Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

kwa lugha rahisi hapo, tajiri ni mwenye mahindi (maana akipandisha bei au akigoma kuuza wewe mwenye milioni utahangaika sana kupata mbadala, au pengine ukipata itakua bei juu mno,

ndipo ile nadharia kwamba ulaya magharibi ni maskini (pengine kuliko afrika) inapoingia,..... leo tukisema kila mtu aishi kwa kutegemea alichonacho, basi wale wenzetu wanaweza kufa sana,

na hii ndiyo inayombeba Urusi, ana bidhaa ambazo ulaya wanazihitaji ili waendelee kuishi na uchumi wao usitetereke pakubwa,......
Ingekua hivi Afrika tusingekua maskini, hata hayo mahindi bila mbegu au viwatilifu na madawa shambani au mashine ya kugeuza mahindi yawe unga unategemea ununue kwa mwingine hakunaga closed economy iliowahi fanikiwa maana hakuna nchi inayojitosheleza kwa vyote.

Having said that, soko la chakula halipo Russia pekee so hii assumption sijui inatoka wapi. Na unaposema atauziwa chakula kwa bei ghali kivipi wakati dollar ni superior kuliko currency nyingi sana duniani ikiwemo hiyo ya Urusi so kwa namna yoyote there's nothing expensive to a dollar.

Kingine food reserve ya USA inaweza sustain crisis sio wajinga kiasi wasubiri crisis ya vita ifike eti hawana chakula. Tanzania tu Tuna stock ya chakula inayoweza sustain miezi zaidi ya 6 bila kuzalisha ndio sembuse USA au Eurozone?

Narudia Tena ulimwengu wa Sasa what matters ni money sio bidhaa otherwise barter trade ingekua inatumika mpaka leo. Ukibisha fuatilia nchi zote zinazotegemea extractive industry kama dhahabu au mazao yakishuka thamani kwenye soko la kimataifa basi na nchi inaporomoka kiuchumi.

Uchumi is all about value addition which money is the attached value on any product ikicheza hiyo hata uwe na chakula matani na matani tutaishia (kumbuka hatugaiwi Bure) tutauziwa Mchele kilo kwa elfu 5 ilihali tunalima Mpunga wa kutosha hapa Tanzania kuliko hata huko Ulaya.

CC The Boy Wonder
 
Mbona Ulaya na Marekani wananunua bado rasilimali muhimu kutoka Urusi na kuendelea kuwekeza nchini humo, kama ambavyo Uchina na India wanafanya. AU haya ninyi wataalamu wetu hamyaoni jamani, ???

Takwimu za UN zinasema kwamba, Urusi na Ukraine kwa pamoja ndiyo wauzaji wakubwa wa mazao ya chakula. Wanaendelea kusema kwamba asilimia 44% ya nafaka kutoka bahari nyeusi imeenda kwa wateja ambao ni mataifa makubwa ya Ulaya na Asia (High Income Countries).

Juzi Urusi katijoa kwenye The Black Sea Grain Deal, na angalia nini kimetokea. Takwimu za masoko ya dunia zinasema baada ya Urusi kujitoa tu kwenye huo makakati hapo majuzi, bei ya nafaka imepanda kwa asilimia 3% nzima ambayo ni sawa na senti 689.25 kwa kibaba kimoja (689.25 Per Bushel). Hii inamaanisha bei ya chakula itapanda sana na kuchochea mfumuko wa bei (Food Price Inflation) kule Ulaya na sehemu nyingine duniani.

Hapa hata upandishe riba juu (Hiking Interest Rates) kiasi gani ili kupambana na mfumuko wa bei, huwezi kufanikiwa. Njia rahisi ya kudhibiti mfumuko wa bei itakuwa ni kutafuta rasilimali, na siyo zenye uhaba na kuziingiza kwenye soko. Fedha zitapoteza thamani na nguvu ya manunuzi itaisha.

Hili nimemwambia ndugu yangu zitto junior , ila yeye anaamini kwamba huu utajiri wa vitu visivyoonekana (Imaginary/ Incorporeal wealth) ndiyo njia sahihi ya kupata taswira halisi ya uchumi wa nchi. Binafsi hili linanipa ukakasi, kwasababu tokea karne za 17 tulitumia vyote, (Utajiri unaoonekana na Utajiri usioonekana) kupima taswira ya utajiri na uchumi wa nchi.

Sasa narudia maswali yangu, tena;

Mosi, imekuwaje taifa ambalo ni asilimia 4% ya Uchumi wa dunia isababishe mfumuko mkubwa wa bei ya chakula kwenye soko la dunia hadi kuathiri nchi tajiri za G7 ambazo zinamiliki asilimia 37.7% ya uchumi wa dunia, ???

