Swali Muflisi: Kwani Hawa Walitoka Wapi?

Unataka kutetea kitu gani?
Not all haya’s are kagasheki but all kagasheki are haya’s. Namanisha sio kila wahaya wote ni kina kagasheki maana kuna Kuna kina Mulokozi kabyemela, mwijage, binamungu etc. Ila ukisikia jina kagasheki fahamu kuwa ni muhaya.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tanzania imewahi kukumbwa na kashfa kubwa tu zilizokuwa zinahusisha mali ya asili au mali ya umma (Hakuna mali ya serikali). Kashfa kubwa zaidi ambazo zilizizima katika taifa letu zilianza miaka mingi nyuma lakini hakuna ambayo iligusa akili na fikra za Watanzania kama ujio wa kashfa ya kuuzwa kwa eneo la mbuga ya Ngorongoro kwa wawindaji kutoka Dubai. Ngorongoro imekuwa ni mtego mkubwa kwa watawala wetu; mtego ambao ni jaribu ambalo hawawezi kulishinda. Hili nitakuja kulizungumzia baadaye inshallah.

Hayo yalifanyika wakati wa Mwinyi. Lakini baadaye yake akaja Mkapa na Kikwete. Hawa ni watu kutoka bara. Ukisikiliza watu wanavyozungumza leo utadhani kuwa wakati wa Mkapa na Kikwete hakukuwahi kutokea kashfa kubwa zilizohusisha mali za umma na mali asili. Na inawezekana tuna vijana wanaoingia mitandaoni siku hizi na kukuta kuna kashfa na wanadhani zimeanza leo. Niwakumbushe tu kashfa kadhaa nyingine:

  • Kashfa ya Sukari
  • Kashfa ya Meremeta
  • Kashfa ya Deep Green Finance
  • Kashfa ya Richmond
  • Kashfa ya Dowans
  • Kashfa ya EPA (escrow account) (humu kulikuwa na mambo ya Daud Balali - tushamsahau)
  • Kashfa ya CIS
  • Kashfa ya Kuuzwa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira
-Kashfa ya Ununuzi wa Rada
- Kashfa ya Ununuzi wa Airbus 320

Hizi ni chache tu; na zimetokea wakati wa "marais wa bara". Ufisadi ni ufisadi tu; haujalizi anayeufanya anatokea wapi. Tusimpinge au kupinga sera za Rais Samia sababu ya Uzanzibari wake. Hatukumpinga Mkapa sababu ya kabila lake au sehemu anayotoka; alijiuzia Kiwira!!! Kikwete hakupingwa sababu ya kuwa anatoka Msoga au mtu wa pwani! Kuna watu walimpinga Magufuli kwa sababu hawakukubaliana naye na of course hakuna aliyesema wanampinga kwa sababu ni Msukuma (sic) au kwa sababu anatoka Chato! Hakupingwa kwa sababu ya asili yake.

Ndugu zangu, kila Mzanzibari ni Mtanzania japo si kila Mtanzania ni Mzanzibari. Kila Mngoni (raia wa Tanzania) ni Mtanzania japo siyo kila Mtanzania ni Mngoni. Tukielewa hili tutaweza kujenga hoja za kupinga bila kuonekana ni wakabila mambo leo!
Daudi Bilal ukumbuke alikuwa ni "Bangusilo" hakuwa na Nia ovu , kama ilivyokuwa kwa Ndullu na wengineo waliokuwa "Gavana" Benki kuu labda hata Waliokuwa viongozi wa Taasisi zingine nyeti . Tatizo ni Wana Siasa na chawa wetu ndio wanaotuharibia wanataaluma wetu. Na waza watoto wetu ambao tunawasomesha Kwa shida na gharama kubwa , tunawafundisha nini. Tunawataka waje wawe wezi, wala rushwa, waonezi nk,. Na Mwisho kuna mambo ya DP weldi, kuna Anani-Tisc ambao ulikwisha Isha , sasa mtu anaendeleaje mkataba Kwa mgongo WA Tisc ulisha kama sio kukwepa Ile Sheria ya manunuzi, kuna mambo ya Tunesco, msd, nhif, na ripoti za SiAji za mwendokasi nk
 
Sisi vijana wa sasa wengi wetu tuna MIHEMKO....

