Taaluma za Afya zinazomuwezesha mtu kujiajiri mwenyewe, bila kusubiri kuajiriwa

Taaluma za Afya zinazomuwezesha mtu kujiajiri mwenyewe, bila kusubiri kuajiriwa

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Orodha kamili ya taaluma za afya na aina ya biashara mtu anazoweza kumiliki/kujiajiri bila mtaji mkubwa—mfumo wa “Skill → Business” (Taaluma - Biashara).

📌 ORODHA YA TAALUMA ZA AFYA NA BIASHARA ZAKE ZA KUJIAJIRI​


1. Pharmacist (Mfamasia)​

Huyu ni mtu aliyesomea kuhusu Dawa za magonjwa ya binadamu.
➡️ Anamiliki Pharmacy (Famasi)
➡️ Duka la vifaa tiba
➡️ Ushahuri wa unywaji wa dawa
➡️ Huduma za matumizi ya dawa majumbani

Anaweza kuanzisha biashara ya Famasi popote pale nchini kwa sababu watu wanaugua kila siku. Haiitaji wafanyakazi wengi, anaweza kuanza na kiduka kidogo tu akiuza dawa muhimu za binadamu.


2. Optometrist / Optician​

Huyu ni Daktari wa magonjwa ya macho. Wanakuwaga na;
➡️ Duka la miwani (Optical shop)
➡️ Huduma inayotembea ya ugunduzi wa magonjwa ya macho
➡️ Huduma ya kuweka Frame & lens kwa rejareja

Huyu akiwa na duka lake maeneo mengi hasa mijini hawezi kulala njaa. Magonjwa ya macho na simu hizi na vyakula hivi ni mengi sana... kiduka kimoja tu chenye miwani na lens na vifaa vya macho inatosha kabisa kuanza biashara. Kilichobaki ni wewe kuchonga tu lense kwa wenye miwani mibovu tu, au wenye magonjwa ya kutokuona vizuri.


3. Physiotherapist​

Huyu ni Daktari wa mazoezi ya viongozi vya binadamu, kazi yake kubwa anakuwa kasomea mwili wa binadamu hususani hasa pale unapohitaji tiba ya mazoezi. Sio kila ugonjwa unafanyiwa mazoezi ya nyumbani, mengine yanahitaji awepo mtu wa tiba ya mazoezi. Hawa jamaa wanaweza kuwa na
➡️ Gym / Fitness studio
➡️ Rehabilitation center (Kituo cha matibabu kwa njia ya mazoezi kwa wagonjwa wenye stroke, kisukari, uti wa mgongo, mifupa n.k)
➡️ Home physiotherapy services (Wanaweza kutoa huduma ya kuja nyumbani kukufanyisha mazoezi ya kimatibabu)
➡️ Sports therapy clinic (pia umiliki vituo maalumu vya matibabu kwa njia ya mazoezi kwa wanamichezo kama wa mpira wa miguu, basketball na michezo mingine inayokumbwa na majeraha)

Unaweza kujenga au kupanga chumba Chako chenye vifaa vya mazoezi ukaanza kutoa tiba na kuweka appointment za wagonjwa Kuja kufanya mazoezi kwa siku, wiki au miezi. Huku pia ukiwa na Gym ya mazoezi kwa watu wa kawaida.


4. Medical Laboratory Technologist​

Huyu ni mtaalamu wa uchunguzi wa wadudu au visababishi vya magonjwa ya binadamu. Mara nyingi wanamiliki;
➡️ Maabara ya uchunguzi (Diagnostic Lab)
➡️ Mobile lab screening (Maabara zinazotembea, kwenye makongamano na mikutano mbalimbali kwa ajili ya kupima magonjwa mbalimbali)
➡️ Sample collection point (Wanakuwa na vituo vya ukusanyaji sampuli kwa ajili ya vipimo kwa ajili ya kupeleka maabara ya Taifa, kwa magonjwa yanayohitaji Sampuli kutunzwa kwa ufanisi, vilevile kuna zile sampuli za magonjwa kama Polio au Measles, wagonjwa wao uwa wanatafutwa sampuli zao zikafanyiwe uchunguzi maabara ya taifa, kwa hiyo wewe unaweza kuwa dalali wa ukusanyaji sampuli za magonjwa Kisha kuzipeleka maabara ya taifa hususani magonjwa yanayohitaji kutaarifiwa "Notifiable Disease")
➡️ Point-of-care testing center (Pia vituo vya upimaji wa haraka, kwa vipimo vinavyochukua dakika chache kutoa majibu mfano Ukimwi, Malaria, wingi wa damu etc)

Taaluma hii haiitaji mtaji mkubwa ni wewe mwenywe tu na vifaa vyako na chumba chako.


