Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
View: https://youtu.be/R6TiVOZZZj4?si=iM4J0sv3gbtjSNmI
Waliitwa vijana...nakumbuka walipotumbuliwa nilisema ni ujana tu unawasumbua. Nikasema warudishwe labda wamejifunza. Tukaseme wapewe nafasi tena Alipokufa JPM hawakuficha hisia zao kuonesha hasimu kaondoka na wala kupima hekima walipozungumza. Tukawaangalia.
Mama alipowarudisha ni ikawa kama ni kuwaponya. Walionewa na sasa wamerudishwa ndani. Wote walipewa wizara walizozitaka sana na ambazo zilionekana zinaendana na uwezo wao. Lakini mara hizi zote wanapata shida kuongoza. Je, hawana uwezo?
Napendekeza wasipewe nafasi yoyote ya kuteuliwa tena sasa hivi. Wabaki wabunge tu ili wajipange na waoneshe wanaweza kuongoza bila kuwa mawaziri. Wabakie wabunge wa kawaida. Inawezekana upande mwingine Raisi Samia ameona siyo suala la uwezo bali kuwaondolea majaribu ya kutumia uwaziri kujijenga majimboni kuelekea 2025. Binafsi naamini kama hili ni kweli basi mawaziri wote wenye Nia ya kugombea mwakani wangetolewa ili wabakie wabunge. Mawaziri wawe wale ambao hawana Nia ya kugombea tena mwakani. Ila nadhani ni uwezo na kukosa hekima.
Maana kama kubebwa kuna watu wamebebwa bwana lakini kama mtu habebeki unang"ang'ania kumuweka mgongoni wa nini..mara akugonge konzi, mara teke, mara akufinye masikio, mara akung'ate halafu bado anataka kupanda mabegani. Kubebwa gani huko? Hata mtoto asipotulia kwenye mbeleko unamshusha bana kha!
Inawezekana kweli wa moja available mbili na aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi. Tukubali kuwa hawana uwezo maana kama hadi sasa bado hawajui hekima ya uongozi watajua lini? Watu wasiopima yanayotoka midomoni au matendo yao watapimiwa na nani...?
Wakubali yaishe?