Leo tarehe 02/10/2026 nilikuwa namsindikiza mtu kusafiri Airport (JNIA), nikakuta gharama za kuegesha magari zimepanda.
Nilikaa dakika 15 lakini nikalipa TZS 3,000 cha kushangaza zaidi hela hiyo haiendi kwenye mamlaka husika bali kwenye kampuni inaitwa PARKTECH TANZANIA.
Baada ya kufuatilia nikaona walitangaza bei hizo mpya terehe 29/09/2026 kama ifutavyo
| S/N | MAELEZO | GHARAMA |
| 1 | Malipo kwa Saa ya kwanza | Gari la abiria: TZS 3,000/=Mini Bus au Van: TZS 5,000/=Bus au Lori: TZS 10,000/= |
| 2 | Kila Saa ya ziada kwa magari yote | TZS 1,000/= |
| 3 | Maegesho ya muda mrefu (Long-Term Parking) | Siku 1–7: TZS 25,000/=Kuanzia siku ya 8: TZS 15,000/= |
| 4 | Maegesho yasiyo sahihi | TZS 50,000/= |
| 5 | Kupoteza kadi ya maegesho | TZS 30,000/= |
| 6 | Kuwekwa malipo ya maegesho | TZS 50,000/= |
| 7 | Teksi zisizoidhinishwa | TZS 100,000/= |
| 8 | Kuendesha kwa mwendo kasi | TZS 30,000/= |
Nimejiuliza maswali yafutayo
1. Kwanini bei imepanda, je ni kwa sababu kuna maboresho ya kimiundo mbinu yamefanyika tofauti. Jibu ni hakuna zaidi ya kuona kampuni mpya inayokusanya ya PARKTECH TANZANIA. Kwa sababu ticket ni kama za mliman city na Dar village
2. Kwa hiyo sijaona sababu yoyote iliyopekea kwamba kuna gharama zimepanda
3. Mbona mliman city na Dar city bei zake ziko chini na wale wanafanya biashara tofauti na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania ambayo jukumu lake ni kutoa hudoma kwa wananchi na sio kufanya biashara?
4. Je, labda Kwasababu kuna kampuni mpya ambayo ndo nimeona inakusanya hizo hela PARKTECH TANZANIA. Lakini mbona mliman city na Dar village ni kampuni binafsi lakini bei zake ziko chini. Kwa saa ni TZS 1,000
5. Kiualisia bei hizi mpya haziendani na huduma inayotolewa kwa sababu hakuna kilichoongezeka
6. Mtu huwezi kukaa dakika 15 mpaka lisaa ukilipa TZS 3,000 alafu huseme lengo la serikali ni kuwasaidia wananchi na hata kama ni kufanya biashara bado bei ziko juu
7. Hii kampuni mpya inayokusanya inatakuwa dili za wapigaji
Hizi bei haziendani na uhalisia wa huduma, serikali iengalie hili