KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Matapeli tu hao wanafanya online business kitapeli hawalipi kodi mbalimbali za serikali na ukute hawana kibali kutoka wizara ya fedha kufanya biashara mtandao.

Hao wakifikishwa mahakamani wataumbuka kwa mambo mengi sana na kukulipa fidia juu.
Ukiwashtaki arrest warrant ikitoka unaenda kuwakamata wakiwa ofisi gani. Yani polisi hawahawa wa bongo ndio uwaambie cyber itrack namba za hao wakopeshaji wakakamatwe, na hapo amri itoke mahakamani. Mtu mwenyewe ndio huyu phone book namba 200+ hakuna wa kumkopesha 50,000.

Huo usumbufu bora uachane nao uwalipe. Sanasana anaweza watishia awasisitize watume sms ya kuomba radhi kwa hizo namba wajifanye hakukopa au hakuchelewesha kulipa.
 
Kama laini uliyojiunga nayo ukaamua kuivunja hapo hawapati kitu, maana wao wanategemea zaidi activation ya laini na location.
Sio kweli.
Unapo allow access to contacts, hapo hapo wanakuwa na uwezo wa kupata data zako (sms na contact) na zinakuwa stoted kweye system yao. Ila kadri utakavyokuwa unaendelea kuwa active nao wanapata updates kwenye system kama umeweka contact mpya. Ukiamua kuvunja simcard wao wanabaki na data zako bila updates.

Pia kwa sasa kupitia NIDA wanaweza kujua simcard zako zingine unazotumia (japo ni kinyume cha sheria ila wanapata ushirikiano kwa wafanyakazi wa makampuni ya simu kwa hongo kidogo wanawapa taarifa.)
 
Hizi kampuni hazina muda mrefu zitafilisika kwa kesi mahakamani,maana Mimi wamenipigia kwamba wananidai wakati hata kumi mbovu haijaingia!
Sasahivi wamempigia mzee wangu kijijini wamemtaitisha, mzee amenicheki kanambia anataka kutupa laini.

Nimemwelewesha lakini mzee nae haelewi 😮‍💨
 
Hizi kampuni hazina muda mrefu zitafilisika kwa kesi mahakamani,maana Mimi wamenipigia kwamba wananidai wakati hata kumi mbovu haijaingia!
Haya mambo yanawezekana kwenye nchi yenye raia wajinga kama Tanzania tu. Sina kusema ila nimebaki kushangaa tu. Yaani mtu akope halafu asipolipa wanatumia msg contact wake walioko kwenye simu? Mnatania au yanatokea kweli?
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
Safi IT
 
Fungua kesi ya defamation watakulipa fidia na litakuwa funzo kwao na kwa makampuni uchwara kama hayo.

Hawana credibility ya kukutangaza kwa watu ambao hukuwaweka kama wadhamini wako.

Pia deadline ilikuwa bado na pia hata deadline ingepita bado wangekupa muda wa ziada wa kulipa deni lao.
Mkuu wewe ni mtu na nusu sana ani.

Umenifanya fikra zangu zikafunguka.

Nimeingia website ya BOT kama ulivyosema kuwa kule kuna ufafanuzi.

Nimekuta orodha ya kampuni za micro-y finance zenye leseni ya BOT, ziko kama kampuni 1500 na point kidogo.

Kati ya hizo 1500 zenye leseni, MKOPO FASTA (PESA M LOAN) haipo.

Alafu pia nikasoma notice ikiyotolewa na BOT mwezi january 2024, inaagiza kwamba micro finance yeyote inayokukopesha ikupe nakala ya MKATABA, mimi sina MKATABA wao.

Kumbe nimekuja kugundua ni wahuni ambao wanavuna pesa kihuni.
 
Pamoja na hao jamaa kukukwaza, lakini niseme wazi watanzania pia tuwe na utamaduni wa kulipa madeni tunapokopa.

Rafiki Akimkopesha mtanzania, urafiki ujue umeisha.

Ukiwa na shida jua pia aliekupa hela kuna sehemu kajinyima ili akupe utatue tatizo lako, ukimaliza jitahidi sana kulipa deni husika.
 
Umeona sass. Mimi ndie nilikwambia angalia website ya BOT. Usiwaogope hao
 
Pamoja na hao jamaa kukukwaza, lakini niseme wazi watanzania pia tuwe na utamaduni wa kulipa madeni tunapokopa.

Rafiki Akimkopesha mtanzania, urafiki ujue umeisha.

Ukiwa na shida jua pia aliekupa hela kuna sehemu kajinyima ili akupe utatue tatizo lako, ukimaliza jitahidi sana kulipa deni husika.
Kama umenifatilia vizuri tangu awali nilisema kwamba, dead line ya kulipa deni ilikuwa ni tatehe ya jana.

Na nilitegemea nikitoka kazini saa kumi na nusu niweke pesa kwenye simu nikawalipe.

Lakini matokeo yake, jana hiyo hiyo saa saba mchana phone book yangu ikatumiwa sms kuwa mimi ni tapeli, ilinichanganya na kunipa hasira sana.

Na mpaka mda huu sijalipa na sina mpango wa kulipa.
 
mkuu ulinifungua pakubwa sana.

Sema tu sasahivi kinacho nitesa ni udhalilishaji walionifanyia.

Tayari nimeanza kutoaminika kabisa, mkuu mimi naenda kufungua shauri mahakamani
Una haki maana wamevunja privacy yako hapo na walichofanya nii kinyume cha sheria.

Unakumbuka kipindi cha magufuri walipotaja wadaiwa wa bodi ya mikopo, walitoa notice ya muda mrefu, hawakukurupuka tu na kutoa majina.

Kuna taratibu za kisheria mpaka mtu anatangazwa kama mdaiwa sugu
 
Hivi mkuu unanishauri niwalipe kwanza au nisiwalipe kabisa.

Maana mimi suala la kuwalipa nafsi yangu inakataa kabisa kwa walicho nifanyia
 
Haya mambo yanawezekana kwenye nchi yenye raia wajinga kama Tanzania tu. Sina kusema ila nimebaki kushangaa tu. Yaani mtu akope halafu asipolipa wanatumia msg contact wake walioko kwenye simu? Mnatania au yanatokea kweli?
Mimi ni muhanga wa hili mkuu, siyo utani.

Contact zangu zote zaidi ya mia mbili zimetumiwa sms hiyo jana na nimeweka screen short hapo kwenye thread.
 
Kama umenifatilia vizuri tangu awali nilisema kwamba, dead line ya kulipa deni ilikuwa ni tatehe ya jana.

Na nilitegemea nikitoka kazini saa kumi na nusu niweke pesa kwenye simu nikawalipe.

Lakini matokeo yake, jana hiyo hiyo saa saba mchana phone book yangu ikatumiwa sms kuwa mimi ni tapeli, ilinichanganya na kunipa hasira sana.

Na mpaka mda huu sijalipa na sina mpango wa kulipa.
Usiwalipe wapuuzi hao,tena wapigie simu kabisa uwafokeee.Hao jamaa wamenidhalilisha sana nawavutia gap nitafute line mpya harafu nivute mpunga na kuifutia usajiri
 
Back
Top Bottom