Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
Tanzania imewahi kukumbwa na kashfa kubwa tu zilizokuwa zinahusisha mali ya asili au mali ya umma (Hakuna mali ya serikali). Kashfa kubwa zaidi ambazo zilizizima katika taifa letu zilianza miaka mingi nyuma lakini hakuna ambayo iligusa akili na fikra za Watanzania kama ujio wa kashfa ya kuuzwa kwa eneo la mbuga ya Ngorongoro kwa wawindaji kutoka Dubai. Ngorongoro imekuwa ni mtego mkubwa kwa watawala wetu; mtego ambao ni jaribu ambalo hawawezi kulishinda. Hili nitakuja kulizungumzia baadaye inshallah.
Hayo yalifanyika wakati wa Mwinyi. Lakini baadaye yake akaja Mkapa na Kikwete. Hawa ni watu kutoka bara. Ukisikiliza watu wanavyozungumza leo utadhani kuwa wakati wa Mkapa na Kikwete hakukuwahi kutokea kashfa kubwa zilizohusisha mali za umma na mali asili. Na inawezekana tuna vijana wanaoingia mitandaoni siku hizi na kukuta kuna kashfa na wanadhani zimeanza leo. Niwakumbushe tu kashfa kadhaa nyingine:
- Kashfa ya Ununuzi wa Airbus 320
Hizi ni chache tu; na zimetokea wakati wa "marais wa bara". Ufisadi ni ufisadi tu; haujalizi anayeufanya anatokea wapi. Tusimpinge au kupinga sera za Rais Samia sababu ya Uzanzibari wake. Hatukumpinga Mkapa sababu ya kabila lake au sehemu anayotoka; alijiuzia Kiwira!!! Kikwete hakupingwa sababu ya kuwa anatoka Msoga au mtu wa pwani! Kuna watu walimpinga Magufuli kwa sababu hawakukubaliana naye na of course hakuna aliyesema wanampinga kwa sababu ni Msukuma (sic) au kwa sababu anatoka Chato! Hakupingwa kwa sababu ya asili yake.
Ndugu zangu, kila Mzanzibari ni Mtanzania japo si kila Mtanzania ni Mzanzibari. Kila Mngoni (raia wa Tanzania) ni Mtanzania japo siyo kila Mtanzania ni Mngoni. Tukielewa hili tutaweza kujenga hoja za kupinga bila kuonekana ni wakabila mambo leo!

- Kashfa ya Sukari
- Kashfa ya Meremeta
- Kashfa ya Deep Green Finance
- Kashfa ya Richmond
- Kashfa ya Dowans
- Kashfa ya EPA (escrow account) (humu kulikuwa na mambo ya Daud Balali - tushamsahau)
- Kashfa ya CIS
- Kashfa ya Kuuzwa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira