KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Pamoja na hao jamaa kukukwaza, lakini niseme wazi watanzania pia tuwe na utamaduni wa kulipa madeni tunapokopa.


Rafiki Akimkopesha mtanzania, urafiki ujue umeisha.

Ukiwa na shida jua pia aliekupa hela kuna sehemu kajinyima ili akupe utatue tatizo lako, ukimaliza jitahidi sana kulipa deni husika.
Kweli aisee
Mimi nimepoteza marafiki wengi sababu nilimkopa ukianza kumdai anachukia
Yaani hii kwa Wabongo ni tamaduni kabisa
 
Huenda ni mimi nilifanya makosa kwa kutopitia terms & conditions vizuri ila hawa jamaa walicho nifanyia ni uzalilishaji mkubwa sana.

Kuna app moja mtandaoni (play store) inaitwa "PESA M FINANCE".

Hawa jamaa walinikopesha elfu 42 mtandaoni kwa muda wa siku 7.

Siku jana nilitakiwa ndiyo nilipe, na jana hiyo nilikuwa kazini nikitegemea nitoke kazini jioni niwalipe pesa yao.

Lakini nashangaa jana mida ya mchana saa saba, watu wanaanza kunitumia kunipigia simu na kunifoadia sms kuwa nadaiwa.

Kumbe hii kampuni ilichofanya baada ya kunikosa hewani jana mda flani, wakatuma sms kwa watu wote walioko kwenye phone book yangu (watu zaidi ya 200) kuwajuza kuwa wananidai na nataka kuwatapeli.

Nikawa napata simu ngingi sana kutoka kwa hao watu waliotumiwa hiyo sms.

Aisee niliona ni udhalilishaji sana hii kampuni imenifanyia.

Sasa nikajiuliza walipataje majina yaliyopo kwenye simu yangu, hapo ndipo nilipokumbuka kwenye app yao ukiwa unafungua kuna sehemu itaandika "allow access to your contacts, messeges n.k" hapo ndipo walipopata majina ya phone book yangu.

Sasa tangu jana hiyo nimekosa raha kabisa baada ya kuzalilishwa na mimi nimeamua kutowalipa mpaka sasa.

Nimepata wazo la kutafta mwanasheria nikawafungulie kesi ya kunidhadhalisha wanilipe fidia, kwanini wanidhalilishe wakati dead line ya malipo ilikuwa bado haijapita
View attachment 2910966View attachment 2910967
Hahaha hao watu washapigwa sana mjini hapa. Sasa wameboresha kwa njia hiyo sawa. Mwqnzoni mwa hizo mambo walikuwa loose sana. Wakagongwa weeeee hii ndo dar salaama
 
Hiyo access uliwapa wewe mwenyewe....
Mara ya kwanza ulipoanza kutumia hiyo app ilikutaka uruhusu matumizi kama location,storage na some authority options ndio maana yamekutokea hayo....

Hao dawa yao simu inakua rooted,Una remove acces ya contact unawaomba mkopo,wanakupa....
Unafungua lucky patcher unaedit custom firmware za app halafu unafuta na application
Toa nondo kidogo mkuu
 
Mimi yalinikuta haya sina hata hamu,ila nilichopanga hawa nawatafutia laini mpya harafu na save namba za uongo uongo ili nikipiga pesa hata elfu 30,000 basi laini naofutia usajiri
Hahahaha? Ufungue line, ujaze majina ya uongo, ukope na kulipa mpaka ufike elf 30 halafu uvunje line. Kweli watu mna hasira.
 
Kwanini watu wanaacha pesa za wazi wazi hivi? Hapo akifungua kesi ya defamation anashinda maana sheria ipo wazi huwezi kumtangaza mtu mitandaoni kwamba unamdai pasipo kufuata procedures zote.
Kwa mtu aliyekopa, ukisoma Terms na Conditions zao, basi hakika huwezi kushinda kesi yeyote mahakamani dhidi yao, zile T & C’s hakika ukizisoma, huwezi kopa kwao, zinajipa nguvu na haki za ajabu sana, zingine ni uncostitutional kabisa, ila kwakuwa umekubali kwa shida zako, ishi nao tu.

Anaeweza kufungua kesi ni contacts wako wanao kuwa harassed wakati hawakushirikishwa wakati unakopa.
 
Back
Top Bottom