Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?

Apple Stocks have a lot to with the company itself, than products alone.
Kabla mtu hajanunua hisa anaangalia performance ya kampuni mfano Return on Assets, Return on Equity, Net Interest Margins n.k Sasa kama bidhaa zako haizuziki sokoni obvious ratio ya returns to investments itakua ndogo sababu Kuna gharama kubwa ipo incurred kwenye patents, material, labor costs, marketing etc. So obviously performance ya I phone au gadgets zozote za Apple Zina impact its value maana hisa kuuzwa or not mtu anaangalia atapata dividends kiasi gani in case of future profits.

Excerpt from their website
In 2022, the iPhone generated over $205 billion for Apple, making up over 52% of the company's revenues.

Sasa kama I phone pekee tu inachangia zaidi ya nusu ya Mapato ya Apple how comes useme Haina mchango kwenye thamani ya kampuni? Hivi tukiondoa 50 percent of company revenue chances are that 50 percent of the company's value whether in assets, share price etc will automatically fall by a double digit figure!!
 
Swiss port Ina trade DSE but Swiss port existed as a company way before it was listed.
Even if a company is private, it still needs to have shares. Ownership companies limited by shares is done through shares, even if it is owned by two people. When a company does well, to a certain threshold, government regulators force them to do IPO. When doing IPO, banks measures INTRINSIC VALUE, which is a long time estimate of a company's performance. When a company goes off to sell stocks, we start to measure a company's current value through MARKET VALUE.

And hey, being LISTED is not always an option. Sometimes, it is a mandatory requirement, especially, when a company has reached a certain level of growth. In America if a company has accumulated a capital, worth $ 1 Billion (A Unicorn Status), then it has to go public. But moderate capital companies, subject to regulations of a state, can go public in order to accumulate capital.

Mkuu Zitto, Much Respect kwako, UISHI MILELE.
Ntakuona baadaye kwasasa ngoja nikafanya mambo mengine.


 
Mkuu, Unafahamu maana ya Liquidity Swap Lines na zinafanyeje kazi, ???
Halafu pia nisaidie ni kwanini hayo mataifa ndiyo yanapewa dola kirahisi, ???
Tukipata haya majibu mawili tutakuwa na mwanga wa kufahamu kuhusu volume..Nasubiri!

Econometrician hebu tusaidiane hapa, Liquidity Swap Lines zinafanyaje kazi,....!!
Hiyo ni lugha tu ya kiuchumi ila ni mikopo kama mikopo mingine tu ya dollar hasa wakati ambapo Kuna crisis na hizo swap lines hazipo fixed Kuna wakati zinapandishwa or in other cases kuwa limitless kwa mataifa kama Japan au UK.

Na kama ambavyo benki haikopeshi tu Kila mtu hata US haiwezi weka dollar available kwa Kila nchi maana mwisho wa siku default rate inaweza kuwa kubwa hivyo dollar isirudi na interest ama ikaishia mikono mibaya ya competitors.

Pia ni regulations tu maana ukiwa na few people holding more dollars it's easy to monitor kuliko ikiuzwa kiholela huwezi regulate mwisho wa siku Ina back fire.

On the other hand, volume or whatever can be affected by the actual availability ya hizo dollar maana kama nyie mnadai sijui dollar zilichapishwa nyingi kuliko mahitaji kivipi Tena recently kulitokea scarcity ya dollar hapa Tanzania na nchi nyingi duniani kiasi dollar ikawa inauzwa na walanguzi kwa bei ya juu sana cha ajabu mnadai imezidi mahitaji.

So labda Econometrician au Gerald .M Magembe aweke sawa.

1. Je Kuna uhusiano wowote wa Quantitative Easing na mfumuko wa bei.

2. Je Quantitative Easing ya dollar ya Marekani umezidi mahitaji ya soko la kimataifa?

3. If that's the case kivipi isemekane volume ya mzunguko wa dollar imepungua from 75% to 57%?

4. Je volume kupungua haimaanishi supply ipo chini? Yaani kivipi Kuna scarcity of dollars whilst wakati huo huo quantitative Easing imezidi demand?

Nadhani haya maswali 4 ndio yatatupa mwanga
 
One, the value of products like iphones are determined by Apple itself. The corporation considers many things like, the cost of production, governmental regulations, intellectual property etc. Here they can choose to overvalue a damn thing. But, the prices of Apple shares, initially they are determined by many factors, considered by regulators on long term basis. This is what we call Intrinsic Value. When Apple products like iphones are selling well in the Market, the current value measured is what we call, a Market Value. And legally, this is a sympathy value
Naelewa sana unachozungumzia Mimi nilichokataa ni ku assume kwamba value ya Apple Haina corelation na mauzo ya bidhaa!! Kama ni hivyo basi Value ya Nokia mbona haipandi? Kuna thousands of publications kuonyesha that value ya bidhaa mfano movie za Marvel zimepandisha thamani ya kampuni na sio sababu ya artificial valuations Bali real performance kwenye marker otherwise nipe mfano wa kampuni ambazo products zake zinafeli ila thamani ya kampuni collectively inapanda??

