Kwani ushirikiano na China uliwahi kuharibika? Ifahamike Tanzania haina mahusiano yoyote mabaya na nchi isiyoihoji kuhusu wizi wa kura, utawala bora na demokrasia. Lakini asukudanganye mtu wachina wanatuchora tu. Toka wamekosa ile dili ya kujenga bandari ya bagamoyo ya $10b, na ujenzi wa SGR wa $7.5b wametutoa maanani. Hapo ilipo kama wataongea miradi au misaada, ni ile isiyovuka $100m, ambayo ni miradi midogo mno. Kwa ujumla hao wachina kwa sasa hawana muda na serikali zisizolinda matakwa yao, wanachofanya ni kupiga picha na viongozi wa ccm wanaovaa Kaunda suti bado na porojo kibao. Viongozi wa China wa maana wanaenda ulaya na Marekani kutafuta wawekezaji wa maana waende kwao kuwekeza. Wakishapata hao wawekezaji, bidhaa reject ndio wanaleta kwetu.