Ndani yake kunaweza kupatika ubaguzi wa KIKABILA ,KANDA ,RANGI ama KIDINI.....

Mzalendo gani wa kuwa na tabia hizo ?!!

Mzalendo gani wa kutoa LAANA...kumlaani kiongozi wake bila ya kujua kuwa ukimlaani kiongozi anayeongoza eneo ulilopo basi UNALILAANI hilo eneo.....

Hoja hujibiwa kwa hoja na si vioja vya "Argumentum ad hominem"[emoji1787]

#Say No To Bigotry [emoji7]
#Say No To Racism[emoji7]

#Say No To Religious Hatred[emoji7]

A saying of the sages "never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeable".

TANZANIA KWANZA KABLA YA NAFSI YANGU [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kama huwezi kupingana nao, basi jiunge nao.
Na katika wamaasai kuna moja kasema Baba au Mama Mzuri ni Yule anayekupa chakula, matibabu, na vitu vingenevyo muhimu ili uione Kesho yako. Hivyo ni vizuri ukazingatia Hilo.katika kufanya shughuli zako .
 
Ndivyo ninavyochukulia... Zanzibar si nchi.
Lakini hawa walikuwa na Deni la Tunesco je ni mkoa Gani Wana Deni la Tunesco. Na Deni Hilo sasa limefutwa. Ingawa Zesco walilipwa hizo bill za umeme na watumiaji wa huo umeme, zikaliwa na mende wa Znz, Sisi ndio tulipishwa mzigo huo
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tanzania imewahi kukumbwa na kashfa kubwa tu zilizokuwa zinahusisha mali ya asili au mali ya umma (Hakuna mali ya serikali). Kashfa kubwa zaidi ambazo zilizizima katika taifa letu zilianza miaka mingi nyuma lakini hakuna ambayo iligusa akili na fikra za Watanzania kama ujio wa kashfa ya kuuzwa kwa eneo la mbuga ya Ngorongoro kwa wawindaji kutoka Dubai. Ngorongoro imekuwa ni mtego mkubwa kwa watawala wetu; mtego ambao ni jaribu ambalo hawawezi kulishinda. Hili nitakuja kulizungumzia baadaye inshallah.

Hayo yalifanyika wakati wa Mwinyi. Lakini baadaye yake akaja Mkapa na Kikwete. Hawa ni watu kutoka bara. Ukisikiliza watu wanavyozungumza leo utadhani kuwa wakati wa Mkapa na Kikwete hakukuwahi kutokea kashfa kubwa zilizohusisha mali za umma na mali asili. Na inawezekana tuna vijana wanaoingia mitandaoni siku hizi na kukuta kuna kashfa na wanadhani zimeanza leo. Niwakumbushe tu kashfa kadhaa nyingine:

  • Kashfa ya Sukari
  • Kashfa ya Meremeta
  • Kashfa ya Deep Green Finance
  • Kashfa ya Richmond
  • Kashfa ya Dowans
  • Kashfa ya EPA (escrow account) (humu kulikuwa na mambo ya Daud Balali - tushamsahau)
  • Kashfa ya CIS
  • Kashfa ya Kuuzwa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira
-Kashfa ya Ununuzi wa Rada
- Kashfa ya Ununuzi wa Airbus 320

Hizi ni chache tu; na zimetokea wakati wa "marais wa bara". Ufisadi ni ufisadi tu; haujalizi anayeufanya anatokea wapi. Tusimpinge au kupinga sera za Rais Samia sababu ya Uzanzibari wake. Hatukumpinga Mkapa sababu ya kabila lake au sehemu anayotoka; alijiuzia Kiwira!!! Kikwete hakupingwa sababu ya kuwa anatoka Msoga au mtu wa pwani! Kuna watu walimpinga Magufuli kwa sababu hawakukubaliana naye na of course hakuna aliyesema wanampinga kwa sababu ni Msukuma (sic) au kwa sababu anatoka Chato! Hakupingwa kwa sababu ya asili yake.

Ndugu zangu, kila Mzanzibari ni Mtanzania japo si kila Mtanzania ni Mzanzibari. Kila Mngoni (raia wa Tanzania) ni Mtanzania japo siyo kila Mtanzania ni Mngoni. Tukielewa hili tutaweza kujenga hoja za kupinga bila kuonekana ni wakabila mambo leo!