Pili, Je dunia na wachumi walikuwa sahihi kuacha kuangalia utajiri wa nchi kwa kurunzi ya Finance Economy peke yake bila kuzingatia Commodity Economy, ???


Jibu ni rahisi tu. Urusi siyo Zimbabwe. Ina sifa zote ambazo ulimwengu wa magharibi unazo. Lakini lililo kuu zaidi, Urusi ina rais mzoefu kwenye siasa za dunia, mahiri na mwenye nia ya dhati kabisa ya kuleta uwiano na usawaziko wa nguvu za kisiasa na kiuchumi.
 
Hapa wengi naona tunashindwa kukubaliana kwamba wewe mwenye milioni(pesa) ndani ili uile(uitumie) lazima awepo mwenye mahindi ndani. So ni lazima kwanza yawepo mahindi ndo mwenye pesa anaweza kuishi na ndo kinachotokea kwa West vs Russia
Kwamba soko la mahindi ni Russia peke yake na hakuna chakula alternative mpaka ununue hayo mahindi?

Food,oil and medical reserves iliyoko USA ni kubwa kuliko hata tuliyonayo sisi watu weusi. Lakini inatunzwa mpaka kukiwa na crisis kama vita na sio kutumika kwa sasa ambapo options za kununua Bado zipo.

The State of U.S. Strategic Stockpiles

Sasa nchi kama hiyo kweli ndio ianguke kisa Russia kagoma kuuza bidhaa zake? Let's be realistic.

The only explanation ni imported inflation kwamba kama sisi Tanzania tunanunua mafuta,gesi au ngano itokayo Russia au Middle East technically bei zetu zitapanda mfano utalii, dhahabu n.k so obviously kama ulihitaji dollar 100 kulala hoteli Tanzania itahitaji dollar 120 that's what we call imported inflation. Na sio directly involved na uwepo wa Russia kama producer wa gesi au mafuta au whatever.

Cc: The Boy Wonder
 
Narudia Tena mkuu, uchumi sio zero sum game ndio maana ukipunguza ajira uchumi haukui ila pia ukiongeza ajira ghafla uchumi unaporomoka. Uchumi is all about kung'ata na kupuliza ndio maana broad money supply (Demand deposits+ Forex + Currency in circulation) huwa inapdandishwa na baada ya muda Fulani inapunguzwa (kwa kuuza au kununua hati fungani) ila ukisema uongeze Hela tu uchumi unakufa ila pia ukipunguza pesa kwa mzunguko uchumi unakufa.

Having said that unakosea pale ambapo unaonyesha kwamba uwepo wa vita ya Ukraine na Russia ndio hiyo inayopelekea inflation kupanda USA Au EU? Ulifanya hivyo lazima uweke control variables (We ni msomi unanielewa hapa) mfano macroeconomic variables kama floating interest rates (Moving average), unemployment rate, COVID 19 repurcussions, kuanguka kwa benki za USA, housing crisis, scarcity ya dollar kwenye soko la kimataifa, Sasa ukifanya test yoyote iwe Panel data au hata Pooled OLS lazima tu utaona jinsi Gani hizo factor zingine zinachangia zaidi uchumi wa EU au US uanguke na sio necessarily Kwa Russia kuzuia mauzo ya grains or whatever resources wanauza kwa EU au USA.

TLDR: You can't conclusively say factor Moja ya Russo-Ukranian War ndio directly inasababisha matatizo ya kiuchumi huko western Bloc bila controlling for other macroeconomic variables ambazo zilishaleta athari za kiuchumi since 2020.

Correlation is not causation
Umezungumza mambo mengi sana bwana Zitto. Nimekubaliana na wewe kitaalamu kabisa, kwamba UVIKO imechangia hali hii iliyopo duniani kipindi hiki. Hili limetokana na ukweli kwamba mataifa mengi kama Marekani yalichapisha fedha nyingi mno kipindi cha UVIKO na leo hii vita ya Ukraine inaonyesha haya madhara. Hakuna anayesema vita vya Ukraine peke yake ndiyo vimeleta haya madhara.

Hilo la uchumi kupanda na kushuka ni kawaida, na siyo mara zote mfumuko wa bei (Inflation) ni kitu kibaya. Mara nyingine hutumika na benki kuu kama mbinu za kuchochea maendeleo. Benki Kuu inaweza kufanya QE na QT bila kuvuka mipaka ili kutimiza malengo maalumu. Huwezi kutekeleza sera za kiuchumi bila kuweka uwiano mzuri baina ya bidhaa, huduma na masoko ya mitaji. IT IS NOT SUSTAINABLE.

