Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Nilikuona kwenye kituo kimoja cha runinga nchini ukisema eti TAKUKURU Imegundua uwepo wa abiria wanaokata tiketi ya shilingi elfu moja kwenda Luvu(Ruvu) lakini wanaitumia kwenda Morogoro!
Swali langu kwako, ndani ya treni wamo wafanyakazi wengi wa TRC wakiwemo mashosti, je, ni vipi shirika limeshindwa kuajiri wakaguzi wa tiketi?
Pili, vituo vya njiani huwa havipewi orodha ya abiria watakaoshuka kwenye vituo vyao ili nao wauze tiketi kulingana na abiria watakaoshuka hapo?
Inakuwaje TRC inauza tiketi nyingi za masafa mafupi ambazo abiria wake hawateremki mpaka TAKUKURU ije TRC ndani ya treni na kuwaambia eti abiria masafa mafupi hawateremki!
Ni wazi TRC imewaajiri viongozi na wafanyakazi wasio na ujuzi na uwezo wa kufikiri.
Nina uhakika yote yanayoendelea stesheni na ndani ya treni mnayajua na lazima yana maslahi kwenu, vinginevyo yasingekuwepo.