Taarifa kutoka TRA kuhusu kubadilisha umiliki wa chombo cha moto

TRA hii akili nawapa bure kabisa.
Ni mara ngapi kwa mwezi umiliki wa vyombo unabadilika?
Wangapi wanabadili? = Very few, kwa sababu ya huu urasimu wenu..
Mtajuaje Kama Mimi mmiliki halali au lah?
Hapo mnategemea kupata Bei gani?
Kuna pesa imekaa tu mifukoni mwetu hamtaki kuichukua.
Asilimia kubwa ya waendesha pikipiki hawana leseni, sio kwamba hawataki kuzinunua Ila urasimu wenu.
Sehemu za kuvhukulia leseni Ni chache mno na ziko mbali na wahitaji.
Isitoshe kumonitor asiye na leseni Ni rahisi kuliko ku monitor gari ambayo haijafanyiwa uhanisho.
Leseni moja Ni 70k.

Hii desa anaweza kuichukua mtu anayechukua PhD ya taxation.
 
Hence: watu hawatauziana na tra Watakosa mapato

Hawa majamaa wamesomea wapi!?

Udsm ndio inaleta majitu kama haya au degree za chupli chupli?

Yaani jitu linaongea kiurahisi tu halijali yaani
Saint Ivuga:

Huyu kabebeshwa gunia la miba alafu watu wamuangalie utekelezaji wake.
 
Stupidity will never end, wakati wenzao agents wanamaliza kazi TRA wanatengeneza Mazingira ya Rushwa waone sura za watu ili wawaombe rushwa
 
Kuna Jamaa aliniambia kubadilisha Kuna la umiliki. Wa gari/kadi ni laki 6🤣😅
 
Kwanink
Wakuu Someni Hii Taarifa Kutoka Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA)View attachment 1968871

=====

October 8, 2021 by Global Publishers

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi ya watu wanakuwa wamesajili vyombo vya moto lakini usajili wao ni batili, hawajasajiliwa na TRA ambapo magari yao yanakuwa yameliingiza nchini kimagendo, jambo linalopelekea magari zaidi ya moja yote yanakuwa na namba moja ya gari.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Oktoba 8, 2021 na Mercy Macha ambaye ni Afisa Msimamizi wa Kodi TRA wakati akitolea ufafanuzi katika kipindi cha Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio huku akiwahimiza wananchi kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo kubadili umiliki wa vyombo vya moto ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kuwakumba.

“Jukumu la TRA sio kukusanya kodi tu, hata kuelimisha pia. Kabla hujanunua gari lazima au chombo chochote cha moto, fika TRA ujue kama chombo hicho ni cha halali, hakidaiwi kodi, fuata taratibu wa kubadilisha umiliki kuja kwako.

“TRA tumekuja na utaratibu mpya, unapokuja kubadilisha umiliki wa chombo lazima mmiliki wa mwanzo awepo, mmiliki mpya (aliyeuziwa) awepo na atuonyeshe kitambulisho chake, chombo lazima kiwepo maofisa wetu wakikague kuanzia Chassis Number. Unapobadilisha umiliki wa chombo lazima zile kodi za uhamishaji wa chombo zichukuliwe, TRA tukusanye mapato.

“Gharama ya kuhamisha umiliki wa chombo cha moto ni Tsh 100,000 jumlisha asilimia 1 ya gharama ya ununuzi iliyoandikwa kwenye kwenye mkataba, na huu mkataba lazima uwe legal, usainiwe na mwanasheria na aweke risiti ya huduma aliyotoa.

“Kuna wanaopewa bajaji za mkataba, anaendesha akimaliza mkataba anakabidhiwa inakuwa ya kwake lakini hawaji kubadilisha umiliki, hawa nao tunawahimiza kuja TRA kubadilisha umiliki wa vyombo vyao.

“Kwa magari ambayo yameingizwa nchini yakiwa na msamaha wa kodi, wakati yanauzwa kuna utaratibu wa kufuatwa kuhakikisha msamaha hauhami kwenda kwa mtu mwingine, mhusika arudi TRA kufuata taratibu hizo. Usiuze chombo chako cha moto bila kuhakikisha umebadilisha umiliki, unayenunua hakikisha nawe unakuwa mmiliki halali wa chombo chako,” Mercy Macha, Afisa Msimamizi wa Kodi TRA.
View attachment 1969147

View attachment 1969149
Kwa nini tunalipia kadi 50,000 .. ? Huu ni udhamba mkubwa. Kwanza hatuhitaji hiyo kadi0
 
Back
Top Bottom