Kuwafukuza Wamasai Ngorongoro kwa hoja kwamba tunalinda mfumo wa ikolojia na kisha kuwakaribisha wanaukoo wa Mfalme wa UAE waje kukaa Katika eneo hilo hilo la Ngorongoro ni utekelezaji wa sera ya ubaguzi wa rangi inayotofautisha makazi ya Waafrika na Waarabu, yaani ukaburu mamboleo

1724507516289.png

Paul Makonda akiwa na Rais wa UAE anayemiliki kampuni ya OBC inayofanya uwindaji wa kibiashara huko Ngorongoro. Picha hii imepigwa Arusha tarehe 30 Juni 2024 kwa kutumia kamera ya kikachero iliyofichwa katika saa ya mkononi. Waandishi wa habari huru hawakuruhusiwa na simu zote zilikatazwa katika eneo la tukio. Lakini wakasahau kuwa hata saa za mkononi siku hizi ni kamera za kazi maalum.

Tofauti na Mwanakijiji anavyofikiri, katika masuala ya state security management swali linalouliza ubini wa mtu haliepukiki, na ndio maana tunatofautisha uraia wa kuzaliwa na uraia wa kununua.

Swali hili, kwa mfano, linatusaidia kuwatambua watu wenye hulka ya kusigina ukuu wa nafsi ya kiutu, yaani personal sovereignty.

Kuna ukuu wa nafsi ya kiutu unaomhusu binadamu mmoja mmoja (natural personal sovereignty) na ukuu wa nafsi ya kiutu unaohusu taasisi (corporate personal sovereignty) kama vile kampuni, ngo, kaya, kijiji, and kata, and wilaya, and mkoa na taifa.

Kutokana na historia ya Waarabu ya kujihusisha na biashara ya utumwa, and ukoloni na ubaguzi wa rangi hapa Afrika na huko Asia, ni wazi kuwa Waarabu wengi wanaanguka katika kundi hili, kama hakuna ushahidi wa kukanusha hitimisho hili.

Yaani Wengi wao wanaamini kuwa hakuna tofauti kubwa kati ya Mwafrika na "mbwa mpumbavu."

Hata Rais Samia juzi akiwa kwenye tamasha la kizimkazi ameonekana akitamka maneno yanayoashiria kwamba anaamini hivyo pia.

Historia ya aina hii peke yake ni ushahidi wa awali, and yaani necessary evidence, but not sufficient evidence. Yaani sio ushahidi unaojitosheleza.

Unaweza kutoshelezwa na kanuni ya "matunda hutambulisha jina la mti, kama ambavyo matendo hutambulisha jina la mtu."

Yaani tunautambua mti kwa kuangalia matunda yake.

Vivyo hivyo tunatambua fikra na mtazamo wa mtu kwa kuangalia matendo yake na kusikiliza maneno yake.

Yaani matendo ya mtu katika wakati wa sasa yanatueleleza yeye ni nani, maana matendo haya humbatiza majina. Mfano:

  • Ukiiba unaitwa mwizi,
  • Ukidanganya unaitwa mwongo,
  • Ukiwaita watu wanaokukosoa "mbwa wapumbavu" unaitwa mtukanaji,
  • Ukiwa mtoza ushuru unaitwa Zakaya kama Ruto wa Kenya,
  • Ukifanya biashara ya utumwa unaitwa msiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu, yaani the violater of personal sovereignty,
  • Ukitenganisha mwili na roho ya mtu baki unaitwa muuaji,
  • Ukimkamata mtu baki na kumpeleka mafichoni kinyume cha matakwa yake unaitwa mtekaji
  • Ukitumia madaraka ya ofisi yako kwa ajili ya kutafuta maslahi binafsi katika namna inayopindisha haki za watu baki unaitwa mla rushwa,
  • Ukivujisha siri za nchi yako kwa maadui wa nje ya nchi unaitwa mamluki yaani double agent,
  • Ukiwa mkuu wa nchi ukaamua kumega kipande cha nchi na kumgawia mjomba wako anayeishi ughaibuni unaitwa mvunja nchi au msaliti.
  • Ukiwa mkuu wa nchi ukatumia madaraka yakl kuwafukuza watu kama vile wamassi kutoka eneo fulani na kisha kulifanya eneo hilo kuwa makazi ya Waarabu unaitwa mkaburu mamboleo
  • Na orodha inaendelea.

