Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?

Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?

Hapa tuweni wakweli tu, waliolengwa kwenye huo mwavuli wa wahamiaji haramu ni wanyarwanda, tuacheni unafiki.
Kama hakulenga wanyarwanda, kwa nini azungumzie kwenye wahamiaji wengi wanyarwana asiende kuzungumzia mpaka wa Namanga?

Tarehe ya sherehe za kuwakumbuka Mashujaa wetu haikupangwa kufuatia shenanigans ya JK Vs PK........it is so happened kuwa iko hivyo and thats the reality.........Kama Rwandans waliona ni free kuingia na mifugo yao na kuona sisi ni mazuzu.......hatufanyi chochote........who knows.....pengine ndio maana idadi yao ni kubwa.......sisi Watanzania hatukupanga kukaribisha idadi fulani ya wahamiaji haramu........Gees!

Ndio maana JK alivilaumu sana sana vyombo husika vya kusimamia sheria na taratibu za nchi........

....Jamani eehh tumseme JK kwa mengine.......lakini kwa hili suala.....tumpe support zetu.....tena mimi binafsi bado naona amekuwa soft sana kwenye hili suala........hawa wahamiaji haramu wote ilibidi wawekwe Kuzuizini (detention) na mali zao kufilisiwa!........ukikamatwa leo nchi za watu wewe ni mhamiaji haramu....hawakurudishi nyumbani kwako ukachukue vitu vyako......wanakuweka kizuizini....huku unasubiri the next flight......kuna Watanzania wengi tu yamewakuta hayo majanga........acheni hizo

Soma magazeti ya leo. Wanyarwanda 520 wameshaondoka kurudi kwao. Soma Mwananchi. Usibishe hata kwa mambo yaliyo wazi kabisa.

.....Mkuu...hili ndio tatizo la magazeti yetu....pamoja na akzi nzuri waifanyayo....lakini wakti mwingine waandishi na Wahariri wana mapungufu.........angekuwa Mnyarwanda mmoja wangeandika?........regardless of their numbers...wahamiaji haramu wote warudi kwao........au wafuate taratibu na sheria za nchi yetu..........ili kuendelea kuishi nchini.........
 
Kama JK angeagiza tu wahalifu wakamatwe na kupewa adhabu wanayostahili kuna mtu yeyote ange criticise?Naona unajaribu kujitoa akili baada yakuishiwa hoja, unajaribu kukikimbia kile ulichokuwa unasimamia mwanzo.
Sasa mbona unajijibu mwenyewe. Umeelewa operation itakayofanyika?

Lengo la operation ni kuwakamata waarifu wote na kuwapa adhabu wanayostahili, wale watakaorusha risasi kwa askari wetu Rais kashasema "hawatachukuliwa mateka" na amesema wanajeshi wanaelewa maana ya kauli hiyo.

What else do you want? Rais amekula kiapo cha kuwalinda watanzania sio cha kulea wahamiaji haramu...
 
Maamuzi ya hekima na busara pekee hutoa majibu sahihi kwa matatizo mabalimbali.

Maamuzi ya kidikiteta, lazima na visasi hasa huishia katika utata, majanga na hata vita visivo na sababu wala lazima

Sikuwahi kusikia nyerere kawafukuza waganda kagera hata siku moja, nakama ilifanyika mwenyetaarifa sahihi aziweke hapa.

Hata pale Nyerere alipofanikiwa kuwatiamikononi wanajeshi na dege lao kutoka Libya, Nyerere aliwarejesha kwao kwa utaratibu maalum (kumbuka mateka wa kivita na waliletwa kwa lengo moja tu wale waarabu kutumaliza)

Nasikitika sana sana kwetu watanzania kushupalia kitendo hiki kiovu, kibaya na kinacholihalibia sifa nzuri taifa letu.

Hili ni tatizo:-

-kikwete anapoelekeza nguvu zake kwa kundi maalumu la watu maalu pekee.

-Kikwete anapochukuwa hatua bila maandalizi wala ushikishwaji bora wa wahusika

-Kikwete bila kuzingatia kwamba huko kwa majirani zetu, pia wapo watanzania wengi wanaioshi bila vibali kama hawa.

Nadhani Kiongozi wanchi yampasa kuruhusu hekima zaid kuchukuwa nafasi yake zaidi ya chochote.