Ambacho tunapishana mimi na wewe ni sehemu ndogo sana: Kwamba serikali za dunia zinaweza kutekeleza sera za kiuchumi kwa kuangalia tu masoko ya mitaji bila kuzingatia masoko ya bidhaa. Ukifanya hivi lazima uchumi upasuke (Economic Bubble). Tena nikafurahi zaidi kwamba unaanza kukubaliana kwamba ECONOMY IS NOT A ZERO-SUM GAME.

Tukitafakari katika minajili hiyo tunarudi kulekule alichokisema mwanauchumi nguli wa Uingereza, David Ricardo kwamba kila nchi ina kitu ambacho nyingine hakina hivyo badala ya kujikita kwenye kuzalisha ambavyo huna ili kujitegemea, jambo ambalo ni gharama, basi nchi lazima zijikite kwenye mambo ambayo zinaweza kuyamudu. Akatupa wachumi kanuni nzuri za kimapokeo ya uchumi, COMPARATIVE ADVANTAGE THEORY.

Ndiyo maana nikauliza swali rahisi tu: Je, ni sahihi kuangalia uchumi wa nchi kwa kuzingatia vitu kama masoko ya mitaji (Capital Markets) peke yake, bila kuzingatia rasilimali muhumi ambazo zinayaendesha na kuyashikilia hayo masoko, ???

Hebu nikupe mfano hai. Mnamo karne ya 17 taifa la India ndiyo lilikuwa moja kati ya mataifa matajiri zaidi duniani, ambapo pato lake la taifa (National GDP) ilikuwa ni asilimia 23% ya uchumi wa dunia, na ilikuwa inauza bidhaa muhimu duniani kote. Miaka yote Uingereza alipoenda kutawala India aliondoka na utajiri uliotokana na rasilimali za India wenye thamani za dola za Kimarekani Trilioni 45.

Huu utajiri ndiyo uliipa Uingereza nyongeza kwenye uchumi (A Surplus) wa Uingereza kwa miaka 30 mfululizo hata baada ya ukoloni kuisha. Binafsi nauliza ili niweze kueleweshwa ambacho ninyi wachumi wenzangu mnakifahamu, ambacho mimi bado sikielewi.

Nakubaliana na wachumi wengine kwamba masoko ya mitaji ni sehemu nyeti mno kwenye uchumi wa dunia. Lakini, undhani ni sahihi sana kiuchumi kusema mataifa ambayo hayana masoko makubwa ya mitaji ni masikini ilhali hayo mataifa ndiyo yanaendesha dunia nzima na masoko ya mitaji kupitia uzalishaji wao, ???

Mzee Nyerere aliwahi kukiri hiki ninachokisema na naomba nimnukuu "Tulikosea sana kuiga na kuamini yale tuliyoyaona kwa wenzetu wa Magharibi. Tukadhani kwamba kila king'aacho ni dhahabu, kumbe hatukutakiwa kuiga. Tulitakiwa tujikite kwenye kuangalia uwezo wa mazingira yetu kiuchumi(Comparative Advantage). Nini tunaweza kuipa dunia"

MWISHO KABISA NAMALIZIA NA HILI: Mnamo mwaka 2008 wakati wa mtikisiko wa uchumi wa dunia, sehemu zote duniani, Magharibi na Mashariki ziliathirika sana. Nchi moja peke yake, AUSTRALIA ndiyo haikuathirika hata kidogo na mtikisiko wa uchumi wa dunia. Australia ilifaidika mno na mtikisiko wa uchumi wa mwaka 2008. Unadhani sababu kubwa ilikuwa ni nini ndugu yangu mchumi, ???
 
Kwamba soko la mahindi ni Russia peke yake na hakuna chakula alternative mpaka ununue hayo mahindi?

Food,oil and medical reserves iliyoko USA ni kubwa kuliko hata tuliyonayo sisi watu weusi. Lakini inatunzwa mpaka kukiwa na crisis kama vita na sio kutumika kwa sasa ambapo options za kununua Bado zipo.

The State of U.S. Strategic Stockpiles

Cc: The Boy Wonder
Ndugu yangu mchumi, wewe umeenda shule na kujifunza kufanya uchambuzi yakinifu. Marekani imekuwa tajiri duniani kwasababu yenyewe ndiyo taifa la pili duniani kuwa na rasilimali nyingi baada ya Urusi. Marekani ana rasilimali zenye utajiri wa dola za kimarekani trillioni 45, huku Urusi akiwa na rasilimali zenye utajiri wa dola za Kimarekani trillioni 75.

