A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na wimbi la taarifa binafsi za wananchi, zikiwemo majina, namba za simu na taarifa za wenza na wanafamilia, kusambaa kupitia karatasi zinazotumika kufungashia chipsi na vitafunwa.
Nyaraka hizi zinadaiwa kutoka hospitalini, taasisi za mikopo, shule, vyuo, stationaries na ofisi zinazotangaza nafasi za kazi.
Hili si suala la usafi wa mazingira pekee, bali pia ni tishio kwa faragha na usalama wa wananchi, kwani taarifa hizo zinaweza kutumiwa kwa utapeli, wizi wa utambulisho na uhalifu mwingine.
Ni jambo la busara kudhibiti vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kulinda mazingira, lakini je, tunalindaje taarifa binafsi za wananchi? Kwa nini taasisi zinazopaswa kuzihifadhi kwa usalama zinaruhusu nyaraka hizo kuishia mitaani?
Mamlaka husika na hasa PDPC wako wapi? Ni mpaka madhara yampate nani ndipo hatua zichukuliwe?
Ni wakati sasa PDPC wachunguze chanzo cha nyaraka hizi na kuhakikisha taasisi zinazingatia taratibu salama za utunzaji na uteketezaji wa nyaraka zenye taarifa nyeti.
Kulinda mazingira ni muhimu, lakini kulinda faragha na usalama wa taarifa za wananchi ni wajibu pia.