KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

KERO Taarifa Binafsi: Kampuni ya mkopo mtandaoni (online loan app) imenidhalilisha sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hahaaaaa, mimi Pesa X. Niliona tangazo nikadownload. Nikaingiza details baadaye nikadelete ile app na kuachana nayo. Kidogo naona nimepokea 4760 toka detax nini sijui. Sijajua ni nini, nikasearch mtandaoni. Nikajua ni wao.

Nikawatafuta kwenye page zao za FB na Instagram. Nikawaambia nataka niwarudishie 4000's yao waliyoniingizia. Jamaa wakauchuna. Baada ya wiki 2 naona simu kuwa nadaiwa 7000's toka kwao. Nikawaambia mbona nikiwatafuta niwarudishie pesa yenu mkanyamaza? Sasa hiyo 7000's nitawapa kwa kigezo gani?

Kila wiki wakawa wananipigia na deni lao kuongezeka sasa nadaiwa 15000's. Siku 2 zilizopita naona wananitumia sms, watanipeleka mahakamani. Nikawaambia silipi hata 100 kwani sijawahi omba mkopo kwenu. Nina 4000's yenu niwalipe, hiyo nyingine siijui. Mawasubiri twende Mahakamani sasa.
 
Kukushika ni ngumu sana mkuu, kuwa na amani ni mikwara tu ile, mimi pesa x wameuamua kunipotezea wenyewe tu.
Aisee, hao waduanzi kwani wangapi wanakopa. Ningekuwa mimi nisingewalipa maana wameshatumia silaha yao ya mwisho.

Alafu haina haja ya wewe kujisikia vibaya kwani sms katumiwa mtu mmoja mmoja kwahiyo kila mtu ataielewa kwa anavyo kufahamu ni rahisi kumjibu kuwa hao ni matapeli
Sijawalipa hata sasa na sina mpango.

Wamenidhalilisha sana.
 

Attachments

  • Screenshot_20240221_195721_Magic SMS.jpg
    Screenshot_20240221_195721_Magic SMS.jpg
    743.9 KB · Views: 72
Huenda ni mimi nilifanya makosa kwa kutopitia terms & conditions vizuri ila hawa jamaa walicho nifanyia ni uzalilishaji mkubwa sana.

Kuna app moja mtandaoni (play store) inaitwa "PESA M FINANCE".

Hawa jamaa walinikopesha elfu 42 mtandaoni kwa muda wa siku 7.

Siku jana nilitakiwa ndiyo nilipe, na jana hiyo nilikuwa kazini nikitegemea nitoke kazini jioni niwalipe pesa yao.

Lakini nashangaa jana mida ya mchana saa saba, watu wanaanza kunitumia kunipigia simu na kunifoadia sms kuwa nadaiwa.

Kumbe hii kampuni ilichofanya baada ya kunikosa hewani jana mda flani, wakatuma sms kwa watu wote walioko kwenye phone book yangu (watu zaidi ya 200) kuwajuza kuwa wananidai na nataka kuwatapeli.

Nikawa napata simu ngingi sana kutoka kwa hao watu waliotumiwa hiyo sms.

Aisee niliona ni udhalilishaji sana hii kampuni imenifanyia.

Sasa nikajiuliza walipataje majina yaliyopo kwenye simu yangu, hapo ndipo nilipokumbuka kwenye app yao ukiwa unafungua kuna sehemu itaandika "allow access to your contacts, messeges n.k" hapo ndipo walipopata majina ya phone book yangu.

Sasa tangu jana hiyo nimekosa raha kabisa baada ya kuzalilishwa na mimi nimeamua kutowalipa mpaka sasa.

Nimepata wazo la kutafta mwanasheria nikawafungulie kesi ya kunidhadhalisha wanilipe fidia, kwanini wanidhalilishe wakati dead line ya malipo ilikuwa bado haijapita
View attachment 2910966View attachment 2910967
Hii chai, hiyo sms ya madai imekosewa kuandikwa
 
Back
Top Bottom