SWAT, FBI na CIA nini tofauti ya hizi taasisi?

Tanzania ilipoanzisha la wasiojulikana mkalipiga vita badala ya kuona mapungufu yao yakaboreshwa kwa faida ya nchi.
Inaelekea wewe hauelewi unataka kulinganisha kulinganisha Marekani na bongo kwenye ujasusi........jaribu kufuatilia NSA wanavyodukuaga mawasiliano ya maraisi hata ambao ni mataifa washirika wao
 
Mbona jamaa mbishi sana wakati inajulikana wazi NSA kazi yao kubwa wanadeal na signal intelligence na kwamba CIA hawafanyi kazi ndani ya marekani ni kukariri.
Nikupe tu mfano CIA siyo law enforcement agency kwamba kazi yao kubwa ni kukusanya taarifa nia kuzituma kwa policy maker wa marekani lakn nikuulize tu siku wakikuhisi unahatarisha maslahi ya marekani hawatokushughulikia kwa sababu kazi yao ni kukusanya taarifa tu.
Halafu inabidi uelewe FBI ni security service na CIA ni intelligence service.
Lakini NSA hapo hapo ni Security service na ni intelligence service Kama unabisha endelea kubisha tu.
Unabisha bila kuwa na uhakika wa unalotetea kwa sababu unachanganya maneno mengi bila kuwa na coherent argument yoyote inayoeleweka. Ninapokuambia kuwa jambo lolote lililomo ndani ya mipaka ya marekani ambalo CIA inaweza kuwa na interest nalo linakuwa tayari ni crime na hivyo litashughulikiwa na FBI, halafu unasistiza kuwa CIA wakihisi unahatarisha maslahi ya marekani eti "watakushugulikia" ni kutokuelewa unachotetea. CIA hawawezi kukuhisi unahatarisha maslahi ya Marekani ukiwa ndani ya mipaka kwa sababu mbili, (a) hawana jurisdiction hiyo, (b) hawana asset za kukufuatilia ndani ya mipaka hadi kufikia kuhisi kuwa unahatarisha maslahi. Kazi hiyo itafanywa na FBI. Kule nyuma nilipotoa mfano kuwa FBI ni sawa na CID ya kwetu ila FBI inachunguza (wazi wazi) crimes zilizokwishafanyika kama CID, lakini vile vile inafanya (kwa siri) jitihada za kuzuia crimes zisifanyike ni wazi kunielewa ndiyo maana unarudia kuwa FBI ni intelligence na security service. Kwenye vetting vetting process kabla appointement ya mtu yeyote kwenye serikali ya marekani, nini lazima FBI ifanye background check. Hiyo background check ni semehu ya jitihada za kuzia crimes zisifanyike; mimi nimsheakumbana nao mara kadhaa sana wanapokuwa wanafanya background check kwa watu waliowahi kuwa wanafunzi wangu. Anafika anakuonyesha beji yake kuwa mimi ni ajenti wa FBI, ila sikuja hapa kukuchunguza wewe, naomba unisadie.

Unapotenganisha Security na intelligence ndipo unapokosea zaidi kwani unashindwa kutambua kuwa intelligence ni element mojawapo ya security kiasi hata FBI wana kitengo chao intelligence kinachofanya kazi ndani ya mipaka; usichukulie security kama vile walinzi wa mageti body guards.

Nilipoandika kuwa post hiyo imechanganya matumizi ya maneno Upelezi na ujasusi na kusahihisha kuwa FBI ni la upelelezi wakati CIA ni la ujasusi pia huenda hukunielewa. Hadi wakati huu tunapobishana hapa, elewa kuwa kazi za CIA ni tatu tu: (a) kukusanya (kwa siri) habari zinazohusiana na usalama na maslahi ya marekani kwa jumla nje ya mipaka, (b) kufanya ushawishi wa wazi wa kubadili mawazo ya watu nje ya marekani ili kuimarisha usalama na maslahi ya marekani, na (c)kufanya sabotage (kwa siri) kuharibu mambo yanayoweza kuhatarisha usalama na maslahi ya marekani nje ya nchi.

FBI kazi zao ni mbili kama nilivyokwishataja hapo juu. NSA wao kazi zao ni mbili pia (a) kukusanya habari (kwa siri) na zinazohusu usalama na maslahi ya marekani kutoka ndani na nje ya mipaka (b) kuzuia majaribio yoyote ya kuhatarisha usalama na maslahi ya marekani ndani na nje ya mipaka.

