Swali Rahisi: Nyerere aliwashughulikiaje Waganda "Illegals" wakati wa "chokochoko" Za Idi Amin?

Hapa tuweni wakweli tu, waliolengwa kwenye huo mwavuli wa wahamiaji haramu ni wanyarwanda, tuacheni unafiki.
Kama hakulenga wanyarwanda, kwa nini azungumzie kwenye wahamiaji wengi wanyarwana asiende kuzungumzia mpaka wa Namanga?

Tarehe ya sherehe za kuwakumbuka Mashujaa wetu haikupangwa kufuatia shenanigans ya JK Vs PK........it is so happened kuwa iko hivyo and thats the reality.........Kama Rwandans waliona ni free kuingia na mifugo yao na kuona sisi ni mazuzu.......hatufanyi chochote........who knows.....pengine ndio maana idadi yao ni kubwa.......sisi Watanzania hatukupanga kukaribisha idadi fulani ya wahamiaji haramu........Gees!

Ndio maana JK alivilaumu sana sana vyombo husika vya kusimamia sheria na taratibu za nchi........

....Jamani eehh tumseme JK kwa mengine.......lakini kwa hili suala.....tumpe support zetu.....tena mimi binafsi bado naona amekuwa soft sana kwenye hili suala........hawa wahamiaji haramu wote ilibidi wawekwe Kuzuizini (detention) na mali zao kufilisiwa!........ukikamatwa leo nchi za watu wewe ni mhamiaji haramu....hawakurudishi nyumbani kwako ukachukue vitu vyako......wanakuweka kizuizini....huku unasubiri the next flight......kuna Watanzania wengi tu yamewakuta hayo majanga........acheni hizo

Soma magazeti ya leo. Wanyarwanda 520 wameshaondoka kurudi kwao. Soma Mwananchi. Usibishe hata kwa mambo yaliyo wazi kabisa.

.....Mkuu...hili ndio tatizo la magazeti yetu....pamoja na akzi nzuri waifanyayo....lakini wakti mwingine waandishi na Wahariri wana mapungufu.........angekuwa Mnyarwanda mmoja wangeandika?........regardless of their numbers...wahamiaji haramu wote warudi kwao........au wafuate taratibu na sheria za nchi yetu..........ili kuendelea kuishi nchini.........
 
Kama JK angeagiza tu wahalifu wakamatwe na kupewa adhabu wanayostahili kuna mtu yeyote ange criticise?Naona unajaribu kujitoa akili baada yakuishiwa hoja, unajaribu kukikimbia kile ulichokuwa unasimamia mwanzo.
 

Je unajua maana ya wahamiaji haramu?je unajua jinsi wanavyowanyanyasa wazawa kwa sababu ya ardhi yao?je unajua jinsi wanavyoteka na kupora mali wafanya biashara wazawa?ondoka nyuma ya bao bonye nenda kashuhudie mambo yanayotendeka usisikid kwenye vijiwe vya kahawa.
 
JokaKuu utaona sijatumia nano "wakimbizi". Rudia tena kusoma uone kama ni apples na oranges..
Mzee Mwanakijiji,

..kwani sheria za Tz zinasemaje kuhusu suala la "illegals"?

..mimi nadhani Mwalimu angefuata sheria za Tz jinsi ya ku-deal na "illegals."

..kwa mfano, hivi mlitegemea Mwalimu angecheka na mtu yeyote yule, raia ,au "illegals," ambaye ameingiza mifugo kwenye misitu ya hifadhi?

..je, Mwalimu angetoa siku 14 kwa majambazi, raia au "illegals," wasalimishe silaha zao? Jasusi atakumbuka jinsi Mwalimu alivyopeleka askari wa JWTZ kushughulikia wale wahuni waliojitangazia uhuru na jamhuri yao kule Mara.

..Kwa hiyo jibu langu ni kwamba Mwalimu angezingatia sheria za Tanzania. Hawa tunaoshughulika nao sasa hivi siyo wakimbizi, ni wahamiaji haramu.

..Kwa mtizamo wangu, tusimkatishe tamaa Raisi Kikwete. Badala yake tum-challenge ashughulike na wahamiaji haramu popote pale ktk Jamhuri yetu.
 
Last edited by a moderator:
We makalio upo? dini yako inakataza uzushi, vipi umeamua kumuasi Allah wako kwa njaa zako?
Hivi matusi yanakusaidia nini au ndio sera za chama chako? haya nionyeshe nimezusha wapi!

Na Allah kaingiaje tena huku?
 

Umesikia popote wasomali, wachina au wahindi wakilalama kwa amri ya kikwete kama ilivyo kwa wanyarwanda?

you must be joking in this case.
 
Wewe sikia, ina maana hizo sherehe za mashujaa zimefanyika mwaka huu tu?, mbona hatuwahi kusikia ametoa maagizo hayo kwa wahamiaji haramu popote?, wewe unadhani matamshi yake hayo hayajachochewa na ugomvi wake na Kagame?, acha kujiongopea wakati ukweli unaujua.
 
Kama kuwaondoa leo hii mrudi kwenu mnaleta pingamizi hivi, je itakuwaje mkiota mizizi kabisa ?????.
Si mtatushikia mitutu nyie !!!!!!!!!.
Hivyo vifungu vyoote ni kutaka kuhalarisha uhalamu wenu.
Hapa mnafanya kampeni chafu,
ajenda zenu zinajulikana.
 

Here we go now, kama hili lingefanyika kwa usawa walau ningepunguza sio kuondoa kabisa lawama zangu.

Lakini kikwete hajafanya hivyo amelenga wanyarwanda pekee kwanini? kwa vipi sheria hii isiwafurushe wasomali, wachina

na wahindi wahamiaji haramu?.........hapa napata kigugumizi kunajambo nyuma ya pazia ni lipi hilo!!!!
 
Umesikia popote wasomali, wachina au wahindi wakilalama kwa amri ya kikwete kama ilivyo kwa wanyarwanda?

you must be joking in this case.

Kulalama ni one thing.....kufuata maagizo ni another thing........kama wewe unawajua wahamiaji haramu ni wajibu wako kama Mtanzania kutoa taarifa.........hata mwizi akikamatwa hulalama.......who is joking here......

JK kawaonea huruma sana hawa wahamiaji haramu......ilitakiwa wote wakamatwe wawekwe kuzuizini......washitakiwe.....halafu warudishwe kwao....kwa utaratibu unaoeleweka......sijui kwa agizo la JK kuna utaratibu gani wa hao wahamiaji haramu kuondoka na kuhakikisha kuwa wameondoka.......
 
mkuu heshima sana kwa kujaribu kujibu hoja lakini kuna swali muhimu umeskip!
Hivi Nyerere alikabiliana vipi na swala hili hili wakati wa 'chokochoko' za Iddi Amini dada?
Je hii ndio njia muafaka ya kukabiliana na wahamaji haramu hasa kutoka rwanda baada ya matusi ya kagame?
 


Mfano mmoja unatosha, fika kariakoo kisha angalia wachina wanafanya nini na sheria zetu za uwekezaji zinasemaje kisha

tafuta majibu kama kikwete na uhamiaji wapo au la. Ukishindwa kuliona hilo hata juwa kali la saa sita mchana huwezi

kuliona aslani
 
Umesikia popote wasomali, wachina au wahindi wakilalama kwa amri ya kikwete kama ilivyo kwa wanyarwanda?


Ndiyo nimeishasikia Wasomali wanalalamika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…