nyinginezo. Lakini katika hizo usitarajie kuiona RUB maana haina maana kwenye exchange duniani.
Na huoni aibu kabisa unataja USD inatumika 55% duniani. Si unajua inayofuata kwa kutumika zaidi inatumika kwa asilimia ngapi?
Wakati huo Russia hizo sio level zake, imekalia kuchimba ardhi na kuuza maliasili.
Narudi palepale. Russia hakuna anayetaka kuiua kiuchumi, hivyo haijawa survival wa kitu ambacho hakipo. Kila siku ukiwa unajihisi unafuatwa na majambazi alafu unafika salama nyumbani utaamini wewe ni bingwa wa kujilinda kumbe wasiwasi wako.
Marekani iache kuua nchi ya pili mpaka ya 10 kwa GDP, iende kuua ya 11 ambayo inabadilishana na South Korea kwenye hiyo nafasi.