Marekani ilianza kuwa nchi tajiri duniani mwaka 1872, kwasababu ilikuwa inafanya biashara ya kimataifa ya rasilimali kama ambavyo Urusi anafanya leo. Ulaya yote na Asia walikuwa wananunua bidhaa muhimu kutoka Marekani ili kuendesha chumi zao. Hadi kufika mwaka 1911, Standard Oil la Rockfeller ndiyo kampuni lilikuwa linaongoza kwa kuuza asilimia 90% ya mafuta ya dunia nzima.

Marekani ilitajirika kwa kuuza rasilimali zake kwa mataifa ya Ulaya, hili ndilo lilimpa nguvu na siyo hizi blah blah za masoko ya hisa ambazo wengi tumemezeshwa mashuleni. Haya hapa ni maneno ya William Seward, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ya Marekani kipindi cha Raisi Abraham Lincoln:

"the nation that draws most from the earth, and fabricates most, and sells the most to foreign nations, must be, and will be, the great power of the earth"

Unapotoa mifano ya namna hii, unathibitisha kwamba bila kuwa na rasilimali muhimu ambazo unazoweza kuzitumia wewe binafsi, na kuziuza kwenye soko la dunia huwezi kufika popote kama taifa.
 
Jibu ni rahisi tu. Urusi siyo Zimbabwe. Ina sifa zote ambazo ulimwengu wa magharibi unazo. Lakini lililo kuu zaidi, Urusi ina rais mzoefu kwenye siasa za dunia, mahiri na mwenye nia ya dhati kabisa ya kuleta uwiano na usawaziko wa nguvu za kisiasa na kiuchumi.
Ndugu Eliakeem nimefurahi kukuona hapa ndugu yangu, maana ni siku nyingi tangu tuachane kwenye ule mjadala wetu kuhusu kukwama kwa mradi wa bwawa la Nyerere.

Nurudi kwenye mada, binafsi najaribu kuuliza hili maswali ambayo yamenitatiza lakini naona sipati majawabu yanayoeleweka. Ukilinganisha uchumi wa Urusi na mataifa ya G7 katika kiwango cha GDP, utaona jinsi ulivyo mdogo. Ila ukiangalia katika kwenye masoko ya kimataifa, na bidhaa anazoziuza unapata taswira nyingine kabisa.


===============================================================
Hebu tuachane na Urusi, tuzungumzie taifa la AUSTRALIA. Ambapo mwaka 2008 wakati wa mtikisiko wa uchumi ulioathiri dunia yote, taifa la Australia peke yake ndiyo halikuathirika na lilipata utajiri mkubwa mno kipindi kile kuliko wakati mwingine wowote ule. Nini, kilichangia hili taifa kutoathirika na mtikisiko, ???

Hebu ndugu zangu wa muda mrefu naowaheshimu sana hapa jukwaani, Chamoto , Drifter, Wyatt Mathewson , na TUJITEGEMEE watusaidie kujibu hii hoja kuhusu AUSTRALIA.
 
Marekani ana rasilimali zenye utajiri wa dola za kimarekani trillioni 45, huku Urusi akiwa na rasilimali zenye utajiri wa dola za Kimarekani trillioni 75.
Haaahaaaa ila hii unafurahisha sana yaani ushasema thamani halisi ni bidhaa sio makaratasi ila bado umethaminisha Mali za Russia in terms of "karatasi" na sio Amount of food exports in units!!

Mkuu, world bank inasema Marekani ndio nchi inayoongoza kuuza chakula duniani hiyo Russia ni ya 14. Hapa chini ni takwimu za WITS utaona hizo data na unaweza tengeneza graph zako ku prove nachosema.


So it's funny how nchi isiyo top 10 ya top exports inaweza athiri nchi inayoongoza export food DUNIA NZIMA.

Based on data from the World Bank, these are the top 20 countries that export the most food products based on value measured in U.S. dollars:

1. United States: $89,719,182,630

2. Germany: $39,143,404,740

3. United Kingdom: $32,834,074,660

4. China: $31,656,304,900

5. Japan: $27,173,445,970

6. France: $27,139,176,830

7. Netherlands: $26,819,981,570

8. Canada: $23,787,571,660

9. Belgium: $17,693,060,460

10. Italy: $15,432,784,080

11. Russia: $14,634,336,170
 
Hiv Tz tuna kitengo cha ujasusi wa kiuchimu
/=Huyu DP-WORLD angept kwa style hii
 
Matatizo ya kiuchumi yameikumba Dunia tokea COVID 19 na recession zilizofuata. So obvious whether Ukraine na Russia zingepigana or not Bado matatizo ya uchumi yangekuwepo G7.

Kingine Russia ana survive madhara ya kiuchumi sababu amekiuka vikwazo mfano Bado anauzia mataifa mengine mafuta, gesi na chuma n.k. Kuna nchi kama China Bado inafanya trade ya wazi na Russia so hiko ndio kina sustain ila kama angesusiwa na mataifa yote sidhani angeweza sustain hata mwezi tu.