Kwa ufupi, mleta mada wetu ameshindwa kutofautisha kashfa zinazoinua foreign companies sovereignty dhidi ya domestic people's sovereignty, yaani ukuu wa nafsi ya kiutu ya watu wa Tanzania. Taifa la Tanzania ni corporate person.

Na hii Kashfa ya Loliondo ni mojawapo ya kashfa zinazosigina ukuu wa nafsi ya kiutu ya dola ya Tanzania tena tangu 1995.

Lakini kwa sasa kashfa hii imepata msukumo maalum chini ya uongozi wa RC Mkonda na Waziri Mchengerwa wanaotekeleza maagizo ya siri ya Rais Samia kwa faida ya Waarabu wa UAE.

Yaani Kasi ya kusigina ukuu wa nafsi ya kiutu ya dola ya Tanzania imeongezeka.

Sasa ombi la OBC la kumegwa rasmi pande la nchi imetekeleza kisheria kwa kufuta vijiji, and kata na tarafa kadhaa.

Hili ni kosa linalofanywa katika mazingira ambayo yanaashiria kuwa huenda tunao viongozi wakuu sita (rais, makamu rais, waziri wa sheria na katiba, mwanasheria mkuu, waziri mkuu na jaji mkuu) wasiojua wala kuheshimu kanuni ya "personal sovereingty, both natural sovereignty and corporate soveteignty. "

Na mara nyingi, kashfa ya Loliondo imekuwa ikiwahusisha marais wazanzibari, wenye nasaba ya Kiarabu.

Katika zama zao tunashangawa na matukio yanayoonekana bayana kutendwa na "drifting agents" na wao wapo wanatazama tu kiasi wkamba wao wanageuka "drifting principals."

Wateule wa Rais wanaonekana wazi kuwa katika michezo ya "agent slack" na "agent shirking" na Rais anaunga mkono kila mtu kula kwa urefu wa kamba yake, na hivyo kuthibitisha wazi wazi kwamba Ikulu kuna tatizo la "principal slack" na "principal shirking."

Kwa ujumla Uongozi wa Marais hawa kutoka Visiwani unakuwa unasifika zaidi kwa "mission creep," jambo ambalo mara nyingi huonekana kutokana na tatizo linaloitwa "cogntive hazard."

Wamekuwa na tatizo na elimu shallow na ya kuunga unga, na kwa kweli hili ndilo chimbuko la madudu yote haya.

Lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba marais wanaotoka upande wa Zanzibar wanafanya kazi kama "double agents" kwa faida ya ulimwengu wa Kiarabu. Wanamega nchi na kuwagawia wajomba na wapwa wao wa huko Uarabuni kwa kutumia kisingizio cha foreign direct investment.

Halafu bado kuna watu wanaendela kuongelea habari ya Rais akitoka bara makamu atoke Zanzibar!

Bado wanaongelea fomu moja kwa ajili ya mgombea Urais kupitia CCM yenye watu makini kuliko huyu Rais wa sasa Samia.

Na hofu hii inao uzito mkubwa katika ulimwengu wa leo ambapo kuna wimbi kubwa la arab settler neo-colonialism.

Lakini Hakuna tishio kama hilo kutoka kwa wabantu kama vile Wangoni, Waha wala Wakurya.

So, we should not downplay those who are pointing a finger from this angle of state security management.

They are genuinely trying to remind our state security management organs about the claim that there is a clear, present and imminent danger of turning Tanzania into an Arab satellite state.

Pale Ngorongoro kuna jambo la aibu kubwa linatokea.

Halmashauri za vijiji vinne zimeungana kuishitaki serikali kuu.

Kesi imeanzia mahakama za chini hadi mahakama ya rufaa ya Afrika Mashariki.

Mahakama ya Rufaa inasema kuna kila dalili kwamba seriki kuu inakandamiza serikali za vijiji.

Badala ya kuukubali ukweli huu serikali kuu inaamua "kuhamisha Magoli" kwa kufuta vijiji, kata na tarafa ili kuzizuia mahakama kutekeleza kazi zake za utoaji haki.

