Swali muhimu kwa Jamila Mbaruku wa TRC kuhusu ukaguzi wa tiketi

Umenena vyema mkuu. Ni kuwe Gate scanner kila Station full stop, ila swali ni je Station za TRC zote zina uzio?
 
Jibu liko ndani ya mabano, mwanzoni nilimkosoa lakini baadae nikajiona mimi ndio mjinga na yeye yuko sawa.
Ahaa haaaah wewe ni mstaarabu sana. Keep it up mkuu. Grace and Glory shall speak for you.
 
Sawa, siwezi kukukatalia: Ukiendea Zanzibar Soko wanaliita Marikiti (Market in English) Bongo Soko tunaliita Soko inatokana na neno Kiarabu (Al Souk) tamka Alsuuk.
Ndugu zetu wa Zanzibar nao wakati wa koloni wao wa mwanzo ni Waarabu ambao soko waliliita Al souk Sasa iweje waliite Marikiti, (Market) lugha ya Mkoloni wa Kiingereza ambaye aikuja baadaye sana. Ina maana soko liliitwaje kabla ya influence ya Kiingereza kuja? Pamoja na hilo neno shule ambalo ni Kijerumani (schule) wao wakaja na neno skuli (School).
 
Sasa turudi kwenye mada natumai ubishi umeisha.
Kushindwa kwa watumishi wa shirika la reli(TRC) kunatuonesha kuwa uongozi ulijikita kupokea makundi na viongozi wa CCM na kuwasafirisha na kuwahudumia bure kwenda Morogoro na kurudi wasijue kuwa malikua wanatengeneza hasara kwenye biashara, neno moja linalowafaa ni kuwa hawafai kuliongoza shirika kwani mambo yaliyowashinda ni mambo ambayo tusio ndani ya shirika tuliyaona na kuyalalamikia na wao bado hawajayaona ila kwakua TAKUKURU imesema wamelazimika kukubali.
 
Naam, Wachina ndo wanafanya hivyo kwenye high speed train zao.

Kama umekata kituo cha mbele ukashuka kabla hamna tatizo, lqkini kama umekata kituo cha nyuma ukashuka mbele ukifika huko ticket inagoma kuscan ili utoke na unalipishwa kwa uhuni huo
Tena walipishwe nauli mara mbili yake kama adhabu siku nyingine wasirudie.
 
Ajira za vimemo,
Unaweza kuta mhudumu badala ya kukagua tiketi yuko anachati umbea wa shilole na asha buheti.
Tuwe wakweli jaman wahudumu wa ndani wanajitahidi kuhudumia. Mara chache nimewaona wakichat.
 
Zanzibar ni kweli kabisa ilitawaliwa na Mwarabu lakini pia ilikuwa Protectorate chini ya Mwingereza tangu mwaka 1890 kama sikosei. Hivyo Wazanzibar utakuta wameadopt lugha zote mbili kwa wakati mmoja mfano mzuri:
1. Soko la Darajani utakuta wenyeji wa Zanzibar wanaliita Marikiti (Market)
2. Soko la Mwanakwerekwe pamoja na masoko mengine yanayaita Soko (Al souk ambayo inatokana na Kiarabu)
Hivyo wanatumia lugha zote mbili kwa wakati mmoja (Soko na Marikiti).
 
Ni kawaida treni kuwa na TT(mkaguzi wa tikiti) na polisi ndani ya teni, treni ni sawa na kijiji hivyo wahalifu wamo na mahabusi pia imo.

..Polisi ni sawa kuwa nao.

..lakini mkaguzi wa tickets ni kuongeza gharama zisizo za lazima.
 
..Polisi ni sawa kuwa nao.

..lakini mkaguzi wa tickets ni kuongeza gharama zisizo za lazima.
Hao wawili hufanya kazi pamoja, TT akikukuta hauna tikiti anakukabidhi kwa polisi ambae anakupeleka mahabusu ya ndani ya treni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…