SWALI: Wanaume mpewe nini muache kuchepuka?



Inawezekana wanaume wanaochepuka ni wengi kuliko wanawake na moja ya sababu ni kwamba Mwanaume ndiye anayetongoza ingawa sio mara zote. Upande wa pili ni huyo mchepukaji (mwanaume) anachepuka na nani? wakati fulani utakuta anachepuka na mke wa mtu ambaye naye, kwa muktadha huu ni mchepukaji.

Kimsingi kuchepuka ni tabia ya mtu, awe mwanaume au mwanamke. Ndiyo maana kukawa na 'serengeti boys' ama wale vijana wanaolelewa ... wakati mwingine 'walezi' wao ni wake za watu. kadhalika kuna wasichana wanaotembea na waume za watu na hapa wanaume ndo wenye makosa.

Wakati mwingine ugomvi kidogo ndani ya nyumba wengine wanachukulia kama ndo ticket ya kuchepuka ili akapate faraja elsewhere (both mwanaume na mwanamke). Maofisini/sehemu ya kazi wakati mwingine imekuwa ndo meeting point kwa sababu huko kuna watu wanaojali wake/waume za watu kuliko wenzi wao halisi... kuingia kwenye mtego wa kuchepuka inakuwa ni rahisi.

Pesa sio kigezo kwa sababu kuna watu wanacheat (mme na mke kila mtu na ndoa yake) bila kuwa na financial gain kwa upande wowote.

Back to your question...inawezekana hakuna kitu utackachompa mtu mwenye hulka ya kuchepuka akaacha kuchepuka ila MUOMBEE KWA Mwenyezi Mungu ili ambadilishe na kubaki kwenye njia kuu!
 
Mama wewe timiza wajibu wako tu ila huwezi kuzuia hawa viumbe kuchepuka maana wao wanapenda kwa kuona hivyo akiona tofauti na alicho nacho ataingiwa na tamaa ya kuchepuka tu. Na ukiona Mwanaume hachepuki ujue hana hela
hahahahaha,
 
Inaonekana ulikua vizuri sana kwenye essay mkuu
 
Kuchepuka ni kama kubadilisha mboga tu.ingawa sometimes unakutana na matembele poli yamepoza kuliko uliyoaacha home.ijapokuwa hotpot lilikuwa linavutia.ila ukianza kula baada ya kumeza tonge la kwanza unatamani hata mikono ukanawie home
ahhahahahah
 
Hii ni maneno ya mtu aliyekomaa kwenye ndoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…