Wakati CIA na FBI kimsingi zinashughulika na mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu wa kawaida, NSA inashughulika na organizations kama mashirika, makampuni pamoja na serikali za nje. Kwa vile CIA haifanyi kazi ndani ya mipaka na FBI haifanyi kazi nje ya mipaka, basi NSA ndiyo ina jukumu la kushughulika na mtandano wa vikundi vya watu walioko ndani ya nchi wakishirikiana na walio nje ya mipaka. Scandal ya Snowden ilikuwa kwenye kitengo hiki kinachofuatilia mitandao ya watu walioko ndani wakishirikiana na walioko na nje ya mipaka.

Mojawapo ya maagizo ya sheria ya usalama iliyounda idara ya homeland security ni kuzitaka FBI, NSA na CIA kuwa zinabadilishana habari.
 
Wewe uelewa wako ni mdogo na nasema hivyo kwa sababu haujanielewa nliandika nn.
Kwani nikuulize hao FBI hawana intelligence analysts au hapo vipi. Kwa hiyo kwa sababu wana maintelligence analysts Basi tubadilishe maana ya kwamba ile ni intelligence service.
Kingine wewe unataka kuleta ligi tu nani amekwambia FBI hawafanyi kazi overseas.
Yaani ufananishe FBI na CID hapo ndo umenichekesha kwa kweli yaani hii ndo inapima wasomi Kama wewe uwezo wao kifikiria na kung'amua Mambo duh.
Halafu kingine uwe unaelewa kwanza kabla ya kujibu.....mm nlimaanisha wakikuhisi ni threat kwa taifa lao ndo watakushughulikia Sasa hapo kwenye kuelewa wewe huyo mhusika atakuwa wapi waliyemhisi is up to you.
Kutokana CIA wanavyofanya kazi nahisi unajua.Kama haujaelewa basi sio ligi hii kwamba tunashindania mbuzi au nn sijui!!!
 
FBI siyo shirika la ujasusi bali ni ofisi inayoshughulika na upelelezi wa makosa ya jinai ndani ya Marekani; ni kama CID hauku kwetu. Wako mbele kidogo zaid ya CID, kwani wanafanya upelelezi wa makosa yaliyokwisha fanyika, na vile vile kufanya upepelezi wa kuzia makosa yasifanyike. Huwa hawafanyi hujasusi bale wanapeleleza na kukusanya ushahidi pamoja na mashahidi. Ushahdi wanaokusanya lazimaa uwe sahaihi kwa sababu baadaye utapimwa na mahakama.
FBI inafanya law enforcement na domestic intelligence agency. CIA hawaruhusiwi kisheria kufanya ujasusi ndani ya Marekani, hiyo ni kazi ya FBI.

1650314123515.png
 
Wewe uelewa wako ni mdogo na nasema hivyo kwa sababu haujanielewa nliandika nn.
Kwani nikuulize hao FBI hawana intelligence analysts au hapo vipi. Kwa hiyo kwa sababu wana maintelligence analysts Basi tubadilishe maana ya kwamba ile ni intelligence service.
Kingine wewe unataka kuleta ligi tu nani amekwambia FBI hawafanyi kazi overseas.
Yaani ufananishe FBI na CID hapo ndo umenichekesha kwa kweli yaani hii ndo inapima wasomi Kama wewe uwezo wao kifikiria na kung'amua Mambo duh.
Halafu kingine uwe unaelewa kwanza kabla ya kujibu.....mm nlimaanisha wakikuhisi ni threat kwa taifa lao ndo watakushughulikia Sasa hapo kwenye kuelewa wewe huyo mhusika atakuwa wapi waliyemhisi is up to you.
Kutokana CIA wanavyofanya kazi nahisi unajua.Kama haujaelewa basi sio ligi hii kwamba tunashindania mbuzi au nn sijui!!!
Mbona hili jambo ni jepesi...

FBI ni domestic intelligence service + law enforcement agency.
CIA ni foreign intelligence service.

Kabla ya Sep 11, mipaka yao ilikuwa mikali sana. Kuna baadhi ya wale hijackers walikuwa kwenye radar za CIA, lakini walipoingia tu Marekani, CIA ikaacha kuwafuatilia kama sheria ilivyowataka, na mbaya zaidi hawakuwaambia FBI kwamba kuna watu wabaya wameingia. Wenyewe walikuwa wanaita FBI vs CIA Turf War. Baada ya Sep 11 moja kati ya recommendation ilikuwa kuunda ofisi ya Director of National Intelligence ili kuondoa huo utopolo.

