Taarifa fupi ya utekaji

Taarifa fupi ya utekaji

.

Ilikua ni asubuhi Jacob Mlay (pichani) alitoa nguo zake nje ili azifue ghafla akapokea sms kutoka kwa Deusdedith Soka, Soka akamwambia Mlay Kaka salama naomba unisindikize Polisi Chang'ombe, Polisi wamenipigia simu niende nikachukue Bodaboda yangu.

Mlay: akajibu sawa ngoja nirudishe nguo zangu ndani maana ndio nilikua nataka nianze kufua, pia naacha simu yangu hii chaji nipigie kwa Tigo yangu.

Soka: Sawa ngoja nimpigie na Dereva wangu Frank Mbise

Tangu siku hiyo Jacob Mlay, Frank Mbise na Deusdedith Soka hawajawahi kupatikana, Jacob Mlay ameacha mtoto mdogo na Mbise ameacha mtoto mdogo.

Credit: Mwaipaya FBView attachment 3260769
Mshana Jr kaa kimachale kumbuka umetoa namba yako hapa jana.
 
Nakubaliana na wewe 100%, anayetuongoza kujifanya mcha Mungu kumbe ni dictator haswa
Kabisa, ukijifanya unatoa maoni ya kurekebisha au kukosoa kitu, ghafla wanakuona ni adui na wanatafuta kukuua, hakika hawa watu ni mashetani, wanathamini madaraka yao na vyeo vyao kuliko utu wa kibinadamu
 
Hivi kama hawajamaa walipigiwa simu na polisi, halafu wakapotea je hakuna mahali pa kuanzia kweli hawa wakapatikana.

No reforms no election
 
Inauma, inasikitisha, inatia uchungu, na inaliza sana
 
.

Ilikua ni asubuhi Jacob Mlay (pichani) alitoa nguo zake nje ili azifue ghafla akapokea sms kutoka kwa Deusdedith Soka, Soka akamwambia Mlay Kaka salama naomba unisindikize Polisi Chang'ombe, Polisi wamenipigia simu niende nikachukue Bodaboda yangu.

Mlay: akajibu sawa ngoja nirudishe nguo zangu ndani maana ndio nilikua nataka nianze kufua, pia naacha simu yangu hii chaji nipigie kwa Tigo yangu.

Soka: Sawa ngoja nimpigie na Dereva wangu Frank Mbise

Tangu siku hiyo Jacob Mlay, Frank Mbise na Deusdedith Soka hawajawahi kupatikana, Jacob Mlay ameacha mtoto mdogo na Mbise ameacha mtoto mdogo.

Credit: Mwaipaya FB

Trump - RAIS wa nchi, akiwa anahutubia kwenye Bunge la senate, kuna baadhi wabunge waliamua kutoka nje kabisa. Kuna wananchi pia nao walipingana na hoja alizowasilisha. Huwezi sikia FBI au CIA wakija na kuwateka. Ukifanya hivyo Tz, ukinusurika kutekwa basi jiandae kuhojiwa uraia au kupewa kesi ya uhujumu uchumi!
 
Back
Top Bottom