Taarifa kwa Mawakili Wasomi wote

Taarifa kwa Mawakili Wasomi wote

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mwanzo mwanzoni,natoa taarifa hii si kama Kiongozi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika,yaani TLS. Natoa taarifa hii kama Wakili Msomi wa kawaida sana ambaye ningefurahi kuona Mawakili Wasomi wenzangu wote wanaipata taarifa hii popote walipo. Nimeipata taarifa hii katika Ofisi za chama chetu.

Kwanza, Mawakili Wasomi wote waliokubaliwa na kusajiliwa tarehe 6/12/2013,wafike Ofisi za TLS kuchukua vitambulisho vyao. Kwakuwa viko tayari.

Pili, kwa Mawakili Wasomi wa miaka mingine, malipo ya kila mwaka ya ada za kiuwakili yanaendelea na yanakaribia mwisho. Kwa taarifa nilizonazo,mwisho ni tarehe 1/2/2014. Malipo haya,kama ijulikakavyo, huwezesha mambo mawili.Mosi, kupatiwa cheti cha kuendesha shughuli za kiwakili kwa mwaka husika,yaani 2014 ( Practising Certificate). Pia, huwezesha kupatikana kwa vitambulisho vya kiwakili.

Malipo haya huzingatia alama za kiwakili ambazo hupatikana katika Semina,Mikutano na kadhalika ifanyikayo kwa mwaka mzima. Alama zinazowezesha Wakili Msomi kupatiwa cheti na kitambulisho ni 10 na kuendelea.Kwa wale walizonazo,walipe ada zao na kufuata taratibu nyinginezo zipasazo. Kwa wasiofikisha alama 10, wanapaswa kuandika barua ya kuelezea kwanini hawakufikisha alama husika na tena kuahidi kuzilipia mwaka huu.

Aipataye tarifa hii,amwarifu na mwingine

Aione: Ruttashobolwa, 'The Choosen' John Mnaku B. Mhozya, MsandoAlberto, VUTA-NKUVUTE na wengineo
 
Ngoja niwahi fasta nikalipie!!! Asante sana kwa taarifa mkuu. Ngoja nimtumie taarifa rafiki yangu ili awahi hukoo kulipia.
 
Msomi mwenzangu Petro Eusebius Mselewa, asante sana kwa taarifa ya kutukumbusha kuhusu jukumu hilo la kulipia ada zetu za uwakili. Ofisi imepanga kuyakamilisha hayo yote kesho, Mwenyezi Mungu akitupa uhai. Naendelea kufurahia ushindi wa kesi ya Jamhuri dhidi ya Samson Maingu Mwigamba. Karibu tufurahi pamoja
 
Du, Wakili Msomi imenimaliza nguvu. Wasiosoma wanajiita Ma-Profesa Maji Marefu na wasomi wanajiita WASOMI. Sijui kujiamini kumepotelea wapi? Mwisho tutaona watu wanatembea na Tatuu usoni, MIE Ni Dr wa Ukweli (PhD).

Mwigulu na yeye anajiita Mchumi wa Daraja la Kwanza.... teteteeeee.......
 
Mbona ni hivi karibuni tu ndiyo nimeanza kusikia hiki cheyo cha WAKILI MSOMI ni kipya? Hii inatofautiana nini na wakili mwingine aliyehitimu vizuri LAW SCHOOL?
 
Nahisi soon tutaanza kuona PROFESSOR MSOMI!!!
 
Siasa imeingia kwenye weledi sasa imekuwa taabu sana, sasa hao mawakili wasomi wamesajiriwa na nani? haya bana ila ntapenda mnisaidie kwanini Umoja wenu Unahitwa Tanganyika sio Tanzania refer: Tanganyika Law Society (TLS)
 
Du, Wakili Msomi imenimaliza nguvu. Wasiosoma wanajiita Ma-Profesa Maji Marefu na wasomi wanajiita WASOMI. Sijui kujiamini kumepotelea wapi? Mwisho tutaona watu wanatembea na Tatuu usoni, MIE Ni Dr wa Ukweli (PhD).

Mwigulu na yeye anajiita Mchumi wa Daraja la Kwanza.... teteteeeee.......

Yaani we acha tu.

Eti wakili msomi. Wamesoma nini hao ambacho wengine hawajasoma?

Mami na wewe kwa nini usijiite mhandisi wa ukwee aliyesomea majuu?:biggrin1:
 
Kwanza, Mawakili Wasomi wote waliokubaliwa na kusajiliwa tarehe 6/12/2013,wafike Ofisi za TLS kuchukua vitambulisho vyao. Kwakuwa viko tayari.

Kwa nini mnapenda kujiita mawakili wasomi? Msipojiita hivyo watu hawatajua kama nyie ni wasomi au? Kuitwa wakili tu peke yake haitoshi?

Na nyie ndo mmesoma sana kuliko wengine au inakuwaje? Na kuna mawakili ambao sio wasomi?

Wapuuzi kabisa nyie watu. Jaribuni kuwa na humility hususan ukizingatia mambo yenyewe mmeiga iga tu kutoka nchi zingine.
 
Na Madokta wasomi, wahandisi wasomi, wahasibu wasomi, walinzi wasomi, wacheza shoo wasomi....

Ni full ujinga na upuuzi tu, if you ask me.

Kula like ki-manually mkuu NYANI!! Upuuzi mtupu bin ulimbukeni!!
 
Back
Top Bottom