Swali la Ugomvi: Tuseme tu Hawana Uwezo?

Kwanza siyo vijana! Ujana unaishia 35yrs.
 
Kuna mahala niliongea humu kwamba raisi alikosea sana kuwarudisha watu ambao mtangulizi wake aliwaondoa kwa sababu ambazo raisi wa sasa azifahamu.

Hivyo yawezekana kwa asilimia 80 raisi katambua kuwa hawa hawabebeki na watamtia gharama.

Asilimai 10 ni MSG kuhusika moja kwa moja na asilimia 10 ingine ni hao watu wa vetting kuchanganywa na maamuzi ya raisi pamoja na MSG.

Haya ni maoni tu huenda kuna sababu zingine ambazo zipo hewani.
 
Kuna mahala niliongea humu kwamba raisi alikosea sana kuwarudisha watu ambao mtangulizi wake aliwaondoa kwa sababu ambazo raisi wa sasa azifahamu.
Sisi tulisema tangu mwanzo kuwa hawa watu hawafai, hatukusikilizwa, na mwisho tukaishia kuitwa sukuma gang.
Mtu unapigwa chini na marais wawili mfululizo kwenye uwaziri, inaonyesha ni kiasi gani wewe ni hopeless na haubebeki hata kwa mbeleko ya ngozi!
 
Chamsingi tukiteuliwa tufanye kazi kwa bidii huku tukichunga kauli na matendo yetu yasilete mkanganyiko kwa jamii.
KAZI IENDELEE
 
Ingependeza kama hawa watu wangeomba na kupeleka C.V zao, pia kufanyike usahili ili kuypata watu wenye uwezo badala ya kuteua kutoka gizani. Wangefanya usahili pengine makosa/mapungufu yao wangeyaona wakati wa usahili, na wangeepuka usumbufu na gharama wanazoingia serikali kwa kuteua na kutumbua.
Waache Kuteua, badala yake watangaze hizi nafasi hata miezi sita kabla ili kuwe na file la waombaji, na inakuwa rahisi kuwa short list wenye uwezo na kukaa na fail zao standby ikiwa mmoja anayepata nafasi ku fail ku deliver/kufa/kustaafua au kufukuzwa.
 
Tukisema hawana uwezo tutakuwa tunakosea maana hatuambiwi kwa nini wanatumbuliwa. Ingekuwa vyema kama kutumbuliwa kungeenda pamoja na sababu ili tuepukane na idle speculations na wenzao wapate funzo la mambo gani hayakubaliki.

Amandla...
Wow!

Hata mimi leo nilikuwa nawaza kwa nini huwa hatuambiwi sababu za wao kutumbuliwa.
 

Ugomvi wana uweza sana tu sema hawajataka
 
Hivyo vijamaa viwili uwezo wao ni mdogo sana.

Makamba issue za kiungozi ni kama kazigeuza za kifamilia hawa na yule dada yake Mwamvita ndio waliamua kula kwa urefu wa kamba.

Genge lake la TANESCO kina Maharage nao hawakuwa nyuma hawa si ndio walinunua software ya kugundua eti umeme ukikatika ijulikane ni wapi kwa bilion 90 wakati umeme wenyewe wa uhakika haukuwepo.
 
Upo vizuri Paskali!!

Tuombe pia Rais akubali kwamba kazi aliyoifanya na mtangulizi ilikuwa ya kutukuka!!

Hao waliogundulika ni wabovu tangu awamu iliyopita asiwabebe! Kutaka kuonekana muungwana kwenye mambo ya nchi ni hatari. Ndio hivyo tunalalamika haya mambo ya Uteuzi na Utenguzi lakini Ukweli ni Kwa sababu hakuwa makini na alitaka kuonesha kuwa mtangulizi alikuwa mbaya.

Nami nikumbushe, ile Timu ya JPM ilikuwa ni Timu yake pia, ilifanya kazi kubwa sana. Kwa maslahi ya nchi asione shida kuirudisha hiyo Timu Ili imsaidie.

Ni ushauri tu
 
Very true Mwanakijiji, hawa jamaa walibebwa saaaaana lakini uwezo wao ni finyu sana na kiufupi ni watu wasioweza ku-deliver kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…