Je unajua maana ya wahamiaji haramu?je unajua jinsi wanavyowanyanyasa wazawa kwa sababu ya ardhi yao?je unajua jinsi wanavyoteka na kupora mali wafanya biashara wazawa?ondoka nyuma ya bao bonye nenda kashuhudie mambo yanayotendeka usisikid kwenye vijiwe vya kahawa.
 
JokaKuu utaona sijatumia nano "wakimbizi". Rudia tena kusoma uone kama ni apples na oranges..
Mzee Mwanakijiji,

..kwani sheria za Tz zinasemaje kuhusu suala la "illegals"?

..mimi nadhani Mwalimu angefuata sheria za Tz jinsi ya ku-deal na "illegals."

..kwa mfano, hivi mlitegemea Mwalimu angecheka na mtu yeyote yule, raia ,au "illegals," ambaye ameingiza mifugo kwenye misitu ya hifadhi?

..je, Mwalimu angetoa siku 14 kwa majambazi, raia au "illegals," wasalimishe silaha zao? Jasusi atakumbuka jinsi Mwalimu alivyopeleka askari wa JWTZ kushughulikia wale wahuni waliojitangazia uhuru na jamhuri yao kule Mara.

..Kwa hiyo jibu langu ni kwamba Mwalimu angezingatia sheria za Tanzania. Hawa tunaoshughulika nao sasa hivi siyo wakimbizi, ni wahamiaji haramu.

..Kwa mtizamo wangu, tusimkatishe tamaa Raisi Kikwete. Badala yake tum-challenge ashughulike na wahamiaji haramu popote pale ktk Jamhuri yetu.
 
Last edited by a moderator:
We makalio upo? dini yako inakataza uzushi, vipi umeamua kumuasi Allah wako kwa njaa zako?
Hivi matusi yanakusaidia nini au ndio sera za chama chako? haya nionyeshe nimezusha wapi!

Na Allah kaingiaje tena huku?
 
Mkuu kuna tofauti kubwa kati ya "Mkimbizi" na "Mhamiaji Haramu (illegal immigrants)".......besides....wanaondoka si illegal immigrants wa kutoka Rwanda pekee (msi-take advantage ya uhasama wa JK na PK ili kukuza issue ambayo haipo).......Wahima, Wachiga and the likes wako Rwanda na Uganda pia, kuna Waganda, Wajaluo pia ambao ni wahamiaji haramu.......they will go out of our country as well......amri ya JK ni across the board.......

Umesikia popote wasomali, wachina au wahindi wakilalama kwa amri ya kikwete kama ilivyo kwa wanyarwanda?

you must be joking in this case.
 
Wewe sikia, ina maana hizo sherehe za mashujaa zimefanyika mwaka huu tu?, mbona hatuwahi kusikia ametoa maagizo hayo kwa wahamiaji haramu popote?, wewe unadhani matamshi yake hayo hayajachochewa na ugomvi wake na Kagame?, acha kujiongopea wakati ukweli unaujua.
Tarehe ya sherehe za kuwakumbuka Mashujaa wetu haikupangwa kufuatia shenanigans ya JK Vs PK........it is so happened kuwa iko hivyo and thats the reality.........Kama Rwandans waliona ni free kuingia na mifugo yao na kuona sisi ni mazuzu.......hatufanyi chochote........who knows.....pengine ndio maana idadi yao ni kubwa.......sisi Watanzania hatukupanga kukaribisha idadi fulani ya wahamiaji haramu........Gees!

Ndio maana JK alivilaumu sana sana vyombo husika vya kusimamia sheria na taratibu za nchi........

....Jamani eehh tumseme JK kwa mengine.......lakini kwa hili suala.....tumpe support zetu.....tena mimi binafsi bado naona amekuwa soft sana kwenye hili suala........hawa wahamiaji haramu wote ilibidi wawekwe Kuzuizini (detention) na mali zao kufilisiwa!........ukikamatwa leo nchi za watu wewe ni mhamiaji haramu....hawakurudishi nyumbani kwako ukachukue vitu vyako......wanakuweka kizuizini....huku unasubiri the next flight......kuna Watanzania wengi tu yamewakuta hayo majanga........acheni hizo

.....Mkuu...hili ndio tatizo la magazeti yetu....pamoja na akzi nzuri waifanyayo....lakini wakti mwingine waandishi na Wahariri wana mapungufu.........angekuwa Mnyarwanda mmoja wangeandika?........regardless of their numbers...wahamiaji haramu wote warudi kwao........au wafuate taratibu na sheria za nchi yetu..........ili kuendelea kuishi nchini.........
 
