Uchaguzi 2020 Taarifa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itazuia Mawakala wa Vyama kuingia na simu zao katika vituo vya kupigia kura imetushtua

Ikilazimu, hata mawasiliano ya simu na internet hayatakuwepo.
 
Goli la mkono hilo, ccm bana
 

Iko kwenye kanuni ipi iliyosainiwa wapi?

Wacha maneno weka hiyo kanuni ya kuzuia simu kwenye listi zilizosainiwa hapa.

Acheni utani nyie. Safari hii tumedhamiria haswa. Ama zetu ama zenu.

ICC ataamua hili battle!
 
Iko kwenye kanuni ipi iliyosainiwa wapi?

Wacha maneno weka hiyo kanuni ya kuzuia simu kwenye listi zilizosainiwa hapa.

Acheni utani nyie. Safari tumedhamiria. Ame zetu ama zenu. ICC ataamua hili battle!
Kama unazo nguvu mbona kila wakati unawaza ICC tu jitokeze tu barabarani wakunyowe kwa kisu!
 
Bado watanzania hatujatatua tatizo kabisa. Lengo tupate tume iliyo huru ambayo haina upendeleo wowote hapo ndipo tutakuwa na uchaguzi wa huru na haki.
 

Kwani hiyo picha inapigwa kutoka wp? Hata isifanane maana yake ni form ya msimamizi ndio itapigwa picha
 
Lazima chama tawala kutumia dola ili kubaki na dola!
Au mmesahau kauli ya Katibu?!
 
Siku ukitia akili kichwani utaelewa tu umuhimu wa simu ili kupambana na wizi wa maccm kwa kutumia hila mbali mbali na simu zitasaidia kuanika wizi na uhuni wao hadharani si kwa Watanzania tu bali dunia nzima.
Hoja Hafifu kabisa..
Mawakala tayari wameaminika na Vyama vyao na sidhani kama kuna uhitaji wa kua na simu kwenye vituo na sidhani kama sheria inaelekeza kufanya hivyo.
 
Hakuna amani bila haki, funga bakuli lako

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Wapwa

Ni ukweli usiofichika kuwa CCM ina mbinu nyingi sana za uwizi wa kura, bahati mbaya nyingi tayari zimeshajulikana. Sasa kuna baadhi ambazo hazipigiwi kelele sana lakini ni mbinu mbaya sana na wakiitumia lazima watafaulu na kutakuwa hakuna pa kulalamika. mawakala muwe makini sana kwenye hili.

1 ) Watendaji kukusanya namba na vitambulisho vya kupigia kura
Kwa takribani miezi 6 sasa maeneo mengi sana, watendaji wamekuwa wakipita nyumba kwa nyumba kukusanya taarifa za wapiga kura, mfano namba ya kitambulisho na eneo unalopigia kura, kuna siku nliuliza hapa hizi taarifa wanazokusanya zinakwenda kufanyiwa nini hakuna aliyekuwa na jibu, na hii wamekuwa wakiifanya kwa siri sana.

Walichokipanga hawa jamaa, ni kwamba mfano kituo A kina wapiga kura 250, inajulikana ya kuwa sio wapiga kura wote watakaoenda kupiga kura, kwa hiyo mfano wakipiga kura watu 130, sababu tayari wana taarifa za wapiga kura wote wa kituo A wanaweza kujua nani amepiga nani hajapiga wakisaidiana na wasimamizi ndani ya kituo, kwa hiyo ni rahisi either kuleta mamluki kumalizia idadi iliyobakia wakiwa na taarifa sahihi za wapiga kura wa kituo husika au kutafuta upenyo wa kuongeza kura nyingine ndani ya box la kura. mfano wakiongoza kura 50 * vituo 50000 watakuwa wamefanikiwa kuongeza kura zaidi ya 2000,000+ .

Sasa nini kifanyike. Hapa tutagemea zaidi WAKALA kuhakikisha anajua idadi KAMILI ya watu wote waliopiga kura ndani ya kituo chake, na sio kupata idadi kutoka kwa msimamizi wa kituo. WAKALA hakikisha muda wote unakuwa kituoni, na kila anayeingia unamuhakiki sura yake ndani ya kitambulisho na unamuhesabu ili kutokuruhusu udanganyifu wowote wa idadi ya waliopiga kura.

2 ) Majimbo yaliyopita bila kupingwa

Haya majimbo yalikuwa ni mkakati wa kuongeza kura za uraisi kwao, huku kuna uwezekano mkubwa wa kupata 100% kwa kila kituo, kwa iyo tunaomba mawakala wetu muwe makini sana na wapiga kura na idadi ya watu watakaopiga kura ndani ya vituo vyenu.


Haki huinua Taifa
 
Kwani hata kukiwa na picha elfu 1 za tukio lile lile kuna ubaya gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maagizo yoyote ya Mahera yasiyo na msingi wa kisheria yapuuzwe na kudhauliwa.

Hili halimo katika sheria, lipuuzwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna. Waingine nazo tu liwalo na liwe!!
 
Napeleka makalioni kwako,wewe ukidhani napeleka wapi sheikh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…