Taarifa kwa Umma: China na Tanzania kuimarisha ushirikiano

kampeni za udikteta πŸ˜‚ yaani unataka kuleta maendeleo unaongea na chama cha siasa badala ya kuongelea miradi.
 
kinachofanyika inasemekana ni kutekeleza ndoto za Nyerere.
Lakini mbona Mwalimu Nyerere alikuwa shatoka huko? Kwani sio Nyerere aliyehimiza uwepo wa vyama vingine vya siasa?
 
Vilevile anaweza kulima Karanga ardhi yetu inaruhusu, unakaria makapi ya Mafuta. Ndiyo maana kutwa kisukari,Presure na Magonjwa mengine ya kusendeka
 
Binafsi siungi mkono hoja kwa nchi maskini za Afrika kushirikiana na China kwa sababu;
1. China ni mnyonyaji asiye na chembe ya utu kama mabeberu ya Ulaya
 
Hao wanaishi tu nyumba moja kuua soo ya hicho cheo, lakini kimitazamo ni nguruwe na msikiti.
Kama unaamini kwamba wameweza kushirikiana kuua soo.... na uamini pia kwamba hao ni kitu kimoja. Usidanganyike
 
Inawezekana hilo kufanyika.
 
Kwani hao wazungu ni marafiki? Waliyoyafanya tumejionea+ukoloni.......acha tudunde kwingine
Bora hao wazungu walikuwa wanatudanganya kwa kutujengea shule, hosipitali, Vyoo, na kufadhili baadhi ya miradi, mpaka sasa utasikia kwa hisani ya USA

Wachina wamejaza maguruguru yale unadumbukiza shilingi 200 na yamejaa mpaka vilabuni, sijui ndiyo yanainui uchumi wa Tanzania
 
Kitu kimoja tukielewe tu sahizi ni namna ya kudeal na wote maana huwezi sema utajitegemea mwenyewe kwa sasa ni lazima uchague A au B mda mwngne ni AB Mchina kama hujielewi anakutandika kweli huku hawa wengine wanakujaga kwa juu na rangi nzuri nzuri huku chini wanafanya ushetani wao haya magonjwa wametuletea huku+ukoloni+utumwa........ishu ni kujitambua wenyewe tu
 
Hiyo iko sawa kabisa kwa mtindo wa chama chao cha kikomunist wanaojitahidi sana kuwafundisha CCM. CCM sasa hivi imo mafunzoni.
 

Hapa umeweka kisu kwenye mfupa. Sina la kuongeza.
 
Hao wazungu na ubeberu wao wameshaua raia wangapi Afrika tokea huyo Marekani awe kinara wao.........Mchina mambo ya ndani kwako hana shida na wewe tofauti na hao Wamagharibi wanataka kuku control hadi jinsi ya kuwaza
 
Hao wazungu na ubeberu wao wameshaua raia wangapi Afrika tokea huyo Marekani awe kinara wao.........Mchina mambo ya ndani kwako hana shida na wewe tofauti na hao Wamagharibi wanataka kuku control hadi jinsi ya kuwaza
Hebu sema tena? Eti "Mchina mambo ya ndani kwako hana shida na wewe"? You can't be serious.

Wewe huoni tunavyonyongwa na vikaragosi wao, au una maana gani? Unasubiri mchina alete manowari pale mlangoni petu kuzuia kila aina ya bidhaa tunazopata kutoka nje?

Huo ni mchezo wa kizamani mkuu. Yeye atawatumia madikteta wetu kumfanyia kazi yake, na beberu wazee wakipiga vikelele, yeye ndiye kinga ya hao madikteta wanaomfanyia kazi zake za kutukandamiza ili tulainike, na yeye apate anachotafuta.

Hapa kwetu anajua CCM ndiye askari wake, kwa hiyo atamlinda kwa nguvu zote. Ndio maana unaona kila siku CCM na china ni pete na kidole. CCM analinda maslahi ya mchina, na mchina analinda maslahi ya CCM.
 
Habari njema sana hii kwa Tanzania na wote wenye mapenzi mema

Habari mbaya kwa mabeberu[emoji16][emoji16]
Sasa ndio wapinzani waelewe kwanini sanctions imeshindikana[emoji1787][emoji1787]
Kuna beberu hatari zaidi ya hao wenye macho yaliyovimba? Kawaulize wazambia!
 
CCM na serikali ya China? Ni uhusiano gani huu? Sina nia mbaya ila naomba tu kuelimishwa...
 
Wachina walishakuwa ndugu zetu wa damu. Hongera kwa Mao Tsetung na JK Nyerere. Wachina hutupa msaada na mikopo nafuu mikubwa kimya kimya. Hutaona kwenye vyombo vya habari hususan TV tunaweka saini kupokea misaada au mikopo hiyo hadharani kama tufanyavyo kwa nchi au taasisi zingine za kimataifa. Misaada ya China haina mashariti ye yote na unazitumia kwenye eneo lo lote unalopenda. Mikopo yao ina grace periods za kuanzia miaka 30 na kwa kawaida baada ya miaka hiyo wanakufutia deni. Hivi ndivyo ilikuwa kwa mfano kwenye ujenzi wa reli ya tazara na bomba la mafuta la tazama.

Nyie endeleeni na urafiki wenu wa makelele kati ya CDM na hao IDU wenu. Sisi uhusiano wetu kati ya CPC na CCM hauna makelele.
 
Siyo habari. Kufikiria China itajenga Afrika kupitia uwekezaji ni kujidanganya. Viongozi wa China wapo busy muda wote kutafuta wawekezaji toka Ulaya.

Nchi inayoongoza kwa kuwekeza nje ya nchi ni Netherlands, ilitakiwa tuelekeze nguvu zetu huko.

Uchumi wa China umebadilishwa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji wa mataifa tajiri ya Ulaya na America nchini China, na siyo kwa uwekezaji wa ndani wa wachina wenyewe.

Mugabe aliamini China ingeziba oengo la mataifa ya Ulaya lakini alikuja kuujua ukweli baadaye kuwa China si lolote si chochote.

China yenyewe sasa hivi ukuaji wa uchumi umeporomoka toka 12% moaka 2% kutokana na kubanwa na Trump. Na hiyo ilikuwa kwa bidhaa chache tu zinazoingia US.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…