Kingine unasema over valuation ndio nikauliza je dhahabu zinazouzwa Nairobi Zina thamani sawa na zinazouzwa Rome au London? means hata commodities are vulnerable to overvaluations meaning your initial points kuwa only financial markets are prone to over valuing and speculations is rather obsolete.
 
Emerging Markets/Emerging Markets
Excuse my french, but I thought China is an emerging economy alongside BRICS economies at least based on world bank classifications sio "Developed Economy" ya level za OECD.
Hivyo kupata dola kwake siyo shida kwasabubu yeye ndiyo soko kubwa la kibiashara la Marekani
Kwahiyo tunakubaliana kwamba commoditiy prices haziwezi kuwa sawa maana Kuna nchi kama China zinashusha thamani ya pesa means utanunua Mpunga mwingi china kwa dollar 1 kuliko ukinunua soko la London?? Which is actually what I said kwamba rather than benchmarking ila bei Zina vary sokoni.

Nitakupa kitabu kizuri, kimeyaweka haya mambo kwa urahisi mno....
Nitashukuru sana
 
Mbona Ulaya na Marekani wananunua bado rasilimali muhimu kutoka Urusi na kuendelea kuwekeza nchini humo, kama ambavyo Uchina na India wanafanya. AU haya ninyi wataalamu wetu hamyaoni jamani, ???

Takwimu za UN zinasema kwamba, Urusi na Ukraine kwa pamoja ndiyo wauzaji wakubwa wa mazao ya chakula. Wanaendelea kusema kwamba asilimia 44% ya nafaka kutoka bahari nyeusi imeenda kwa wateja ambao ni mataifa makubwa ya Ulaya na Asia (High Income Countries).

Juzi Urusi katijoa kwenye The Black Sea Grain Deal, na angalia nini kimetokea. Takwimu za masoko ya dunia zinasema baada ya Urusi kujitoa tu kwenye huo makakati hapo majuzi, bei ya nafaka imepanda kwa asilimia 3% nzima ambayo ni sawa na senti 689.25 kwa kibaba kimoja (689.25 Per Bushel). Hii inamaanisha bei ya chakula itapanda sana na kuchochea mfumuko wa bei (Food Price Inflation) kule Ulaya na sehemu nyingine duniani.

Hapa hata upandishe riba juu (Hiking Interest Rates) kiasi gani ili kupambana na mfumuko wa bei, huwezi kufanikiwa. Njia rahisi ya kudhibiti mfumuko wa bei itakuwa ni kutafuta rasilimali, na siyo zenye uhaba na kuziingiza kwenye soko. Fedha zitapoteza thamani na nguvu ya manunuzi itaisha.

Hili nimemwambia ndugu yangu zitto junior , ila yeye anaamini kwamba huu utajiri wa vitu visivyoonekana (Imaginary/ Incorporeal wealth) ndiyo njia sahihi ya kupata taswira halisi ya uchumi wa nchi. Binafsi hili linanipa ukakasi, kwasababu tokea karne za 17 tulitumia vyote, (Utajiri unaoonekana na Utajiri usioonekana) kupima taswira ya utajiri na uchumi wa nchi.

Sasa narudia maswali yangu, tena;

Mosi, imekuwaje taifa ambalo ni asilimia 4% ya Uchumi wa dunia isababishe mfumuko mkubwa wa bei ya chakula kwenye soko la dunia hadi kuathiri nchi tajiri za G7 ambazo zinamiliki asilimia 37.7% ya uchumi wa dunia, ???

Pili, Je dunia na wachumi walikuwa sahihi kuacha kuangalia utajiri wa nchi kwa kurunzi ya Finance Economy peke yake bila kuzingatia Commodity Economy, ???

Kaka umeni-inspire sana naomba nikucheki DM kama hutojali
 
Mkuu, Unafahamu maana ya Liquidity Swap Lines na zinafanyeje kazi, ???
Halafu pia nisaidie ni kwanini hayo mataifa ndiyo yanapewa dola kirahisi, ???
Tukipata haya majibu mawili tutakuwa na mwanga wa kufahamu kuhusu volume..Nasubiri!

Econometrician hebu tusaidiane hapa, Liquidity Swap Lines zinafanyaje kazi,....!!

Tumuulize python na Library zake statmodel, scipy, keras na sckit-learn ama tusubiri kwanza?
 
Vikwazo vinauma, lakini havileti matokeo yaliyokusudiwa. Kuna kitabu nimekisoma, kimeandikwa na Nicholas Muelder kinaitwa, "The Economic Weapon: The Rise of Sanction as a tool of modern war". Kinaeleze historia ya vikwazo vya uchumi. Kuna sehemu kasema Uingereza wakati ndiyo taifa kubwa duniani, kipindi cha vita ya kwanza ya dunia, aliiwekea vikwazo Uturuki, vikaua watu laki 5 lakini vikabuma. Uturuki iliangushwa kijeshi siyo kiuchumi. Nimesoma nikawaza sana:
View attachment 2703599

Hiki kitabu nakipataje?
 
Excuse my french, but I thought China is an emerging economy alongside BRICS economies at least based on world bank classifications sio "Developed Economy" ya level za OECD.