Lakini it's worth noting nchi za ulaya zimepunguza dependence na gesi ya Urusi so obviously Mapato yanaanza shuka taratibu so vita ikiendelea miaka 5 mingine watafikia break-point. Huwezi sustain uchumi wakati nchi Yako ni closed economy so Kuna limits atafika mind you vita ya Ukraine pia inammaliza pesa na watu na nguvu za kidiplomasia.

Only time will determine the fate of Russia
Mimi siyo mchumi ila nafatilia sana siasa za duniani kiuhalisia west walijidanganya na vikwazo walivyoweka labda walijua au wakafumba macho kwamba liwalo na liwe au hawakutegemea uhalisia huu wa mambo unavyotokea kwenye vikwazo walivyoweka

Mosi tukumbuke China ndiyo namba mbili kwa uchumi duniani ni mzalishaji mkubwa wa bidhaa duniani ni namba mbili kwa population duniani asingweza kufata vikwazo vya west abadani ni kuhatarisha usalama wake wa ndani mwenyewe hasa kama maandamano yakitokea kwenye nchi yenye population kubwa kama ile kwa sababu ya kupanda gharama za maisha na ukosefu wa ajira ingekuwa ngumu kuyahandle na labda umwagaji mkubwa wa damu au serilkali kuanguka vile vile kwa India na Russia alisema toka mwanzo ataendelea kufanya biashara na nchi rafiki wala hakujitenga kama ambavyo west walitaka iwe

Kama China ingekuwa west Leo hii tungesema mengine kwenye hii vita ila ndyo ivyoo uchumi wa Russia kudororo haitatokea utashuka kidogo tu hizi ni karata za marekani kwa maadui zake lakin naona zimeenda kombo na kuna hatihati inaweza muongezea China nguvu na kumpandisha kiuchumi hasa kuongezeka kwa matumizi ya pesa ya china kwenye ununuzi wa bidhaa duniani
 
Hata NATO ikaamua kumpa full support ya zana za kijeshi Russia, sidhani kama itachukua wiki Russia kutapika maeneo aliyoteka.

NATO imeona mbali uwezekano wa matumizi ya Nuclear ktk hii vita, hii wanafanya waende step kwa step hapo Ukraine.

Tukumbuke walipotenga bajeti ya miaka mitano kuisaidia Ukraine, watu waliwaona NATO kama wehu, waliona ukubwa wa Jeshi la Russia dhidi ya Ukraine basi vita isingechukua hata miezi mitatu.
Usituone wote watoto uku silahaa wanazoogopa kuzitoa ni kwasababu wanajua respond ya russi itakavyokuwa na siyo kingine tuna miezii 10 kelele za hii vitaa tutaisikia kiuchache sana
 
Marekani ilitajirika kwa kuuza rasilimali zake kwa mataifa ya Ulaya, hili ndilo lilimpa nguvu na siyo hizi blah blah za masoko ya hisa ambazo wengi tumemezeshwa mashuleni.
Kuna kitu unakosea soko la hisa hali operate hewani Bali ni value attached kwa kampuni (inazalisha bidhaa) mfano Apple inauza simu Sasa ikiingiza faida si ndio soko la fedha linapanda liquidity maana more people buy stock so sio kama fedha inaelea hewani.

Kwahiyo fedha peke yake Haina thamani unless iwe attached na bidhaa ndio maana hao Russia waliuza Alaska wakapewa "makaratasi" na hao hao wamarekani.

Kingine Kuna vitu kama ubunifu au hatimiliki au kipaji au nguvu kazi vipi utavithaminisha kwa kilo za mahindi?? Ila pesa pekee inaweza quantify intagible assets ambazo zinaongeza pia uzalishaji na maarifa yanayozaa hizo bidhaa zenyewe.

So Dunia iki focus kwenye uzalishaji wa bidhaa kama kipimo Cha uchumi mzuri vipi kuhusu intagible assets? Vipi kuhusu tatizo la kuthaminisha hiyo ngano ya Urusi Ili upate cobalt ya DRC?

Cc Gerald .M Magembe
 
Nakusoma mkuu, lakini hapa nataka nieleweshwe zaidi. Unataka kusema kwamba bila nishati kutoka Urusi, uchumi wa nchi za Ulaya hauwezi kwenda mbele ? Kwanini Ulaya wasitumie nishati mbadala (Renewables) kama umeme wa jua, makaa ya mawe, nyuklia na upepo ?


Kama ni mfumo wa kijamaa, kwanini Urusi ya kisovieti (USSR) ilianguka na kufilisika ilhali kila kitu kilikuwa kinamilikiwa na serikali ya kikomunisti ?