Kama kuwaondoa leo hii mrudi kwenu mnaleta pingamizi hivi, je itakuwaje mkiota mizizi kabisa ?????.
Si mtatushikia mitutu nyie !!!!!!!!!.
Hivyo vifungu vyoote ni kutaka kuhalarisha uhalamu wenu.
Hapa mnafanya kampeni chafu,
ajenda zenu zinajulikana.
 
Mzee Mwanakijiji,

..kwani sheria za Tz zinasemaje kuhusu suala la "illegals"?

..mimi nadhani Mwalimu angefuata sheria za Tz jinsi ya ku-deal na "illegals."

..kwa mfano, hivi mlitegemea Mwalimu angecheka na mtu yeyote yule, raia ,au "illegals," ambaye ameingiza mifugo kwenye misitu ya hifadhi?

..je, Mwalimu angetoa siku 14 kwa majambazi, raia au "illegals," wasalimishe silaha zao? Jasusi atakumbuka jinsi Mwalimu alivyopeleka askari wa JWTZ kushughulikia wale wahuni waliojitangazia uhuru na jamhuri yao kule Mara.

..Kwa hiyo jibu langu ni kwamba Mwalimu angezingatia sheria za Tanzania. Hawa tunaoshughulika nao sasa hivi siyo wakimbizi, ni wahamiaji haramu.

..Kwa mtizamo wangu, tusimkatishe tamaa Raisi Kikwete. Badala yake tum-challenge ashughulike na wahamiaji haramu popote pale ktk Jamhuri yetu.

Here we go now, kama hili lingefanyika kwa usawa walau ningepunguza sio kuondoa kabisa lawama zangu.

Lakini kikwete hajafanya hivyo amelenga wanyarwanda pekee kwanini? kwa vipi sheria hii isiwafurushe wasomali, wachina

na wahindi wahamiaji haramu?.........hapa napata kigugumizi kunajambo nyuma ya pazia ni lipi hilo!!!!
 
Umesikia popote wasomali, wachina au wahindi wakilalama kwa amri ya kikwete kama ilivyo kwa wanyarwanda?

you must be joking in this case.

Kulalama ni one thing.....kufuata maagizo ni another thing........kama wewe unawajua wahamiaji haramu ni wajibu wako kama Mtanzania kutoa taarifa.........hata mwizi akikamatwa hulalama.......who is joking here......

JK kawaonea huruma sana hawa wahamiaji haramu......ilitakiwa wote wakamatwe wawekwe kuzuizini......washitakiwe.....halafu warudishwe kwao....kwa utaratibu unaoeleweka......sijui kwa agizo la JK kuna utaratibu gani wa hao wahamiaji haramu kuondoka na kuhakikisha kuwa wameondoka.......
 
Tatizo la wahamiaji haramu ni la muda mrefu, mwaka 2000 nikienda Kagera ilibidi kusindikwa na polisi kwa msafara, wananchi wa huko kuishi kwa mashaka makubwa na ya ukatili.
Tuliambiwa ni kutokana na vitaBurundi na Rwanda.

Hatua zikachukuliwa kuleta usuluhishi kwa gharama na usalama wetu.
'Wahamiaji' 30,000 wakpewa uraia na wengine 160,000 wakafuatia ili waweze kuishi na kushiriki shughuli kama raia wengine. Kifungu cha 12(1) cha kuthamini utu na heshima yao kilitimizwa.

Tatizo siyo watu kuishi bali ni kwa jinsi gani watu hao wamefauta taratibu kama wale 190,000 walivyofanya. Hawa tunaowaongelea ni wahamiaji HARAMU.

Ninamlaumu sana rais kwa kutoa onyo waondoke. Hawakupaswa kupewa onyo walipaswa kushtakiwa kwasababu kama wahamiaji haram sheria ilipaswa ichukue mkondo wake.
Na kwa vile tunaamini wanapaswa kulindwa na sheria za nchi 13(3) basi walitakiwa wafikishwe mahakamani ili sheria hizo ziwalinde au ziwahukumu. Kutakiwa kuondoka nchini ni kuwapendelea.

