TAA yatangaza viwango vipya vya maegesho ya magari, viwanja vya ndege na faini zake kufika hadi Laki moja

TAA yatangaza viwango vipya vya maegesho ya magari, viwanja vya ndege na faini zake kufika hadi Laki moja

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetangaza viwango vipya vya ada za maegesho ya magari katika viwanja vya ndege, huku ada za saa ya kwanza zikianzia Shilingi 3,000 kwa magari ya abiria.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, magari ya abiria yatalipia Shilingi 3,000 kwa saa ya kwanza, huku mabasi madogo na magari aina ya van yakitozwa Shilingi 5,000, na mabasi pamoja na malori yakitozwa Shilingi 10,000 kwa saa ya kwanza.

Kwa kila saa ya ziada, magari yote yataongezewa ada ya Shilingi 1,000.

Kwa upande wa maegesho ya muda mrefu, magari yatakayopaki kwa kipindi cha siku 1 hadi 7 yatalipia Shilingi 25,000, huku kuanzia siku ya nane ada ikiwa Shilingi 15,000.

TAA pia imeweka adhabu kwa baadhi ya ukiukwaji wa taratibu za maegesho. Maegesho yasiyoruhusiwa (Wrong Parking) yatatozwa Shilingi 50,000, kupoteza kadi ya maegesho Shilingi 30,000, kukwepa malipo ya maegesho (Parking Evasion) Shilingi 50,000, teksi isiyoruhusiwa kuingia (Unauthorized Taxi) Shilingi 100,000, huku mwendo kasi (Overspeed) ukitozwa Shilingi 30,000.

Tangazo hilo limeeleza kuwa baadhi ya magari na taasisi zimepewa msamaha wa ada, ikiwemo magari yenye vibali maalum pamoja na mahakimu, viongozi wa mikoa na wilaya, Shirika la Msalaba Mwekundu na magari ya wagonjwa (ambulance).

photo_2026-09-28_23-43-03.jpg
 
Wanachowaza wao ni kuongeza gharama tu kila kukicha badala ya kumpunguzia gharama msafiri wao wanaongeza sijui huwa wanawaza nini..
 
Tax zisizoruhusiwa ni kama Bolt ? Ama kweli airport sio kwa wote, mimi huwa natoka mpaka nje na bolt, Tax za mle ndani nauli zao zina machozi ya hizi tozo 🤣🤣
 
Wizi mtupu , yaani mtu amekuja kupata huduma kwao , akipaki gari nje unamchaji pesa ..Hii ni tatizo kubwa hata tukiende kwenye intermodal transport , gharama zitakuwa maradugu.
 
Na Bado airport ya Dar, mwendokasi zitaingia ndani kabisa. Wale tax wajipang
 
Kwa kweli ni hatari. Inabidi mtu akusubirie nje ya airport maana hizo fees siyo rafiki
Tax zisizoruhusiwa ni Bolt ? Ama kweli airport sio kwa wote, mimk hua natoka mpaka nje na bolt, Tax za mle ndani nauli zao zina machozi ya hizi tozo 🤣🤣
 
Hapa nimekuandikia vizuri, kwa Kiswahili fasaha na cha kitaalamu - tayari kwa kutuma TAA au kuposti:

---

MALALAMIKO KUHUSU GHARAMA MPYA ZA MAEGESHO - JNIA

Leo tarehe 02/10/2026 nilifika katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kumsindikiza ndugu yangu anayesafiri. Nimekutana na mabadiliko ya gharama za maegesho ya magari ambayo yamepanda kwa kiasi kikubwa.

Nimekaa maegeshoni kwa dakika 15 tu, lakini nimelipishwa TZS 3,000. Cha kushangaza zaidi, malipo hayo hayakuenda kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), bali kwa kampuni binafsi inayoitwa PARKTECH TANZANIA. Hata tiketi wanazotoa zinafanana na za Mlimani City na Dar Village.

