Swali limeulizwa huko:-kwanini wanaume hampendi kuongozana na wake zenu?

Uwe unakuja vicoba huwa tunafundishana haya, sis tumekuwa wazembe, hatuogi, hatuvai vizuri, hatutumii unyunyu na wanaume wanashindwa kutumudu wakati mashangazi na singo maza wao wapo vizuri kila idara.
sisi tukiolewa tuna relax, ni kosa kubwa sana, Ma-shangazi wanakesha saluni.
 
Aisee wako wanaume wenzetu wa hivyo na mimi sijui ni kwanini,au wanakwepa vile vi maswali 'mbona yule mdada kakutizama sana mwanamke wako nini',au utasikia 'tununue kabisa na maharage ya wiki nzima na nazi na mchicha na mkaa,wakati anajua kabisa mnaenda kwenye harusi'...
 
Minafikiri mwanamke anapaswa afaham aina na tabia za mume wake.
Mfano mie hatuwezi tukawa tumeenda Bar alafu aniulize habari za mboga sijui mkaa.... bladi hell..🀨
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…