Uchaguzi 2020 Taarifa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itazuia Mawakala wa Vyama kuingia na simu zao katika vituo vya kupigia kura imetushtua

Sasa Askofu kila mtu akipiga picha, then tuanze kutafuta picha ya nani ndio sahihi? Tume ina lengo zuri kwamba taarifa za matokeo ziwe na channel moja, sio kila mtu na matokeo yake itakuja kuleta taharuki na hatimae vurugu.Endelea kuchunga kondoo wa Bwana mambo mengine haya kuhusu. Usichanganye siasa na dini
Nakushangaa. Taharuki itatoka wapi kama matokeo yako sahihi na wazi kwa kila muwakala? Kupiga picha ni kuweka kumbukumbu "for future reference". Mnaopinga hili mna nia ya kuchezea matokeo.
 
Sasa Askofu kila mtu akipiga picha, then tuanze kutafuta picha ya nani ndio sahihi? Tume ina lengo zuri kwamba taarifa za matokeo ziwe na channel moja, sio kila mtu na matokeo yake itakuja kuleta taharuki na hatimae vurugu.Endelea kuchunga kondoo wa Bwana mambo mengine haya kuhusu. Usichanganye siasa na dini
mnaogopa nini kama mna uhakika mtashinda kihalali?
 
Rais anawapongeza team iliyowezesha mkataba mpya wa madini akiwamo professor P Kabudi . Amewaomba viongozi wa dini wawaombee sana

Maendeleo hayana vyama
Lisu aliesema tutashitakiwa sijui anajisikiaje sasa
 
Mkuu penda kufikirisha ubongo otherwise kichwa kinaweza kuwa mzigo usiyo na maana kwa miguu,NEC inasema mawakala siyo lazima kupewa nakala za matokeo na wakati huohuo inakataza simu kuhifadhi matokeo,Si ndo upuuz huu
Yaani hawa Tume wanatuona sisi wapiga kura ni mazuzu. Tushinde kwenye jua tukisubiri kupiga kura halafu mwisho wa siku wazichezee kura zetu? Wallah haikubariki kamwe.
 
SUALA LA SIMU KWA MAWAKALA: TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI MSIHARIBU UCHAGUZI WA WATANZANIA!

Taarifa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itazuia Mawakala wa Vyama kuingia na simu zao katika vituo vya kupigia kura imetushtua hata sisi viongozi wa Kanisa! Simu ina mambo mengi sana katika ulimwengu wa sasa ikiwemo kutunza kumbukumbu kwa njia mbalimbali.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiwezi kuwafanya mawakala kama 'tabula rasa' yaani watu wasioweza kuhifadhi kumbukumbu yo yote na hata kushindwa kuwasiliana. Mawakala wakiwa na simu wanaweza kupiga picha matokeo halisi ili kudhibiti wizi wa kura! Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuzuia Mawakala kuingia na simu katika chumba cha kupigia kura ni sawa na kuandaa usiri utakaopelekea mazingira ya kuibiwa au kuchakachuliwa kwa kura!

Tunaitahadharisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuacha kutoa maelekezo au kutunga kanuni kwa lengo la kufanya Matokeo ya Uchaguzi Mkuu yasiheshimike na wananchi! Ili kuleta afya ni vizuri maelekezo na kanuni za Tume zikubaliwe na vyama vyote. Tume iepuke kutoa kanuni na maelekezo katika kipindi hiki kwa lengo la kuubeba upande mmoja na kuunyonga upande mwingine!

Sisi tumekwisha kutimiza wajibu wetu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
Hiyo ni kanuni ya tume, na chama chako chadema walisaini fomu ya maadili ya uchaguzi! Na walikubali, Sasa wewe askofu mchunga siasa unapinga Kama Nani?

Viongozi wa dini Leo walikuwa ukumbi wa Mwalimu Nyerere wakati Rais anapokea gawio la billion 100!!
Wewe endelea na siasa, siku ya mwisho Mungu atakuuliza haesabu yake
 
Tununue digital camera zile ndogo, maana wamezuia simu sio digital camera, tupige picha matokeo tutoe memory card tukishatoa unatia mdomoni unameza, hata wakichukua camera tayari ushahidi upo tumboni
Doctor anakufanyia oparesheni anakuta memory imeharibika,anaandika taarifa ya kifo.
 