Serikali ya kijiji ni corporate person, kama ilivyo serikali kuu.

Kila mperisona anao ukuu wa nafsi unaopaswa kuheshimiwa na waperisona baki. Lakini inashangaza kwamba Rais wetu na wasaidizi wake woooote wanaonekana kama hawana habari na ukakasi wa jambo hili.

Mpaka napata mashaka kuhusu elimu, weledi na umakini wa baadhi ya wakubwa hawa. Ni aibu tupu.

Tuendelee kukusanya ushahidi, na mwisho wa siku utaelewa a tu.

Lakini kwa sasa nashauri jambo moja muhimu: Tuboreshe vigezo vya kikatiba vya kuwapata viongozi wakuu wa nchi.

Hasa rais, makamu wa rais, waziri mkuu, jaji mkuu, mwanasheria mkuu na waziri wa katiba na sheria.

Nafasi hizi lazima zijazwe na watu walio tayari kuheshimu kanuni ya ukuu wa nafsi ya kila mtu, au tuseme kila mperisona, bila kujali kama ni mperisona asilia au mperisona shirika.

- Rais msiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana

- Makamu wa Rais msiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana

- Waziri Mkuu msiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana

- Jaji mkuu msiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana

- Mwanasheria mkuu msiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana.

- Waziri wa Sheria na katiba msiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana.

_ Viongozi wakuu wasiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana.

- Serikali ya wasiginaji wa ukuu wa nafsi ya kiutu hapana.

- Viongozi wakuu wasiginaji wa personal sovereignty hapana!

- Viongozi wakuu wasiginaji wa natural personal sovereignty hapana!

- Viongozi wakuu wasiginaji wa corporate personal sovereignty hapana!

1724507721010.png

Picha ya ndege iliyopigwa tarehe 30 Juni 2024 siku Makonda alipokutana na Mfalme wa UAE. Mashuhuda wanasema ndege hii ilibeba wanyama wa Tanzania na kuondoka nao.
 
Sisi vijana wa sasa wengi wetu tuna MIHEMKO....

Ndani yake kunaweza kupatika ubaguzi wa KIKABILA ,KANDA ,RANGI ama KIDINI.....

Mzalendo gani wa kuwa na tabia hizo ?!!

Mzalendo gani wa kutoa LAANA...kumlaani kiongozi wake bila ya kujua kuwa ukimlaani kiongozi anayeongoza eneo ulilopo basi UNALILAANI hilo eneo.....

Hoja hujibiwa kwa hoja na si vioja vya "Argumentum ad hominem"[emoji1787]

#Say No To Bigotry [emoji7]
#Say No To Racism[emoji7]

#Say No To Religious Hatred[emoji7]

A saying of the sages "never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeable".

TANZANIA KWANZA KABLA YA NAFSI YANGU [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
TANZANIA KWANZA KABLA YA NAFSI YANGU

mkuu umemaliza vizuri sana maana kuna watu wako tayari kushangilia wakisikia sgr yetu imezima kama sio watanzania!
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tanzania imewahi kukumbwa na kashfa kubwa tu zilizokuwa zinahusisha mali ya asili au mali ya umma (Hakuna mali ya serikali). Kashfa kubwa zaidi ambazo zilizizima katika taifa letu zilianza miaka mingi nyuma lakini hakuna ambayo iligusa akili na fikra za Watanzania kama ujio wa kashfa ya kuuzwa kwa eneo la mbuga ya Ngorongoro kwa wawindaji kutoka Dubai. Ngorongoro imekuwa ni mtego mkubwa kwa watawala wetu; mtego ambao ni jaribu ambalo hawawezi kulishinda. Hili nitakuja kulizungumzia baadaye inshallah.