Benki Kuu ya Urusi ilitoa tamko mwaka 2021 kwamba asilimia 65% ya viwanda vya uzalishaji inategemea teknolojia na bidhaa kutoka nje. Hebu fanya tafiti zaidi naweza kuwa nakosea. Swali langu hapa, ni hili kama utegemezi wa bidhaa za nje ni asilimia 65% kwanini mpaka sasa uzalishaji wa Urusi haijaanguka ?


Nadhani hii inaweza ikawa moja ya sababu kubwa. Japo naendelea kusubiri nondo za wadau, watufundishe zaidi.
Mataifa ninayoyauzia nishati ni hayo hayo yananiuzia teknolojia sasa goma kuniuzia teknolojia au bidhaa nibaki na nishati yangu

Ugumu uko hapo inabidi maisha yaendelee tu kwa amani
 
Kuna kitu unakosea soko la hisa hali operate hewani Bali ni value attached kwa kampuni (inazalisha bidhaa) mfano Apple inauza simu Sasa ikiingiza faida si ndio soko la fedha linapanda liquidity maana more people buy stock so sio kama fedha inaelea hewani.
Ndugu yangu Zitto, hivi unashindwaje kufahamu kwamba masoko ya mitaji kama (Hisa, Hati-Fungani) yanashikiliwa na FEDHA. Lengo kubwa la taasisi za kiuchumi kama mabenki ni kuhakikisha fedha zinakuwepo kwenye mzunguko. Ili kuhakikisha fedha inakuwepo kwenye mzunguko ili kusukuma uchumi, ndiyo tunatumia nyenzo mbalimbali kama kuuza hisa, hati-fungani na kutoa mikopo.

Sasa nikupashe kidogo kuhusu hisa. Share/Stock is a debt instrument just like debenture or anything else. It proves someone's ownership or claim over a particular company. Kisheria hisa ni mali (Incorporeal Property) kama mali nyingine, hivyo huathirika na mfumuko wa bei, kama ambavyo bidhaa nyingine huathirika. Hili nalo lina ubishi gani, ???

Buying stocks, buying bonds, hedging or taking loans are tools used by governments to keep money within the economy.
Kwahiyo fedha peke yake Haina thamani unless iwe attached na bidhaa ndio maana hao Russia waliuza Alaska wakapewa "makaratasi" na hao hao wamarekani.​
Moja ya kitu kinanisikitisha kuhusu wewe ni kwamba wewe una akili lakini umeshindwa kujituma zaidi. Kuhusu mauzo ya Alaska, mimi niliyasoma nikiwa mwaka wa pili chuo kikuu. Urusi alinunua Alaska kwa vipande vya dhahabu, siyo fedha za makaratasi. Hata Louisiana nayo ilinunuliwa kwa vipande vya dhahabu kutoka ufaransa.

Kiufupi ni kwamba, kabla ya mwaka 1972 dunia yote ilikuwa inatumia The Gold-Standard, na siyo pesa za makaratasi. Fiat Currencies zimeanza kutumika baada ya BRETTON-WOODS II. Hata mikopo ambayo Marekani aliitoa kwenye vita zote za dunia, ilitolewa kwa mfumo wa dhahabu. Mbona suala rahisi kama hili linakupita wewe mchumi, ???
Kingine Kuna vitu kama ubunifu au hatimiliki au kipaji au nguvu kazi vipi utavithaminisha kwa kilo za mahindi?? Ila pesa pekee inaweza quantify intagible assets ambazo zinaongeza pia uzalishaji na maarifa yanayozaa hizo bidhaa zenyewe.
Intellectual Property & Entertainment, and Population fall within a category of labor markets. And like Capital Markets, Labor Markets are affected by money. If there's Inflation hitting the economy making money lose its value, even the labor market becomes a victim too. They do not exist in isolation.

Yes, a bushel of maize can cause a disruption even in Hollywood and Silicon Valley...
 
Haaahaaaa ila hii unafurahisha sana yaani ushasema thamani halisi ni bidhaa sio makaratasi ila bado umethaminisha Mali za Russia in terms of "karatasi" na sio Amount of food exports in units!!
Ndugu Mchumi kwani huelewi kwamba, Currency is:
1. A Debt Instrument
2. A Store-Hold of Wealth

Nikiwianisha mali kwa fedha za makaratasi ambazo zina mali nyuma yake (Backed or Pegged to Gold) sioni tatizo lolote lile. Narudi palepale, fedha ambayo imechapishwa bila mpangilio maalumu na kupewa thamani na Benki Kuu (Fiat Currency) ni moja ya tatizo ambalo limetufikisha hapa leo.