Hoja Hafifu kabisa..
Mawakala tayari wameaminika na Vyama vyao na sidhani kama kuna uhitaji wa kua na simu kwenye vituo na sidhani kama sheria inaelekeza kufanya hivyo.
kuna utwasikia wakisema ucahuguzi huu lazima tunashinda ukiwauliza mnashindaje bila soni utasikia '' Tutaiba" . Mwizi lake giza na kificho. Mbona chaguzi za ndani za vyama zilionyeshwa mbashara. Iweje uchaguzi uwe siri?
 
Hawa maaskofu wengine wa aina hii sijui wanapatikana kwa vigezo gani imagine huyo anayesema hayo ni askofu anaetegemea kuongoza kondoo zake katika njia ya kwenda mbinguni sijui anawaza nini manake kwenye kituo Kuna mawakala na hata wagombea wanaweza kuwepo Sasa suala la. Kusema mawakala wapige picha matokea sijui haoni impact yake badae kuwa kila wakala anaweza kuwa na version yake ya kura kwa kweli viongozi wetu wa dini kuweni makini kwa dhamana mlio nayo ni kubwa Sana msitake sasa waumini tuanze kugawanyika kwa kuonyesha dhahiri mna ushabiki wa kisiasa ni vyema mkahubiri amani na kuombea uchaguzi uishe salama msiwe vyanzo vya vurugu manake hata nyie mtakua wahanga
Unakasirika kwa kusema ukweli?
 
Hiyo ni kanuni ya tume, na chama chako chadema walisaini fomu ya maadili ya uchaguzi! Na walikubali, Sasa wewe askofu mchunga siasa unapinga Kama Nani?

Viongozi wa dini Leo walikuwa ukumbi wa Mwalimu Nyerere wakati Rais anapokea gawio la billion 100!!
Wewe endelea na siasa, siku ya mwisho Mungu atakuuliza haesabu yake
Kama MTANZANIA ,
 
Wewe uliona wapi hicho kifungu katika kanuni za maadili ya uchaguzi kinachokataza simu au ndo porojo zenyewe?
 
SUALA LA SIMU KWA MAWAKALA: TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI MSIHARIBU UCHAGUZI WA WATANZANIA!

Taarifa kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itazuia Mawakala wa Vyama kuingia na simu zao katika vituo vya kupigia kura imetushtua hata sisi viongozi wa Kanisa! Simu ina mambo mengi sana katika ulimwengu wa sasa ikiwemo kutunza kumbukumbu kwa njia mbalimbali.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi haiwezi kuwafanya mawakala kama 'tabula rasa' yaani watu wasioweza kuhifadhi kumbukumbu yo yote na hata kushindwa kuwasiliana. Mawakala wakiwa na simu wanaweza kupiga picha matokeo halisi ili kudhibiti wizi wa kura! Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuzuia Mawakala kuingia na simu katika chumba cha kupigia kura ni sawa na kuandaa usiri utakaopelekea mazingira ya kuibiwa au kuchakachuliwa kwa kura!

Tunaitahadharisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuacha kutoa maelekezo au kutunga kanuni kwa lengo la kufanya Matokeo ya Uchaguzi Mkuu yasiheshimike na wananchi! Ili kuleta afya ni vizuri maelekezo na kanuni za Tume zikubaliwe na vyama vyote. Tume iepuke kutoa kanuni na maelekezo katika kipindi hiki kwa lengo la kuubeba upande mmoja na kuunyonga upande mwingine!

Sisi tumekwisha kutimiza wajibu wetu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
Mbona mwakataza simu kanisani mnakuwa mnaficha nini? Mbona mahakamani, benki, n.k simu zinakatazwa? Tena nilichoona 2015 kituo sinza A, simu hazipaswi kuingizwa kituoni kabisa zinasambaza uongo mwingi. Aidha TCRA wawe madhubuti katika kushughulikia wasambaza uongo.
 
Back
Top Bottom