Hayo yalifanyika wakati wa Mwinyi. Lakini baadaye yake akaja Mkapa na Kikwete. Hawa ni watu kutoka bara. Ukisikiliza watu wanavyozungumza leo utadhani kuwa wakati wa Mkapa na Kikwete hakukuwahi kutokea kashfa kubwa zilizohusisha mali za umma na mali asili. Na inawezekana tuna vijana wanaoingia mitandaoni siku hizi na kukuta kuna kashfa na wanadhani zimeanza leo. Niwakumbushe tu kashfa kadhaa nyingine:

  • Kashfa ya Sukari
  • Kashfa ya Meremeta
  • Kashfa ya Deep Green Finance
  • Kashfa ya Richmond
  • Kashfa ya Dowans
  • Kashfa ya EPA (escrow account) (humu kulikuwa na mambo ya Daud Balali - tushamsahau)
  • Kashfa ya CIS
  • Kashfa ya Kuuzwa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira
-Kashfa ya Ununuzi wa Rada
- Kashfa ya Ununuzi wa Airbus 320

Hizi ni chache tu; na zimetokea wakati wa "marais wa bara". Ufisadi ni ufisadi tu; haujalizi anayeufanya anatokea wapi. Tusimpinge au kupinga sera za Rais Samia sababu ya Uzanzibari wake. Hatukumpinga Mkapa sababu ya kabila lake au sehemu anayotoka; alijiuzia Kiwira!!! Kikwete hakupingwa sababu ya kuwa anatoka Msoga au mtu wa pwani! Kuna watu walimpinga Magufuli kwa sababu hawakukubaliana naye na of course hakuna aliyesema wanampinga kwa sababu ni Msukuma (sic) au kwa sababu anatoka Chato! Hakupingwa kwa sababu ya asili yake.

Ndugu zangu, kila Mzanzibari ni Mtanzania japo si kila Mtanzania ni Mzanzibari. Kila Mngoni (raia wa Tanzania) ni Mtanzania japo siyo kila Mtanzania ni Mngoni. Tukielewa hili tutaweza kujenga hoja za kupinga bila kuonekana ni wakabila mambo leo!
Umepatwa na nini siku hizi? Unawezaje kulinganisha wizi wa mali na uuzaji wa pande la nchi!
 
Usipoona uhusiano siwezi kukusaidia..hakuna mwizi anayeanza kwa kuiba vikubwa ambavyo ni rahisi kuonekana...
 
Epa na Escrow ni kashfa mbili tofauti
 
Sisi vijana wa sasa wengi wetu tuna MIHEMKO....

Ndani yake kunaweza kupatika ubaguzi wa KIKABILA ,KANDA ,RANGI ama KIDINI.....

Mzalendo gani wa kuwa na tabia hizo ?!!

Mzalendo gani wa kutoa LAANA...kumlaani kiongozi wake bila ya kujua kuwa ukimlaani kiongozi anayeongoza eneo ulilopo basi UNALILAANI hilo eneo.....

Hoja hujibiwa kwa hoja na si vioja vya "Argumentum ad hominem"[emoji1787]

#Say No To Bigotry [emoji7]
#Say No To Racism[emoji7]

#Say No To Religious Hatred[emoji7]

A saying of the sages "never give wisdom to unworthy as it unjust to the knowledgeable".

TANZANIA KWANZA KABLA YA NAFSI YANGU [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ni UDINI tu unawasumbua, hayo ya ukabila, ukanda na rangi wala hayawasumbui

Hawa jamaa ni udini tu, magufuli, mwenzao, alitimua watu mjini pale kimara ila kimyaaaaaa
Hakuna aliyemwambia aondoke
 
.

Ndugu zangu, kila Mzanzibari ni Mtanzania japo si kila Mtanzania ni Mzanzibar.
Kikatiba na Kisheria sawa, ila kwa utashi, utayari wenyewe hawataki…na siku zote hujitambulisha kama Wazanzibar na huishi na kutenda kama Wazanzibar ni vile tu utanzania una fursa nyingi wanabaki kuuvumilia tu, hawauishi, wanauvumilia
 
Mkuu kuwa muwazi, au kuna agenda unaificha!

Vilio vyote vya waTz kwa sasa umesikia kuna mtu anazitaja sababu kuwa zinasababishwa na Uzanzibari wa Rais?

Kwa hiyo ufisadi wa kina Mwinyi hadi Magufuli, kwako ndiyo shamba darasa unalotumia kuunga mkono ufisadi wa Serikali ya Rais Samia?

Katika waandishi wabobezi na ninao waheshimu sana katika Jf ni pamoja na wewe Mzee Mwanakijiji, imekuwaje leo, kuna nini kimekupata!