Kwahiyo tunakubaliana kwamba commoditiy prices haziwezi kuwa sawa maana Kuna nchi kama China zinashusha thamani ya pesa means utanunua Mpunga mwingi china kwa dollar 1 kuliko ukinunua soko la London?? Which is actually what I said kwamba rather than benchmarking ila bei Zina vary sokoni.


Nitashukuru sana
China ni developed ila hataki ingia huko sababu atabanwa.
Kingine ni kuwa China kaamua peg pesa yake sababu ya unlimited dollars alizonazo kutokana na exports nyingi huku imports zikiwa chache na zaendelea pungua

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru kwa kunialika kwenye mjadala huu, Proved, japokuwa nimechelewa kujiunga. Majukumu mengine [yaliyo nje ya platform hii] yanachangia kutopatikana humu mara kwa mara.

Awali kabla ya yote, kuna suala moja la msingi sana ambalo kwa maoni yangu haliko sawa kuhusiana na mjadala wenyewe uliopo mezani.

Hoja au mada ina kichwa cha habari kinachosema: "Swali la uchumi: Kwanini vikwazo vya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi havifanyi kazi dhidi ya Urusi?"

Hiyo title pekeyake ina-demand ama inahitaji set of valid statements zinazozipa justification hoja kuu iliyomo katika title husika kwa sababu title imebeba hoja nyingine kubwa tu ambayo ni conclusion ya mjadala mwingine huru. Hoja ambayo inapaswa kusapotiwa na premises ama hoja zingine ndogondogo ili kuithibitisha. Nimeipitia mada nzima kuanzia title, introduction na context ya mjadala kwa ujumla wake. Kwa bahati mbaya, sijaziona hizo premises ambazo zinaakisi hoja iliyopo katika title ya mada ama mjadala mzima.

Ninachozungumzia ni uthabiti ama validity ya mjadala. Nitafafanua!

Hoja yoyote inayouliza "Kwanini" ama "Why" kwa kiingereza ni hoja ambayo inatumia conclusion ya hoja nyingine ambayo tayari imethibitika kuwa ni kweli (True), ili kuzibaini sababu ama reasons za kuwepo kwa huo ukweli (Truth). Ukiuliza "Kwanini kitu fulani hakifanyi kazi dhidi ya fulani?" maana yake ni kuwa hoja ama swali hilo limetumia conclusion "kutofanya kazi" kutoka katika hoja nyingine/zingine huru kujengea hoja ya "Kwanini" iliyopo mezani ambayo ndiyo mleta mada ameiwasilisha.

Ili statement "havifanyi kazi" iliyomo katika title ya mada iwe sahihi ama valid, inahitaji kusapotiwa na mtiririko wa premises, reasons, evidence, facts ama data zilizotokana na tafiti mbalimbali ili kufikia conclusion niliyoisema ya "kutofanya kazi" kisha ndipo tuingie sasa katika hoja mpya ya "Kwanini havifanyi kazi" iliyopo mezani, kitu ambacho sijakiona katika context ya mada/mjadala.

Mfano mwingine rahisi:
Kuna utofauti mkubwa kati ya general question kama "Umeenda shule leo?" na swali kama "Kwanini umeenda shule leo?".

Swali la pili hapo lenye "Kwanini" ni sahihi ama valid endapo tu conclusion "kwenda shule" inaweza kuthibitika kuwa ni kweli kwa ushahidi wa akiwemo anayeulizwa na muuliza swali mwenyewe. Kama kuna possibility yoyote ile kuwa huyo anayeulizwa hilo swali hajaenda shule siku hiyo, basi swali zima linakosa mantiki, hivyo swali sahihi linalopaswa kuulizwa kwanza pengine ni lile la kwanza.

Mfano mwingine ni kutoka katika mada yenyewe:
Swali la pili limeuliza kitu kama hiki; "Kwanini makampuni ya Urusi ya nishati ndiyo yameongoza duniani kwa kuuza zaidi nishati, ilhali yamewekewa vikwazo vikali?". Hapo kuna conclusion "kuongoza duniani" inayotokana na hoja ambayo haijaambatanishwa na facts wala data zozote zile zenye kuthibitisha statement hiyo. Swali dogo tu: takwimu sahihi za mauzo ya nishati ziko wapi?

Kwa kifupi ni kwamba, title ya mada imebeba hoja nyingine huru ambayo haina uthibitisho ukizingatia maudhui ya mada ama mjadala mzima. Vilevile, maudhui ya mjadala hayajakidhi mahitaji yenye kuyapa usahihi maswali yote yaliyowasilishwa mwishoni. Mada imejikita zaidi kuelezea superiority ya western countries kiuchumi bila ya kutupa facts zenye kusapoti title iliyowasilishwa pamoja na maswali matatu ya mwishoni ambayo ndiyo mjadala uliopo mezani.

Baada ya kusema hayo, nitaendelea kupitia michango ya wadau wengine kisha nitachangia zaidi pale ambapo nitapata muda wa kufanya hivyo. Haya ndiyo maoni yangu kwa sasa. Asante!
 
Back
Top Bottom