Taarifa kuhusu kuondolewa kwa hitajio la VISA kwa Watanzania wanaoingia nchini DRC kuanzia Machi 20, 2025

Taarifa kuhusu kuondolewa kwa hitajio la VISA kwa Watanzania wanaoingia nchini DRC kuanzia Machi 20, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2025-03-22_16-50-27.jpg
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOLEWA KWA HITAJIO LA VISA KWA WATANZANIA WANAOINGIA NCHINI JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO (DRC) KUANZIA TAREHE 20 MACHI, 2025

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kwamba, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imeondoa hitajio la Visa kwa raia wa Tanzania wanaoingia DRC kuanzia tarehe 20, Machi, 2025.

Baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwezi Julai 2022, tarehe 2 Septemba 2023, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliondoa utaratibu wa malipo ya visa kwa raia wa DRC kwa matarajio ya nchi ya DRC pia kufuta utaratibu wa kutoza malipo ya visa kwa msingi wa kuungana mkono (reciprocity).

Serikali ya Jamhuri wa Tanzania inaamini kuwa uamuzi huu wa Serikali ya DRC ni hatua nzuri katika kuimarisha mtangamano na utakuwa na manufaa, ikizingatiwa kuna mwingiliano mkubwa wa wananchi wa nchi hizi mbili katika masuala mbalimbali ya kijamii na kibiashara. Vilevile, kuondolewa kwa hitajio la Visa kutachochea ukuaji wa uwekezaji, biashara na kupunguza gharama.

Hatua hii ni moja ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na ujirani mwema kwa vitendo, na ni ishara ya Tanzania kuzingatia miongozi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, pamoja na Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AICFTA).

IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
 
Hivi bila kumtaja Rais wa inavyoitwa awamu ya sita SSH mkuu wa Wizara Idara anakuwa anakalia kuti kavu?

Jambo hili ni jema maana haiingii akilini DRC kuwatoza watanzania kulipa USD 100 kwa kuingia DRC wakati wote tumo ndani ya EAC.
 
Back
Top Bottom