Nashindwa kujizuia kuamini mzee aliyekula chumvi nyingi namna hiyo leo kugeuka kuwa chawa!

Yawezekana bwana, dunia hii ni duara, lolote laweza kutokea na kwa muda wowote.

Maana mtu anaweza kubadili dini siku zake za mwisho akiwa hoi mahututi kitandani akipambania uhai na mauti, ama kutoa maagizo ya ujenzi wa nyumba yake wakati huo kaburi lake likichimbwa!
Labda hujasikia hoja za baadhi ya viongozi ambao wanasema "Mzanzibari Samia..."...
 
I second you...hakuna taifa lolote linalostawi bila ustawi wa watu wa taifa husika. Kuhamisha kwa nguvu watu wa taifa lako ili kupisha wageni wawekeze ni uzwazwa na yeyote anayrlitazama hili kwa jicho la husda basi ni mzandiki.
Mojawapo ya matatizo ambayo naamini bado yanatukabili ni hili la kuamini kuwa kuna watu nje ya Tanzania (Nyerere aliwaita wajomba zetu) ambao wanaweza kuja Tanzania na kututendea kwa vile wanatupenda saaana. Alianza Mkapa katika hili la kutukuza "wawekezaji"... tuliwaita "wafadhili" siku hizi nasikia wanaitwa "washirika wa maendeleo".
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tanzania imewahi kukumbwa na kashfa kubwa tu zilizokuwa zinahusisha mali ya asili au mali ya umma (Hakuna mali ya serikali). Kashfa kubwa zaidi ambazo zilizizima katika taifa letu zilianza miaka mingi nyuma lakini hakuna ambayo iligusa akili na fikra za Watanzania kama ujio wa kashfa ya kuuzwa kwa eneo la mbuga ya Ngorongoro kwa wawindaji kutoka Dubai. Ngorongoro imekuwa ni mtego mkubwa kwa watawala wetu; mtego ambao ni jaribu ambalo hawawezi kulishinda. Hili nitakuja kulizungumzia baadaye inshallah.

Hayo yalifanyika wakati wa Mwinyi. Lakini baadaye yake akaja Mkapa na Kikwete. Hawa ni watu kutoka bara. Ukisikiliza watu wanavyozungumza leo utadhani kuwa wakati wa Mkapa na Kikwete hakukuwahi kutokea kashfa kubwa zilizohusisha mali za umma na mali asili. Na inawezekana tuna vijana wanaoingia mitandaoni siku hizi na kukuta kuna kashfa na wanadhani zimeanza leo. Niwakumbushe tu kashfa kadhaa nyingine:

  • Kashfa ya Sukari
  • Kashfa ya Meremeta
  • Kashfa ya Deep Green Finance
  • Kashfa ya Richmond
  • Kashfa ya Dowans
  • Kashfa ya EPA (escrow account) (humu kulikuwa na mambo ya Daud Balali - tushamsahau)
  • Kashfa ya CIS
  • Kashfa ya Kuuzwa Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira
-Kashfa ya Ununuzi wa Rada
- Kashfa ya Ununuzi wa Airbus 320

Hizi ni chache tu; na zimetokea wakati wa "marais wa bara". Ufisadi ni ufisadi tu; haujalizi anayeufanya anatokea wapi. Tusimpinge au kupinga sera za Rais Samia sababu ya Uzanzibari wake. Hatukumpinga Mkapa sababu ya kabila lake au sehemu anayotoka; alijiuzia Kiwira!!! Kikwete hakupingwa sababu ya kuwa anatoka Msoga au mtu wa pwani! Kuna watu walimpinga Magufuli kwa sababu hawakukubaliana naye na of course hakuna aliyesema wanampinga kwa sababu ni Msukuma (sic) au kwa sababu anatoka Chato! Hakupingwa kwa sababu ya asili yake.

Ndugu zangu, kila Mzanzibari ni Mtanzania japo si kila Mtanzania ni Mzanzibari. Kila Mngoni (raia wa Tanzania) ni Mtanzania japo siyo kila Mtanzania ni Mngoni. Tukielewa hili tutaweza kujenga hoja za kupinga bila kuonekana ni wakabila mambo leo!
Kashfa ya Dp world
 
Back
Top Bottom