Ndugu Mchumi, sijaona sehemu yoyote umenijibu swali langu kuhusu AUSTRALIA....

 
Ndugu Eliakeem nimefurahi kukuona hapa ndugu yangu, maana ni siku nyingi tangu tuachane kwenye ule mjadala wetu kuhusu kukwama kwa mradi wa bwawa la Nyerere.

Nurudi kwenye mada, binafsi najaribu kuuliza hili maswali ambayo yamenitatiza lakini naona sipati majawabu yanayoeleweka. Ukilinganisha uchumi wa Urusi na mataifa ya G7 katika kiwango cha GDP, utaona jinsi ulivyo mdogo. Ila ukiangalia katika kwenye masoko ya kimataifa, na bidhaa anazoziuza unapata taswira nyingine kabisa.


===============================================================
Hebu tuachane na Urusi, tuzungumzie taifa la AUSTRALIA. Ambapo mwaka 2008 wakati wa mtikisiko wa uchumi ulioathiri dunia yote, taifa la Australia peke yake ndiyo halikuathirika na lilipata utajiri mkubwa mno kipindi kile kuliko wakati mwingine wowote ule. Nini, kilichangia hili taifa kutoathirika na mtikisiko, ???

Hebu ndugu zangu wa muda mrefu naowaheshimu sana hapa jukwaani, Chamoto , Drifter, Wyatt Mathewson , na TUJITEGEMEE watusaidie kujibu hii hoja kuhusu AUSTRALIA.
Australia???


Ngoja niende gugo
 
Intellectual Property & Entertainment, and Population fall within a category of labor markets. And like Capital Markets, Labor Markets are affected by money. If there's Inflation hitting the economy making money lose its value, even the labor market becomes a victim like any other market. They do not exist in isolation.
Ndio nauliza kama bidhaa ndio thamani ya uchumi je intangible assets kama IP na Knowledge mfano ya udaktari au ukandarasi ambaye haiwezi kuwa valued na kilo za ngano je huoni makaratasi ya pesa ni nyenzo nzuri ya kufanya fair valuation ya hizi intangible assets?
Sasa nikupashe kidogo kuhusu hisa. Share/Stock is a debt instrument just like debenture or anything else. It proves someone's ownership or claim over a particular company. Kisheria hisa ni mali (Incorporeal Property) kama mali nyingine, hivyo huathirika na mfumuko wa bei, kama ambavyo bidhaa nyingine huathirika. Hili nalo lina ubishi gani, ???

Buying stocks, buying bonds, hedging or taking loans are tools used by governments to keep money within the economy.
Naona haujanielewa, ndio nasema apple sio kampuni halisi?? Haiuzi electronics? Sasa apple imeuza bidhaa say za shilingi 100 ina maana Kila aliyeweka hisa say anapewa shilingi 1 Sasa hapo debts na loans zinaingiaje wakati it's actual money changing hands at real time?

Mie siongelei financial markets kama za wanunua madeni, factors sijui intermediaries n.k ila naongelea real companies selling real products ila mtaji na faida haweki na kuchukua mtu mmoja Bali ni watu wengi waliokuja pamoja kuendesha kampuni.

Sasa basi kama Kuna actual bidhaa zinauzwa how comes una term mauzo ya hisa ni kama pesa inayoelea hewani tu bila actual value attached to gadgets za apple?

Kingine gold is more scarce than "makaratasi ya pesa" hivyo it would only get expensive na nchi chache pekee zingeshikilia uchumi wa Dunia and things would get rough. Ila FIAT money allows hata nchi kama South Sudan kuattach value kwenye bidhaa zake bila kuhitaji kuwa na dhahabu kwenye reserve yake.

Kingine unaweza kma dhahabu is everything sababu Imepewa thamani na watu other than that Kuna rare metals kuliko dhahabu na Zina thamani zaidi. Hata Sasa tumeona demand ya madini kama cobalt imepanda sababu Kuna uhitaji wa electronic gadgets.

Having said that, hivi ukiwa na dhahabu ila hauna Mchele shida si Ile Ile kama unayoikosoa pesa maana itahitaji tu utafute mwenye Mchele akuuzie au utakula dhahabu?

So matatizo ya gold standard ni mengi kuliko faida zake, inakua ni kama lotto kwamba wanaoshinda ni wachache kuliko wanaokosa.

So dhahabu sio pesa zenyewe kama zenyewe hazina thamani unless ziwe attached na value ya bidhaa Fulani ndio uchumi unazunguka hivyo otherwise barter trade ingekua inafanya kazi mpaka Leo.
 
