Taarifa kwa Umma: China na Tanzania kuimarisha ushirikiano

Taarifa kwa Umma: China na Tanzania kuimarisha ushirikiano

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,086
TAARIFA KWA UMMA

CHINA NA TANZANIA KUIMARISHA ZAIDI USHIRIKIANO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China Nchini Tanzania Bi. Wang Ke. Mazungumzo hayo yamelenga katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizi mbili.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 12 Desemba, 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

"China tumeongea na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu malengo yetu ya kiuchumi ya muda mfupi na muda mrefu, na Katibu Mkuu ametueleza malengo ya maendeleo ya Tanzania kwa mwaka 2021-2025 na 2021-2030, tumepata kufahamiana vema kila mmoja wetu na sasa ushirikiano wetu utaimarika zaidi." Balozi Wang Ke


Screenshot_20201213_212418.jpg


Balozi ameongeza zaidi kwa kusisitiza kuendeleza ushirikiano kati ya Chama Cha Kikomunisti cha watu wa China (CPC) na CCM, na China wanautazama ushirikiano wetu kama ni wenye manufaa makubwa kati ya mataifa haya mawili kwa siku za mbeleni.

Screenshot_20201213_212725.jpg


Wakati huo huo, Katibu Mkuu akifafanua kwa ufupi mazungumzo hayo, ameeleza kuwa, yamelenga agenda ya maendeleo katika nchi yetu na ushirikiano wetu wa kihistoria kati ya China na Tanzania na kati ya CPC na CCM, hasa ushirikiano katika sekta za uwekezaji, Afya na Elimu ya ufundi ili kukuza soko la ajira, kama Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ilivyoahidi.

Aidha, Katibu Mkuu amepokea salama za pongezi kutoka serikali ya China kwa ushindi mkubwa wa CCM na kwa kuendesha uchaguzi wetu kwa gharama za ndani, jambo ambalo ni geni kwa mataifa mengi ya Afrika.

Huu ni utaratibu wa viongozi wa Chama kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine yenye dhamira na nia njema kwa Nchi yetu.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 

Attachments

  • Screenshot_20201213_212725.jpg
    Screenshot_20201213_212725.jpg
    45.4 KB · Views: 10
Mafuta ya kula lita sh 6000/=
Wewe endelea kujitekenya na kucheka mwenyewe.
Kwanini sasa ununue mafuta ya kula wakati unaweza kulima maalizeti na karanga kisha ukachuja mafuta yako madumu kadhaa ukapata mafuta.

Badala ya kulalamika nenda kakodi shamba lima malizeti na karanga. Ndio kipindi chenyewe hiki ukishavuna kachuje mafuta.
 
Huwezi endelea kwa kuwa kisiwa
Huwezi endelea bila mabeberu

Tanzania haiwezi wala haitaki kuwa kisiwa

Kinachotakiwa ni maridhiano kwenye biashara na ushirikiano. Na Sio kwamba washirika toka Ulaya na Amerika hawatakiwi.

Wasiotakiwa ni Mabeberu.... Beberu yoyote awe anatoka Asia, Africa, America, Europe hafai

Mabeberu sio watu powa

20201118_230335.jpg
 
mambo ni yanazidi kupamba moto kwelikweli.
tunazidi kutekenya roho za watu. zinatekenyeka kwelikweli.

Kwani ushirikiano na China uliwahi kuharibika? Ifahamike Tanzania haina mahusiano yoyote mabaya na nchi isiyoihoji kuhusu wizi wa kura, utawala bora na demokrasia.

Lakini asukudanganye mtu wachina wanatuchora tu. Toka wamekosa ile dili ya kujenga bandari ya bagamoyo ya $10b, na ujenzi wa SGR wa $7.5b wametutoa maanani.

Hapo ilipo kama wataongea miradi au misaada, ni ile isiyovuka $100m, ambayo ni miradi midogo mno. Kwa ujumla hao wachina kwa sasa hawana muda na serikali zisizolinda matakwa yao, wanachofanya ni kupiga picha na viongozi wa ccm wanaovaa Kaunda suti bado na porojo kibao.

Viongozi wa China wa maana wanaenda ulaya na Marekani kutafuta wawekezaji wa maana waende kwao kuwekeza. Wakishapata hao wawekezaji, bidhaa reject ndio wanaleta kwetu.
 
Back
Top Bottom