Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mwanzo mwanzoni,natoa taarifa hii si kama Kiongozi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika,yaani TLS. Natoa taarifa hii kama Wakili Msomi wa kawaida sana ambaye ningefurahi kuona Mawakili Wasomi wenzangu wote wanaipata taarifa hii popote walipo. Nimeipata taarifa hii katika Ofisi za chama chetu.
Kwanza, Mawakili Wasomi wote waliokubaliwa na kusajiliwa tarehe 6/12/2013,wafike Ofisi za TLS kuchukua vitambulisho vyao. Kwakuwa viko tayari.
Pili, kwa Mawakili Wasomi wa miaka mingine, malipo ya kila mwaka ya ada za kiuwakili yanaendelea na yanakaribia mwisho. Kwa taarifa nilizonazo,mwisho ni tarehe 1/2/2014. Malipo haya,kama ijulikakavyo, huwezesha mambo mawili.Mosi, kupatiwa cheti cha kuendesha shughuli za kiwakili kwa mwaka husika,yaani 2014 ( Practising Certificate). Pia, huwezesha kupatikana kwa vitambulisho vya kiwakili.
Malipo haya huzingatia alama za kiwakili ambazo hupatikana katika Semina,Mikutano na kadhalika ifanyikayo kwa mwaka mzima. Alama zinazowezesha Wakili Msomi kupatiwa cheti na kitambulisho ni 10 na kuendelea.Kwa wale walizonazo,walipe ada zao na kufuata taratibu nyinginezo zipasazo. Kwa wasiofikisha alama 10, wanapaswa kuandika barua ya kuelezea kwanini hawakufikisha alama husika na tena kuahidi kuzilipia mwaka huu.
Aipataye tarifa hii,amwarifu na mwingine
Aione: Ruttashobolwa, 'The Choosen' John Mnaku B. Mhozya, MsandoAlberto, VUTA-NKUVUTE na wengineo