5. Nurse (RN/EN) and Midwife​

Huyu ni muuguzi, anaweza kujiajiri kupitia kuwa na
➡️ Home nursing care agency (kuwa wakala wa kutolea huduma za kiuuguzi majumbani, mfano kuna mgonjwa anahitaji kubadilishiwa mrija wa mkojo yuko nyumbani basi nurse anaweza kutoa huduma hiyo kwa kumfata mgonjwa nyumbani)
➡️ Wound care clinic (kuwa na kituo cha kusafishia vidonda kwa watu wenye vidonda mbalimbali ikiwemo vya cancer, sukari, ajali)
➡️ Maternity/home midwifery services (Kituo cha wamama wajawazito kwa ajili ya upimaji wa mimba na kujifungua)
➡️ Injection & BP monitoring point (Kituo cha kuchoma sindano za dawa na kupimia pressure)

Nurse haitaji hospital hili kutoa huduma, mfano abaweza kuwa na kiduka chake kwa ajili ya wagonjwa wenye muendelezo wa kuchoma sindano, badala warudi labda hospitali wao wanaenda tu na dawa zao kwenye duka la nurse (Sio famasi) hili kuwachoma.

Kwenye hii biashara anaweza kuwa nurse Peke yake au wakajiajiri zaidi hili kusaidizana kazi


6. Nutritionist / Dietitian​

Mtaalamu wa lishe, huyu anaweza kuwa na
➡️ Nutrition clinic (kituo cha lishe kwa ajili wa wagonjwa wenye matatizo ya lishe, au wenye kuhitaji mafunzo ya ulaji na mbadala wa vyakula kwa wenye shida na vyakula fulani kulingana na hali walizokuwa nazo, mfano watoto wenye utapiamlo, wagonjwa wa kisukari, shida za moyo, pressure na kadharika)
➡️ Weight management center (Kituo cha mafunzo ya ulaji kukabiliana na ongezeko au upungufu wa uzito wa mwili)
➡️ Online nutrition coaching (Mafunzo ya mitandaoni kuhusu lishe)
➡️ Corporate wellness consultancy (Kituo cha mahojiano na ushahuri kuhusu utamamu wa mwili hasa kuhusiana na lishe)

Unaweza ukawa na ofisi yako tu yenye mafundisho kuhusu lishe kwa wenye kuhitaji huduma, pia unaweza kuwa na jiko kwa ajili ya kufundisha maandalizi ya milo kamili. Ambapo unakuwa na darasa kwa ajili ya wateja wako wenye kuhitaji Elimu hiyo.



7. Clinical Officer / Medical Doctor​

Huyu ni tabibu au Mganga wa magonjwa ya binadamu: Huyu anaweza kuwa na
➡️ Mini-clinic / Home-based clinic (Ofisi ndogo binafsi au ofisi inayohusu kutoa huduma majumbani kwa kuona wagonjwa walioshindwa kufika hospitali kutokana na Changamoto mbalimbali)
➡️ Telemedicine practice (Kutoa huduma na ushahuri wa kimatibabu kwa njia ya Simu au Video call)
➡️ Chronic care management service (Huduma yenye kuhitaji mgonjwa kuonwa na Daktari kwa muda mrefu, ambapo labda muda na kazi za hospitali zinakula sana muda hivyo muda unakuta hautoshi mgonjwa kupata huduma na kuonwa vizuri kwa kina na Daktari hususani kwa wenye magonjwa sugu yenye kuhitaji huduma ya muda mrefu kwa siku, hivyo Daktari anaweza kuwa na ofisi yake binafsi nje ya muda au siku za kazi hili kumuhudumia mgonjwa vizuri)



8. Dentist / Dental Therapist​

Huyu ni Daktari wa kinywa na meno; anaweza kuwa na
➡️ Dental clinic (Clinic ya wenye matatizo ya kinywa na meno, kwa ajili ya kuwahudumia watu wenye matatizo hayo)
➡️ Mobile dental screening (schools, companies)- (Anaweza kuwa na ratiba ya kupata tender za kuwatembelea wanafunzi mashuleni kuwapa elimu ya utunzaji kinywa na meno na namna ya kuepuka magonjwa hayo)
➡️ Cosmetic dentistry services (Anaweza kuwa na kituo cha kutengeneza na kurekebisha meno kwa wale wenye kuhitaji meno ya urembo au meno bandia, au wenye kutaka kuchonga meno ya dhahabu)
➡️ Oral hygiene shop (Pia wanaweza kuwa na duka kwa ajili ya kuuzia vifaa vya usafi wa kinywa na meno, mfano dawa za meno, perfume za kinywa, na vifaa vingine)




9. Radiographer / Sonographer​

Huyu ni mtu wa mionzi, anaweza kuwa na
➡️ Portable ultrasound services (huduma ya ultrasound ya haraka au hile ya kuhitajika papohapo)
➡️ Diagnostic imaging center (anaweza kuwa na kituo kidogo cha kufanyia huduma ya mionzi kwa kulipia, mfano X-ray)
➡️ Community pregnancy ultrasound days (Anaweza kufanya huduma ya kupanga ratiba ya kufanya kipimo cha ultrasound ya wajawazito kwa kulipia katika maeneo ambayo kuna uhaba wa kifaa icho hasa vijijini ndani ndani au hata maeneo ya mjini. Unatenga siku ya clinic maalumu ya wajawazito kufanya ultrasound kwa kila mwezi au miezi 3 kwa kulipia)




10. Psychologist / Counsellor​

Huyu na Daktari wa magonjwa ya afya ya Akili. Siku hizi vichaa ni wengi, Daktari huyu anaweza kuwa na
➡️ Mental health counselling clinic (Klinik maalumu ya kulipia kwa ajili ya wagonjwa wenye msongo wa mawazo, wanahitaji huduma ya matibabu ya akili)
➡️ Online therapy (Huduma ya mitandaoni ya afya ya akili)
➡️ Corporate mental wellness programs (Huduma ya kuzungumza na watumishi au wanafunzi kuhusu utimamu wa afya ya akili makazini na mashuleni)
➡️ Marriage & relationship counselling (Elimu kuhusu Maisha, mahusiano, na ndoa hususani yenye kuhusisha afya ya akili)

Unalipia kupata huduma



11. Environmental Health Officer​

Huyu ni Afisa afya mazingira
➡️ Pest control business (anaweza kutoa huduma ya kupambana na wadudu kama mbu, kunguni, mende, mchwa kwa kufanya fumigation mashuleni, kwenye mataasisi, mahotelini, kwenye usafiri wa umma)
➡️ Water testing & sanitation consultancy (Huduma ya maji taka, kwa kuwa na kampuni ya unyonyaji maji taka na usafishaji kwenye majiji na majumbani kwa kuomba tender)
➡️ Occupational safety training (utoaji elimu ya usalama makazini)
➡️ Food safety inspections (Huduma ya ukaguzi wa vyakula kwa ajili ya usafi na afya masokoni na kwenye mahoteli)


12. EMT / First Aid Specialist​

Huyu na mtoa huduma ya dharura; anaweza kuwa na
➡️ First Aid training company (Kampuni ya huduma ya kutoa mafunzo kupambana na nyakati za dharura hasa zenye kuhitaji matibabu ya huduma ya kwanza)
➡️ Event medical standby services (Kuwa na huduma ya kwanza na kumiliki kituo cha huduma ya kwanza chenye ambulance kwa ajili ya kusafirisha watu wenye kuhitaji unaglizi maalumu kabla ya kufika hospital, mfano kwenye ajali mbalimbali)
➡️ CPR & BLS training center (Kituo cha kufanya mafunzo ya utojai huduma ya kwanza kwa kila mtu hasa makazini pale linapotokea janga)




17. Biomedical Engineer / Technician​

Huyu ni mhandisi wa vifaa tiba. Anaweza kuwa na huduma ya
➡️ Medical equipment repair shop (duka la matengenezo ya vifaa tiba vilivyoharibika)
➡️ Calibration services (Kituo cha lifanyia Calibration ya vifaa tiba)
➡️ Hospital equipment installation (Ofisi maalumu kwa ajili ya kuomba tender za ku-install vifaa tiba mahospitalini)
➡️ Sale of refurbished hospital devices (Duka la kuuzia vifaa tiba vipya na refurb)

​

 
Wewe somea Nursing halafu uanze kutafuta wagonjwa wa kuhudumia nyumbani (huku ulimwengu wa tatu)
au sijui usomee Environmental Health Officer halafu ujiajiri? labda ufungue kampuni ya fumigation na sijui utaanzia wapi ukiwa fresh na upate soko.
Ingekuwa rahisi hivyo watu wote si wangejiajiri? ukiwa mwalimu fungua shule, ukisoma account, saidia watu mahesabu ya bishara, Ukisoma Sheria saidia watu kesi, nk nk nk
vitu vingine ni rahisi kuandika nyuma ya key board
 
Wewe somea Nursing halafu uanze kutafuta wagonjwa wa kuhudumia nyumbani (huku ulimwengu wa tatu)
au sijui usomee Environmental Health Officer halafu ujiajiri? labda ufungue kampuni ya fumigation na sijui utaanzia wapi ukiwa fresh na upate soko.
Ingekuwa rahisi hivyo watu wote si wangejiajiri? ukiwa mwalimu fungua shule, ukisoma account, saidia watu mahesabu ya bishara, Ukisoma Sheria saidia watu kesi, nk nk nk
vitu vingine ni rahisi kuandika nyuma ya key board
Think big
 
Back
Top Bottom