Ila strictly speaking, CIA hawawezi kufuatilia mtu ndani ya Marekani, hata iwe vipi; na FBI wakitoka nje ya Marekani ujue kuna jambo kama jinai, mfano; ubalozi kupigwa bomu, lakini hawawezi kufuatilia mtu nje ya Marekani.

I stand to be corrected.
 
CIA wanafanya kazi ndani ya Amerika sema kazi zao ni limited. Mfano TV Show Carrie Mathison vs Nicholas Brody (Homeland)
Wachana na hizo show zitakupoteza

Huu ni ukurasa Rasmi wa FBI wanaelezea tofauti zao na CIA

1650314872384.png
 
Wachana na hizo show zitakupoteza

Huu ni ukurasa Rasmi wa FBI wanaelezea tofauti zao na CIA

View attachment 2192409
Mm nimekutolea mfano tu ili kuleta maana Kama unabisha Basi......
Kwani unahisi hizo official websites hatuzijui tunazijua. Ila mm kwenye suala la kuniambia CIA hawafanyi kazi ndani ya Marekani naona Kama unaniongopea tu.
 
Wachana na hizo show zitakupoteza

Huu ni ukurasa Rasmi wa FBI wanaelezea tofauti zao na CIA

View attachment 2192409
Ntaongepewa vitu vingine lakini sio ishu za maintelligence.......sijui kuhusu TISS sijui nn mtu hawezi kiniongopea hata siku moja nikakubali kirahisi
 
Unaongopewa na nani? Unapewa facts, jibu kwa facts sio series au labda unadhani kuwa na ofisi US ndio maana yake wanafanya kazi ndani ya US? Labda tuseme, hawaruhusiwi ku-target watu walioko ndani ya Marekani. Kama una hata operation moja ya CIA ndani ya USA, weka hapa

CIA kwa Marekani ni kama ilivyo Mi6 ya UK, nao hawaruhusiwi kufanya kazi za ndani. FBI kwa Marekani ni kama ilivyo Mi5 kwa UK hawaruhusiwi kufanya kazi za nje. Ndio maana ya Foreign na Domestic Intelligence service.
 
Wewe wakunipa fact mm Sasa mbona fact zako hazina logic.......unaniambia habari za Secret Intelligence Service au unahisi hatujui.....
 
Unaongopewa na nani? Unapewa facts, jibu kwa facts sio series au labda unadhani kuwa na ofisi US ndio maana yake wanafanya kazi ndani ya US? Labda tuseme, hawaruhusiwi ku-target watu walioko ndani ya Marekani. Kama una hata operation moja ya CIA ndani ya USA, weka hapa

CIA kwa Marekani ni kama ilivyo Mi6 ya UK, nao hawaruhusiwi kufanya kazi za ndani. FBI kwa Marekani ni kama ilivyo Mi5 kwa UK hawaruhusiwi kufanya kazi za nje. Ndio maana ya Foreign na Domestic Intelligence service.
Kwanza Kama unaelewa maana ya logic usingeropoka.....ungekuwa unajua usingebisha mfano wa series au unataka kushindana
 
Kama Wewe ni mfuatiliaji wa Mambo Mbali mbali, Bila shaka Lazima umewahi Kukutanana Na Majina Kama SWAT, CIA au FBI Wakati Tukipiga Stori za Uongo na Ukweli vijiweni.
Sasa Leo Nataka Uzijue Kiundani Taasisi hizi.

1. SWAT.
Ni Kifupi Cha Special Weapons and Tactics.
Na ilianzishwa Rasmi Mwaka 1964 (Hii ni Kwa Marekani lakini)
SWAT ni kikundi Maalum cha polisi kwa ajili ya kupamba na Matukio yanayohitaji Kutumia Silaha au Mbinu Maalum
Kwa mfano; matukio ya Utekaji na ujambazi, https://t.co/Qcu5ZZ8wUT

