Taa ya Mungu inayotumika kuchunguza yale yaliyomo kwenye moyo wa mtu

Taa ya Mungu inayotumika kuchunguza yale yaliyomo kwenye moyo wa mtu

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,237
Reaction score
1,744
Mit 20:27 SUV
[27] Pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake.

Ukisikia unachunguzwa au unafuatiliwa nyendo zako zote, inaweza kukushtua na kukuongeza umakini katika kutembea kwako na kutenda kwako, wengine tunajua tunachunguzwa kila wakati kutokana na kazi zetu au majukumu yetu.

Kimwili tunaweza tusijulikane kwa baadhi ya mambo, hata kama kuna watu watakuwa karibu na sisi kutufuatilia hatua kwa hatua kwa yale tunafanya, kuna mahali wanaweza kukwama na wasijue baadhi ya mambo yetu.

Mungu ameweka taa ndani yetu, taa inayoweza kuangaza mambo ya sirini yakawa wazi mbele zake, bila kujalisha yanafinyika katika usiri mkubwa au maficho ya namna gani, hii taa aliyoiweka Mungu inamlika kila kitu.

Tunaweza tukawa na kamera nyingi za kutusaidia kujua matukio mbali ya siri, ila fahamu pamoja na kamera hizo unaweza kukosa kujua baadhi ya matukio, maana yatafanyika katika eneo ambalo hutojua kabisa.

Katika mstari huu, neno pumzi kwa maana nyingine ni roho ya mwanadamu iliyoumbwa na Mungu, ni ile sehemu ya ndani ya mtu, kwa mwanamume na mwanamke, roho ya mwanadamu katika uumbaji wa Mungu ni jambo la kwanza lililofanyika kisha ikavalishwa katika miili miwili, yaani mwili wa mwanaume na mwanamke.

Mwa 2:7 SUV
[7] BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Roho hii ya mwanadamu ndio injini, ndio chanzo cha dhamiri, ufahamu, na ule uhusiano wa kiroho alio nao mtu na Mungu. Mungu anapotaka kuwasiliana na wewe, atasema nawe kupitia mtu wa ndani, sikio lako la ndani likiwa vizuri litaweza kutambua sauti ya Mungu.

Mungu akitaka kumchunguza mwanadamu, anatumia chombo hichi cha roho ya mwanadamu, taa hii inaweza kumwangazia mwanadamu na akawa wazi mbele za Mungu.

Mfano, mtu akitaka kuona kitu kilicho kwenye giza, atatumia tochi au taa, ataweza kuona hicho kitu vizuri na kwa uwazi, ndivyo ilivyo na kwetu, Mungu hutumia Pumzi ya mtu, au roho ya mwanadamu kumchunguza yeye mwenyewe na kujua hali yake.

Elewa hili, Mungu akitaka kujua hali yako ya kiroho, atatumia roho ileile aliyoiumba Yeye na kuiweka ndani ya mwili wako, bila kujalisha una siri gani umeibeba kwenye moyo wako, mbele za Mungu hakuna siri, upo wazi sana.

Tunapaswa kuwa na roho safi mbele za Mungu, na dhamiri zetu zinapaswa kuwa wazi mbele za Mungu, tukijua hatuwezi kudanganya kitu mbele zake, bila kujalisha watu wanatuona ama hawatuoni, hakikisha moyo wako unakuwa safi mbele za Mungu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom