KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Fungua kesi ya defamation watakulipa fidia na litakuwa funzo kwao na kwa makampuni uchwara kama hayo.

Hawana credibility ya kukutangaza kwa watu ambao hukuwaweka kama wadhamini wako.

Pia deadline ilikuwa bado na pia hata deadline ingepita bado wangekupa muda wa ziada wa kulipa deni lao.
 
Hii adha alikutana nayo PS wa ofisini kwetu, tulimshauri atafute mwanasheria akaogopa akaishia kulalamika. ila yeye case yake ni tofauti kidogo, walimdhalilisha akiwa ameshafanya malipo tayari na wao ndio walichelewa kuconfirm malipo.
Kwanini watu wanaacha pesa za wazi wazi hivi? Hapo akifungua kesi ya defamation anashinda maana sheria ipo wazi huwezi kumtangaza mtu mitandaoni kwamba unamdai pasipo kufuata procedures zote.
 
Kuwapa access haimaanishi watumie namba zake unless wametaja hicho kipengele.
 
Wananitishia kuwa watanitafta niwatejeshe na gharama walizotumia, au ni mikwara tu.

Sema wameniaibisha sana
Matapeli tu hao wanafanya online business kitapeli hawalipi kodi mbalimbali za serikali na ukute hawana kibali kutoka wizara ya fedha kufanya biashara mtandao.

Hao wakifikishwa mahakamani wataumbuka kwa mambo mengi sana na kukulipa fidia juu.
 
Wanakupunguzia heshima!

Wapo watu wanakuheshimu na ni muda hawajasikia kutoka kwako so wakiona sms dizain hiyo wanasema huyu jamaa alivyokuwa smart siku hizi amekuwa tapeli anatapeli mpaka mitandaoni?basi siyo wa kumuamini tena.
Ndicho ninachohisi kiko kichwani mwa watu wangu sasahivi
 
Matapeli tu hao wanafanya online business kitapeli hawalipi kodi mbalimbali za serikali na ukute hawana kibali kutoka wizara ya fedha kufanya biashara mtandao.

Hao wakifikishwa mahakamani wataumbuka kwa mambo mengi sana na kukulipa fidia juu.
Mimi interest zao ndiyo zinanifanya nipate wasi wasi kuwa hawa ni wahuni tu.
 
Wananitishia kuwa watanitafta niwatejeshe na gharama walizotumia, au ni mikwara tu.

Sema wameniaibisha sana
Wataishia kutuma sms za vitisho tu. Mwongozo wa BOT ni wanaotakiwa kukopesha ni wale wenye leseni. Ingia website ya bot utaona majina ya kampuni zote zenye leseni ya kutoa mikopo. Hao ni wapigaji tu
 
H
Hata kama dead line ingekuwa imepita kuna due interest (ada ya ucheleweshaji) huwa wanaweka.

Ndiyo maana mimi naona kwa kunitangaza kisheria wamenikosea.
 
Nipo kwenye cycle ya hii industry, ni ngeni kwa Tz ila Kenya, Nigeria, Ghana kote hii industry ilishapita.

Kuna sheria za kudai na kuwasiliana na mteja, kuna sheria pia za kuwasiliana na 'wadhamini' wa mteja.

Kampuni hujitahidi kucheza ndani ya hizi sera na sheria. Inatarajiwa mkopaji akipigiwa apokee kama ana plan mpya ya ulipaji aiseme ama ana changamoto n.k

Anayekupigia ana target ya kuifikia kwa siku ili alipwe mshahara, na wengi hua na prejudice kua mteja hataki kulipa ndiyo sababu wengi hufanya hivyo.

Consult mwanasheria, angalia wapi wamekosea na kama sheria inakupa locus standi
 
ukiunstall application vp bado wanaweza kuaccess your phonebook?
 
Tafuta mwanasheria peleka mahakamani hizo mbwa.


Nawaza niwafanyie uhuni flani ili iwe fundisho kwao sema majukumu ya kifamilia yamenibana.


Ila hizi mambo zikiendelea nitaanza kudeal nao mmoja baada ya mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…