Ndugu yangu Zitto, hivi unashindwaje kufahamu kwamba masoko ya mitaji kama (Hisa, Hati-Fungani) yanashikiliwa na FEDHA. Lengo kubwa la taasisi za kiuchumi kama mabenki ni kuhakikisha fedha zinakuwepo kwenye mzunguko. Ili kuhakikisha fedha inakuwepo kwenye mzunguko ili kusukuma uchumi, ndiyo tunatumia nyenzo mbalimbali kama kuuza hisa, hati-fungani na kutoa mikopo.
Ni kweli Hati fungani inaongeza au kupunguza pesa kwenye mzunguko ila Sasa swali linakuja kwanini tusichapishe pesa nyingi tukawa tunampa Kila mtu say aende china akanunue viwanda? Au tusichapishe pesa nyingi tununue Boeing hata 100??

Sababu ni kwamba pesa za makaratasi lazima ziwe at par na thamani ya bidhaa zilizopo sokoni Ili kuensure velocity of money, volume, and currency in circulation zinaendana na upatikanaji wa resources. Sababu pesa zikiwa nyingi kuliko bidhaa ndio utahitaji malori ya pesa kununua Mchele kilo Moja so lazima wakati ambapo bidhaa ni nyingi ila wanunuzi hamna ndio mzunguko wa pesa unaongezwa ila wenye pesa wakiwa wengi kuliko bidhaa then serikali inaondoa pesa kwenye mzunguko.
 
ukweli kwamba mataifa mengi kama Marekani yalichapisha fedha nyingi mno kipindi cha UVIKO na leo hii vita ya Ukraine inaonyesha haya madhara. Hakuna anayesema vita vya Ukraine peke yake ndiyo vimeleta haya madhara.
Na ndio hapa mzizi wa mada, kwa kiasi gani macroeconomic factors zimechangia economic crisis au inflation ya Sasa? Maana trust me bila hata vita Bado uchumi unge shake maana watu walikua hawazalishi?

Na kuchapisha pesa sio kosa as long as zinakua at par na uzalishaji uliopo? Mfano hapa Tanzania JPM alitoa trillion 1 kwa mabenki Ili yakopeshe watu wanunue mbegu walime, wenye kampuni za utalii wazifufue n.k Sasa pesa thamani ya bidhaa ilipotengemaa kwa uzalishaji ndio pesa ikaondolewa Tena kidogo kupitia tozo n.k Ili Ile trillion 1 iondolewe kwenye mzunguko kabisa.

Uchumi ndio unafanya kazi hivyo Wala hakuna kitu kama pesa kuchapishwa nyingi na ikaendelea Baki kwenye mzunguko
 
Ndio nauliza kama bidhaa ndio thamani ya uchumi je intangible assets kama IP na Knowledge mfano ya udaktari au ukandarasi ambaye haiwezi kuwa valued na kilo za ngano je huoni makaratasi ya pesa ni nyenzo nzuri ya kufanya fair valuation ya hizi intangible assets?
Mchumi hebu tufanya mambo yawe marahisi na tuipe mada mipaka.
1. Kipimo kipi kinatumika kupima utajiri wa mataifa, ???
2. Nini kitu gani hufanya taifa moja liwe na uchumi mkubwa zaidi ya jingine, ???

Nadhani tuanzie hapa, bila kwenda huko kwingine tunapoteza mwelekeo wa mada...
 
Ni kweli Hati fungani inaongeza au kupunguza pesa kwenye mzunguko ila Sasa swali linakuja kwanini tusichapishe pesa nyingi tukawa tunampa Kila mtu say aende china akanunue viwanda? Au tusichapishe pesa nyingi tununue Boeing hata 100??

Sababu ni kwamba pesa za makaratasi lazima ziwe at par na thamani ya bidhaa zilizopo sokoni Ili kuensure velocity of money, volume, and currency in circulation zinaendana na upatikanaji wa resources. Sababu pesa zikiwa nyingi kuliko bidhaa ndio utahitaji malori ya pesa kununua Mchele kilo Moja so lazima wakati ambapo bidhaa ni nyingi ila wanunuzi hamna ndio mzunguko wa pesa unaongezwa ila wenye pesa wakiwa wengi kuliko bidhaa then serikali inaondoa pesa kwenye mzunguko.
Mchumi, hebu nisaidie: Hivi leo BOT ikaamua kufanya QE ili kuingiza fedha kwenye mzunguko, au tukachapisha fedha nyingi ambazo zikapelekea kuwa na Money Base (MO) kubwa ambayo inazidi bidhaa na rasilimali zilizoko sokoni na upatikanaji wa rasilimali, nini kitatokea, ???

Swali langu kuhusu Australia, mbona hunipi majibu mchumi ???
 
Back
Top Bottom