Sijui watu hao walioingia kwa maelfu na kunyang'anya wakazi wa Kagera ardhi zao hadi kujimilikisha ardhi walifuata 12(1), 13(1) 13(3)? Sijui watu hao walioingia na silaha na kusababisha uvunjifu wa amani wanastahili 12(i). Wao hawakuheshimu sheria za nchi sasa tuanzie wapi kama si kuwakamata, hata kuwaondoa tu ni huruma kubwa

Moja kati ya malalamiko yetu siku ni serikali kutofauta sheria, sioni kwanini tuilamu serikali kwa kufuata sheria. Hata Sweden ambako uhuru, haki za kidinadamu n.k. zimetamalaki kuliko sisi wababishaji, wameondoa wasomali wasiofuata taratibu. Hawakufukuza wasomali wote bali walioshindwa kufuata tartibu.

Kwanini kuna selective justice?
Siku za nyuma Burundi na DRC nao walirudishwa.Lakini tuangalie zaidi ya hapo, watu 20,000 wanapovamia eneo moja kujitwalia ardhi, kufukuza wenyeji na kuingia na silaha ni tofauti na wahamiaji 3 kutoka Gambia.

Tunakumbuka 190,000 walopewa uraia walikataa kuhamia mikoa mingine wakitaka wabaki Kigoma na Kagera. Kiusalama hili ni jambo jema?
Je, tuwape uhuru, haki na ubinadamu wakati watu wetu wakikosa haki hizo katika nchi yao?

Je, hatujajifunza tatizo la DRC limeanzaje na je tuendelee ku-entertain hatari hata pale tunapoona kuna ulazima wa kufanya wa kuchukua hatua?
Hakuna haki isiyo na wajibu,je, wao walitimiza wajibu wao wakati wanakuja nchi ya watu?

Kwanini Collective punishment?
Unapokuwa na wananchi kutoka nchi jirani 20,000 na kiongozi wao akitishia 'hit' etc, sidhani ni muafaka kuamini kuwa hawezi kutumia kundi hilo kubwa kuvuruga zaidi usalama.

Ni rahisi kwa PK kuwapa silaha waanzishe uasi Kagera kama alivyofanya DRC ili tuwe busy kwa faida yake. Siwezi kusema hii ni collective punishment niseme ni consequences za kauli za PK ambazo zinatishia usalama wetu na njia rahisi ni kuchukua tahadhari.

Nyerere alifanyaje huko nyuma? Nadhani JokaKuu amelieza.
Burundi na Rwanda kwa pamoja walishawahi kueleza tatizo la usalama linatokana na waasi waliokimbilia Tanzania. Nadhani Tanzania iliamu kuwapa urai 190,000 ili iweze kukabiliana nao kisheria na kuleta usalama katika nchi hizo. Je, ni muafaka tuwaache bila kujua ni raia wetu halafu waanzishe mapambano dhidi ya serikali zao na tuwaunge mkono kama tulivyofanya kwa Uganda?

Je, hili ni nje ya EAC spirit?
Wanaosema hili wamepotoka. Hadi sasa hatuna mkataba wa pamoja kuhusu uhamiaji.
Upo mkataba wa Kenya, Uganda na Rwanda na nadhani ni muafaka PK awapeleke huko.

Hata kama tutakuwa nao, ni wajibu wa serikali yoyote dunia kujua akina nani wapo katika nchi na haki zao ni zipi. Hatuwezi kuwa na EAC spirit katika njia za kijinga.
mkuu heshima sana kwa kujaribu kujibu hoja lakini kuna swali muhimu umeskip!
Hivi Nyerere alikabiliana vipi na swala hili hili wakati wa 'chokochoko' za Iddi Amini dada?
Je hii ndio njia muafaka ya kukabiliana na wahamaji haramu hasa kutoka rwanda baada ya matusi ya kagame?
 
Kulalama ni one thing.....kufuata maagizo ni another thing........kama wewe unawajua wahamiaji haramu ni wajibu wako kama Mtanzania kutoa taarifa.........hata mwizi akikamatwa hulalama.......who is joking here......

JK kawaonea huruma sana hawa wahamiaji haramu......ilitakiwa wote wakamatwe wawekwe kuzuizini......washitakiwe.....halafu warudishwe kwao....kwa utaratibu unaoeleweka......sijui kwa agizo la JK kuna utaratibu gani wa hao wahamiaji haramu kuondoka na kuhakikisha kuwa wameondoka.......

Mfano mmoja unatosha, fika kariakoo kisha angalia wachina wanafanya nini na sheria zetu za uwekezaji zinasemaje kisha

tafuta majibu kama kikwete na uhamiaji wapo au la. Ukishindwa kuliona hilo hata juwa kali la saa sita mchana huwezi

kuliona aslani
 
Back
Top Bottom