Prof_Adventure_guide
JF-Expert Member
- Dec 21, 2023
- 533
- 1,499
Hebu tuangalie ukweli uliopo mitaani bila kuogopa mtu. Taifa letu limefika mahali ambapo viongozi wetu wamegeuza nchi kuwa shamba la bibi, wanajiamulia mambo yao wanavyotaka wao na hawana habari kabisa na maisha magumu ya wananchi wa chini. Watu wanakufa na njaa, vijana wanazunguka mtaani hawana mbele wala nyuma, lakini wao wako bize na dili zao na misafiri isiyo na maana. Hii ni pure bullshit!
Inauma sana kuona nchi inaendeshwa kwa matakwa ya mtu binafsi badala ya kufuata katiba, sheria na kanuni zilizowekwa. Watu kama Tundu Lissu wamekuwa wakipiga kelele mchana na usiku kuonyesha huu uozo, lakini viongozi wa CCM wanawageuzia kibao na kuendelea na mambo yao ya kifedhuni bila huruma yoyote ile. Hawawezi kusikia kilio cha mwananchi wa kawaida kwa sababu wamelewa madaraka na wanaishi kwenye dunia yao ya kifahari.
Huu ni muda wa kusimama kidete na kuwakumbusha kuwa nchi hii sio mali yao ya urithi. Wananchi wamechoka na hii fake governance na mifumo yao ya kibabe inayowaminya wanyonge. Inatosha sasa, taifa linahitaji mabadiliko ya kweli na sio hawa viongozi wa aina hii ambao kazi yao ni kuangalia matumbo yao tu wakati taifa linazama!