Kampeni zinaendelea, CCM chama changu mmejifungia sijua wapi. Kila siku Polepole anaitisha waandishi wa habari kuwaeleza yaleyale, kwanini tusimkemee na kumfundisha namna ya kutengeneza habari zinazouza? Jambo likirudiwa mara kwa mara kwa njia ileile hata Kama ni zuri linaboa.
Press kila siku hazina tija kwa wapiga kura wala wanachama, tunatamani tukimbie Kama wanavyokimbia wenzetu huku mtaani.
Kampeni za Lisu yupo peke yake bila usaidizi wa Mbowe wala figure kubwa ya chama na anatoboa, sisi tunakwama wapi?
Kwanini tumepoteza mvuto kwa wapiga kura? Kwanini tusitumie mbinu kuwajua wanaotuhujumu na kukaa nao meza moja ya maridhiano kuliko kuwatisha?
Uanachama Ni haki ya mtu, tuwarudie tuliowakata na kuwaomba radhi ili wakasimame majukwaani na sisi. Muda unaotumia kufanya press ungetengeneza maridhiano ndani ya chama na kukubali kwamba ninyi watu wachache amwezi kushinda uchaguzi Wala kuwavutia watu wawachague.
Mlishawatukana Watanzania, mliwaambia wabunge wetu wasiguswe hata wasipofanya chochote na wao wakabweteka kwa sababu tulisema wasiguswe. Tulidhani wanaoumia ni wapinzani kumbe mliwaumiza Watanzania, wabunge wetu walichaguliwa na wananchi na si wapinzani, ombeni radhi kwa kuwadharau wapiga kura.
Achana na press fanyeni Mambo yanayoonekana Kama wenzenu, wao wamesoma wapi Hadi wawe na upeo mkubwa kiasi hiki? Sisi tunakosaje wanamikakati Kama walivyo CHADEMA?