2. CIA
Ni Kifupi Cha “Central Intelligence Agency”.
Hili ni shirika la upelelezi la serikali ya Marekani, inayohusika na kukusanya, usindikaji, na kuchambua habari za usalama wa kitaifa kutoka duniani kote. https://t.co/utdhNVpbT3
Liliundwa rasmi September 18, 1947. makao Yake Makuu Yako Pale Langley, Virginia.
Limejikita zaidi Katika Msauala Ya Kijasusi Ya USA Kwa Ndani Na Nje ya USA.
Kwa Mujibu wa Vyanzo mbalimbali, CIA inatajwa Kama Shirika Bora La Kijasusi duniani Huku “Mossad”La Israel Likifuata. https://t.co/UZE3be22VR

3. F.B.I (Federal Bureau of Investigation).
Shirika la Ujasusi la Shirikisho la Marekani.
Ilianzishwa July 26 1908,Inakadiliwa Kuwa na Wafanyakazi Takribani 35,000 na Bajeti yake kwa mwaka ni
US$9,748,829,000. https://t.co/azEvACoF0e
FBI NA CIA yote ni Kama Mashirika Ya Kujasusi, lakini Tofauti Iliyopo Ni Kwamba,
FBI imejikita katika masuala ya kipelelezi yanayoihusu Marekani Kama Taifa lakini (Domestically) ila CIA ipo Ki Dunia Zaidi.
FBI inafanya kazi chini Ya Idara Ya Masuala Ya Haki Ya Marekani .

Muongo...
FBI hawahusiki na suala lolote la Ujasusi bali wao wamejikita zaidi kwenye upepelezi yaani investigation.

Kubwa ziima
 
CIA wanafanya kazi ndani ya Amerika sema kazi zao ni limited. Mfano TV Show Carrie Mathison vs Nicholas Brody (Homeland)
Hiyo show siyo ya CIA na wala hiyo siyo kazi ya CIA bali ni uigizaji tu. Holywood huigiza kitu chochote; ukitaka movie na show za TV zinazohisha CIA zipo nyingi sana; zote hazina baraka za CIA.
 
Wewe uelewa wako ni mdogo na nasema hivyo kwa sababu haujanielewa nliandika nn.
Kwani nikuulize hao FBI hawana intelligence analysts au hapo vipi. Kwa hiyo kwa sababu wana maintelligence analysts Basi tubadilishe maana ya kwamba ile ni intelligence service.
Kingine wewe unataka kuleta ligi tu nani amekwambia FBI hawafanyi kazi overseas.
Yaani ufananishe FBI na CID hapo ndo umenichekesha kwa kweli yaani hii ndo inapima wasomi Kama wewe uwezo wao kifikiria na kung'amua Mambo duh.
Halafu kingine uwe unaelewa kwanza kabla ya kujibu.....mm nlimaanisha wakikuhisi ni threat kwa taifa lao ndo watakushughulikia Sasa hapo kwenye kuelewa wewe huyo mhusika atakuwa wapi waliyemhisi is up to you.
Kutokana CIA wanavyofanya kazi nahisi unajua.Kama haujaelewa basi sio ligi hii kwamba tunashindania mbuzi au nn sijui!!!
Post yote hii haina mantiki kwani nilikwambia kuwa FBI wana wana kitengo chao cha intelligence kinachowasaidia kuzia uharifu kabla haijatendeka, halafu unaniuliza tena iwapo FBI hawana intelligence analysts? Swali gani hilo au unataka jibu la namna gani.

FBI hawana jurisdication kufanya kazi nje ya nchi bali wanaweza kufanya kwa kuombwa kuzisaidia mamlaka zenye jurisdiction kunakohusika. Nadhani hata sisi Tanzania tuliwahi kuwaomba kutusaidia kuchunguza mauaji ya padri mmoja huko Zanzibar. Wakienda kufanya uchunguzi wao nje ya nchi kwa ajili ya Marekani basi huwa ni kwenye balozi zao tu, kama walivyokuja kufanya uchunguzi hapa kwetu wakati ubalozi wao ulipolipuliwa.

Marekani hawawezi kukuchukulia hatua yoyote kwa kukuhisi tu; halafu nikakwambia kuwa CIA hawana resources za kukufuatilia ndani ya nchi hadi wafikie kukuhisi. Hiyo ni kazi ya FBI.

Nadhani aliyeanzisha uzi alikuwa na nia ya kufahamisha watu wengine hapa kwenye jukwaa, usijaribu kueneza habari za kupotosha watu kwa kuandika usiyofahamau na kulazimisha yakubalie kuwa ni kweli.
 
Back
Top Bottom