Baada ya kufuatilia, nimebaini TAA walitangaza bei mpya tarehe 29/09/2026 kama ifuatavyo:
S/N | MAELEZO | GHARAMA
1 | Malipo kwa Saa ya kwanza | Gari ndogo: 3,000/= , Mini Bus/Van: 5,000/= , Basi/Lori: 10,000/=
2 | Kila saa ya ziada | 1,000/=
3 | Long-Term Parking | Siku 1-7: 25,000/= , Kuanzia siku ya 8: 15,000/=
4-8 | Faini mbalimbali | 30,000/= hadi 100,000/=
Hoja na Maswali yangu:

1. Kwanini bei imepanda? Hakuna maboresho yoyote ya miundombinu yanayoonekana uwandani zaidi ya kuingia kwa kampuni mpya ya ukusanyaji.

2. TAA ni taasisi ya umma ambayo jukumu lake kubwa ni kutoa huduma kwa wananchi, si kufanya biashara. Kwanini gharama zake ziwe juu kuliko za Mlimani City na Dar Village ambazo ni kampuni binafsi za kibiashara na zinalipisha TZS 1,000 tu kwa saa?

3. Gharama hizi mpya haziendani na uhalisia wa huduma. Hakuna kilichoongezeka, lakini wananchi tunalazimishwa kulipa TZS 3,000 hata kwa dakika 15.

4. Kuingia kwa kampuni binafsi kukusanya mapato ya kiwanja cha umma kunaleta maswali mengi. Kama lengo ni kuboresha huduma, kwa nini wananchi ndio wabebeshwe mzigo mzito?

Naiomba Serikali na Mamlaka husika iangalie upya bei hizi. Ni kandamizi kwa wananchi wa kawaida na haziendani na dhamira ya Serikali ya kuwasaidia wananchi.
 
Leo tarehe 02/10/2026 nilikuwa namsindikiza mtu kusafiri Airport (JNIA), nikakuta gharama za kuegesha magari zimepanda.

Nilikaa dakika 15 lakini nikalipa TZS 3,000 cha kushangaza zaidi hela hiyo haiendi kwenye mamlaka husika bali kwenye kampuni inaitwa PARKTECH TANZANIA.

Baada ya kufuatilia nikaona walitangaza bei hizo mpya terehe 29/09/2026 kama ifutavyo

S/NMAELEZOGHARAMA
1Malipo kwa Saa ya kwanzaGari la abiria: TZS 3,000/=Mini Bus au Van: TZS 5,000/=Bus au Lori: TZS 10,000/=
2Kila Saa ya ziada kwa magari yoteTZS 1,000/=
3Maegesho ya muda mrefu (Long-Term Parking)Siku 1–7: TZS 25,000/=Kuanzia siku ya 8: TZS 15,000/=
4Maegesho yasiyo sahihiTZS 50,000/=
5Kupoteza kadi ya maegeshoTZS 30,000/=
6Kuwekwa malipo ya maegeshoTZS 50,000/=
7Teksi zisizoidhinishwaTZS 100,000/=
8Kuendesha kwa mwendo kasiTZS 30,000/=


Nimejiuliza maswali yafutayo

1. Kwanini bei imepanda, je ni kwa sababu kuna maboresho ya kimiundo mbinu yamefanyika tofauti. Jibu ni hakuna zaidi ya kuona kampuni mpya inayokusanya ya PARKTECH TANZANIA. Kwa sababu ticket ni kama za mliman city na Dar village

2. Kwa hiyo sijaona sababu yoyote iliyopekea kwamba kuna gharama zimepanda

3. Mbona mliman city na Dar city bei zake ziko chini na wale wanafanya biashara tofauti na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania ambayo jukumu lake ni kutoa hudoma kwa wananchi na sio kufanya biashara?

4. Je, labda Kwasababu kuna kampuni mpya ambayo ndo nimeona inakusanya hizo hela PARKTECH TANZANIA. Lakini mbona mliman city na Dar village ni kampuni binafsi lakini bei zake ziko chini. Kwa saa ni TZS 1,000

5. Kiualisia bei hizi mpya haziendani na huduma inayotolewa kwa sababu hakuna kilichoongezeka

6. Mtu huwezi kukaa dakika 15 mpaka lisaa ukilipa TZS 3,000 alafu huseme lengo la serikali ni kuwasaidia wananchi na hata kama ni kufanya biashara bado bei ziko juu

7. Hii kampuni mpya inayokusanya inatakuwa dili za wapigaji

Hizi bei haziendani na uhalisia wa huduma, serikali iengalie hili
 

Attachments

Back
Top Bottom